Sunday, June 01, 2014

Mama Mzazi wa Mh. Zitto Kabwe Afariki Dunia

Mh. Zitto Kabwe amefiwa na mama yake mzazi Bi Shida Salum.  Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.

KUSOMA KUHUSU MAISHA YA BI SHIDA SALUM BOFYA HAPA:

Taarifa kutoka Facebook:

My mother has just passed away. Inna lillah wainna illaih raajiun
Marehemu Bi Shida Salum, alikuwa mama mzazi wa Mh. Zitto Kabwe
 
  Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Kabwe akiwa na mama yake Mama Hajjat Shida Salum, enzi za uhai wake.


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania, (CHAWATA), Shida Salum, ambaye alikuwa mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na

Maendeleo, CHADEMA, aliyekuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Ami, Masaki, Dar es Salaam akisumbuliwa na maradhi ya saratani, ameaga dunia.

8 comments:

Jabir said...

Innalillah Wainnailayh raj'uun.

Mhe. Zitto stahmili kwa msiba wa Mama mpenzi. Mimi na familia yangu tunakuombea kwa Allah akupe ww na wanafamilia moyo wa subira ktk kipindi hichi cha msiba. Na Inshaallah ampumzishe marehemu Mama Shida kwa salama kwa kumfutia madhambi yake.

Sote tutakufa na kwake allah tutarejea. Atupe safari ya amani.

Jabir

Anonymous said...

Pole sana mheshimiwa zitto kabwe

Anonymous said...

Apumzike kwa amani Mama Shida:Mola amuweke mahala pema,na ampunguzie
adhab Kabri mpaka siku ya kiama ambayo hatujui i lini

John K. said...

Poleni sana Zitto, familia, jumuia ya walemavu, Wanaharakati na CHADEMA.

Anonymous said...

Pole sana Mh. Zitto na familia kwa ujumla, Mungu awape moyo wa uvumilivu wakati wa majozi haya makubwa.

Anonymous said...

To Hon. Zitto Kabwe and Family,

Please accept my sincerest condolences for the tragic loss of your dear mom.

I hope that the Lord will give you the strength and the wisdom to weather these difficult and sad times.

May the good Lord Rest her Soul in Eternal Peace.

Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un

Anonymous said...

Lala Salama Mama Shida Salum. Hapa hatuna mji udumuo bali tunautizamia ule ujao. Pole Zitto , Marafiki zako tuko na wewe katika kipindi hiki kigumu mno maishani. Endelea kumtumaini Mungu huku ukiamini kuwa kila nafsi itaonja mauti.
Jifariji na maneno haya kutoka kwenye Biblia takatifu.
"Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika,wakaa milele. (ZAB 125:1)

Anonymous said...

pole na pole sana mhe Zitto, Mungu akupe nguvu za kuhimili msiba huu mzito