Saturday, June 21, 2014

Ajali Mbaya Imetokea Lugalo Leo - Watu Saba Wamakufa


 Taarifa na picha kitoka kwa Mdau OS:


Ajali mbaya ya gari imetokea mchana huu, katika maeneo ya Lugalo jijini Dar es Salaam. Katika ajali hiyo, inakadiriwa zaidi ya watu saba wamefariki dunia.

Mashuhuda wanasema, ajali hiyo imesababishwa na gari aina ya dalala iliyokuwa ikitokea maeneo ya Tegeta kuja Mwenge. Gari hiyo ililigonga dalala nyingine kabla ya kulivamia roli na baadaye gari nyingine aina ya Toyota Discover.

2 comments:

Anonymous said...

wazo la kupanua barabara tumeshachelewa kidogo kwani itahusisha ubomoaji wa mali za watu na hakuna aliye tayari kutoka barabarani watakimbilia mahakamani na mradi utakwama.

Kuhusu kutumia mabasi mapya na makubwa hili ni wazo zuri, tuwaombe hunday na youtong wajenge assembly plant za mabasi makubwa na mapya, ili mabasi yale yapatikane kwa bei nafuu. Pia miradi mikubwa ya ujenzi ielekezwe nje ya mji.

Tuhamishe baadhi ya maofisi, mfano wizara ya mambo ya ndani, wizara ya elimu na wizara ya nishati na madini zihamie mbweni jkt, na majengo yale wapewe ifm yawe madarasa na mabweni.

Tuangalie uwezekano wa kuanzisha ''corporate street'' yaani tutenge eneo maalumu la uwekezaji wa majengo kwa ajili ya maofisi mahili, eneo hili litakuwa na majengo kuanzia gorofa ishirini lakini yenye nafasi ya kutosha maegesho yakutosha, miundombinu ya uhakika.

Anonymous said...

Poleni sana mliopotelewa na ndugu na waliojeruhiwa. Tunahitaji kuwabana zaidi wanaotoa leseni za udereva. Ziwe za halali. Pili tutumie magari mapya. Daladala nyingi ni mbovu sana. na ni chakavu hazistahili kubeba abiria kabisa. Anyway najihangaisha. Wacha tufe tu hakuna jinsi.