Wednesday, June 25, 2014

Mbunge Shukuru Kawambwa Yuko Canada - Hajafa! Ilikuwa Uzushi

 
Mb. Shukuru Kawambwa

Kutoka Facebook

TAARIFA TOKA BAGAMOYO
Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.

UKWELI
Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.


5 comments:

Anonymous said...

Habari iliyotufikia hivi punde ni kuwa waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi wa Tanzania mh. Shukuru Kawambwa amefariki dunia.... Bado tupo katika mchakato wa kuthibitisha hili... tumempigia simu ila haipokelewi. Inasemekana alikuwa safarini kuelekea mkoani Mwanza na amepata mshtuko wa ghafla..

Anonymous said...

Taarifa hizo sio.kweli Dr. ni mzima na.bukheri wa afya. Yuko Ubeligiji kikazi

Anonymous said...

Huu ni uchuro tu Dk Kawambwa yupo hai!

Anonymous said...

Aanatafuta nini katika nchi zote hizo?

Anonymous said...

Tanzanians, do not be dismayed, this and many more will come and go towards 2015 elections.