Thursday, September 06, 2007

Maneno ya Hoyce Temu juu ya Ushindi wa Richa

Top Photo from Jiachie Blog
Hoyce Temu (Miss Tanzania 1999)

From Haki Ngowi Blog:

HOYCE Temu, mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999, amesema hapingi taji la Miss Tanzania kwenda kwa Richa Adhia kutokana na rangi au asili yake, bali mrembo huyo hana sifa na vigezo vya kuvikwa taji hilo.

Hoyce alisema hayo jana kwenye Ukumbi wa Haidery Plaza, ikiwa ni siku tatu baada ya kufanyika kwa shindano hilo na Richa kuvikwa taji la Vodacom Miss Tanzania 2007.

Muda mfupi baada ya Richa kuvikwa taji, Hoyce alifikia hatua ya kububujikwa machozi kwa kile alichosema na anachoendelea kusisitiza kuwa, mrembo huyo hakustahili kutwaa taji hilo. Kitendo hicho cha Hoyce kilitafsiriwa kwa maana mbalimbali, huku wengine wakimlaumu kwamba mrembo huyo wa mwaka 1999, ameonyesha ubaguzi kwa sababu anampinga Richa kwa asili yake.

Akifafanua msimao wake jana, Hoyce alisema hampingi Richa kwa uasili au rangi yake, bali hakustahili kuvikwa taji hilo, isipokuwa mrembo namba mbili hadi wa tano. Walioshika nafasi hizo katika shindano hilo lililofanyika kwenye viwanja wa Leaders Club ni Lilian Abel, Queen David, Victoria Martine na Khadija Sulla.

Hoyce alisema kilichotokea katika shindano hilo, kinatishia kutekwa kwa maudhui halisi ya uwepo wa shindano hilo nchini kutokana na baadhi ya wadau kujali zaidi lugha ya kigeni katika kujibu maswali.

“Sikuona kigezo chake cha kumfanya achaguliwe kuwa Vodacom Miss Tanzania mwaka 2007, kwani inaonekana wazi wadau kuangalia zaidi lugha ya kigeni katika kujibu maswali baada ya kuipa kipaumbele lugha yetu.“Napenda nieleweke kuwa simpingi Radhia kwa uasili au rangi yake, bali ninahoji vigezo vilivyomfanya hata akavikwa taji kwa sababu hana hadhi aliyopewa ya kuiwakilisha nchi katika shindano la kimataifa,” alisisitiza Hoyce huku akionyesha masikitiko.

Alisema kilichomliza siku ya shindano, si suala tu la Radhia kutangazwa mshindi, pia ni kuona shindano zima la safari hii lilivyokuwa na upungufu mwingi. Hoyce miongoni mwa upungufu huo, anasema ni kukosekana kwa vazi la ubunifu wakati kila wakati imekuwa ikisisitizwa kuhusu suala la ubunifu wa vazi la taifa.

Alisema, hofu yake ni kwamba, kama hali hiyo itaendelea hivyo ya warembo kutoshindanisha ubunifu wao, kuna hatari hata utamaduni halisi wa Mtanzania ukamezwa na ule wa kigeni.

Alisema dosari nyingine ni utaratibu uliotumika katika kuuliza maswali, kwani kwa kawaida kapu la maswali linapopelekwa mbele, huwa halirudi nyuma hadi wote wamalizike, lakini safari hii wakati wa kujibu swali kwa mrembo Victoria Martin, kapu liliondolewa na baadaye karatasi ikatolewa tupu.

“Sipo hapa kwa ajili ya kutaka kumvua taji Richa, isipokuwa nipo kwa ajili ya kurekebisha haya, ili yasije kutokea miaka ijayo.“Na tunachotakiwa ni kuangalia Nancy alipungukiwa vigezo gani hadi kushindwa kuchukua taji la ‘Miss World 2005’, ili tuweze kuchagua ambaye ataweza kujazia vigezo hivyo na kurudi na taji hilo na si kurudi nyuma tena,” alisema kwa uchungu huku akionekana akitaka kulia.

Aidha, alisema kuwepo na utaratibu wa kutangaza mataji, kwani unapotangaza mapema mrembo aliyeshika taji jingine kabla ya taji la Tanzania, unamnyima haki yake ya kupigania taji lake, kwa kuwa atajua hataweza kushinda tena.

Vinginevyo anasema watangaze utaratibu wa kuwa mrembo anaweza kushinda taji la Miss Tanzania hata kama katangazwa kupata taji lingine.Pia alishauri kwa wanaopewa kazi ya kusimamia kambini wanatakiwa kuwa makini kuangalia warembo ambao wanatakiwa kushika taji hilo kwa uhalali

10 comments:

Anonymous said...

Nakupa hongera Chemi kwa kuwa 'fair'.
Jana ulimwaga sifa na pongezi kwa miss TZ na leo umetoa upande wa 2 kwa wale wanaopinga ushindi wake kuwa sio halali!

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 6:36am, nashukuru kwa maoni yako. Niliona hii story kwa Haki Ngowi, na niliona itakuwa vizuri kubalance kama unavyosema.

Richa amechaguliwa kwa mwaka huu. Hakuna kumvua taji lake. Tuombe afike mbali na awakilishe Tanzania vizuri huko mbele. Ingekuwa vizuri huko acheze ngoma ya kiafrika kama Sindimba au Sangula ila watu wamshangae zaidi.

Anonymous said...

Ningekuwa waziri naehusika na utamaduni ningeubatilisha uamuzi huu, shame on you TANZANIANS

Unknown said...

Unajua hata mimi ninafikiri kuchaguliwa kwa Richa was a strategic move.ushiriki wake utaonesha jinsi watanzania tulivyo multicultural, which is true.Kuna wabongo kibao wamechanganyika na waarabu, na watu walioa wahindi, na wazungu na watu walichanganyika na nchi kibao za kiafrika.

Mimi nimesoma sana habari mbali mbali kuhusiana na ushindi wake, watanzania wengi wameonyesha uracisim, kinachoshangaza ni kwamba watanzania hao hao wanachukia racist perceptions and actions wakiwa abroad and yet they are the first ones to display racist remarks tena kwa mwananchi mwenzao.

Richa is first and foremost very attractive, so is lilian abel who was my favourite, but Richa won and I accept that, tena wala hainiumi. Indians wamekuwa the focus of our anger simply because hatuelewi mambo mengi. Wahindi ndiyo waendeshaji wa viwanda vikumba bongo ambayo imeajiri wabongo kibao, wameanzia mashule mengi , mahospitali, na wanafnaya huduma za jamii nyingi pasipo ubaguzi. Truth be told as a community the indians are very well organised and networked, ndo maana wanafanikiwa. Wabongo inabidi tujifunze hii,and stop habouring racist perceptions.

This as nothing to do with miss tanzania, although her selection imeibua mjadala mpana. I hope that she does well in miss world, she certainly has the beauty, we should all suppot her.

Hoyce temu sijui alitaka ashinde nani, and the way she voice her comments was very, very unprofessional, that is way her conerns were brushed aside na kamati. She has her respect...atuliye nayo,and try not comprise it.

Anonymous said...

nakupinga wewe bwana unayesema eti amepewa ushindi kwa sababu ni stretegy maalum ya kuonyesha multiculturalism ya watanzania
ukisema hivyo basi ndio kusema ni kweli hoyce temu anapoint kwamba hakushinda kwa kuzingatia viwango husika vya kumpata mrembo ...

huyo dada ameshinda ninaassume ni kwa sababu amepita viwango vyote (irrespective of any rumors or any deficiencies in the whole process)

watanzania sisi ni wanafiki tena sana tuu nimeshasema mara kadhaa tabia moja ya mtanzania ni kujisifia. tunapenda kujisifia na japo hatujiwezi hatuna ubora ule unaopaswa kujisifia

ooh,tanzania hatuna ubaguzi ni wamoja hatuna ukabila ,nk yes it used to be ....way back in the 70's and 80's right now ni lazima tukubali kwamba tumebedilika na suala zima la ubebari .ubebari kiasili unakuja na individualism na mashenzi mengine mengi tuu.

huyo dada ameshinda na ni mtanzania kam wengine na anahaki zoote kama mtanzania wengine na watanzania we need to be receptive and supportive equally ushindi wake huko aendapo ni kwa ajili ya watz sote na si kwa ajili ya mshenzi lundenga au yule model wa nigeria (jaji)
talking about the falling legend ,who was hit with a meltdown kwa sababu ya ushindi wa huyu dada,hoyce temu ,kwa kweli nimeshangaa kiasi fulani si kwa sababau ya kutokubali matokeo .
kwa sababu imenifanya ni anze kukjiuliza what really happens behind the scenes ,behind the closed doors ya mashindano haya
je kuna mtu aliyemtegemea (kupangwa) kuwa ndie mshindi wa mwaka huu?je kuna corruption huko nyuma ya milamgo ?
to what extent anafahamu the evils and corrosion ya miss tanzania nyuma ya pazia? hii pia inanipa wasiwasi kwamba labda hata yeye hakushinda kweli kama vile sisi umma wa tanzania tunavyozani thus why the crowning of miss tz 2007 ,smacked her with a shock,disbelief ,no way!and chopped her with nothing short of a meltdown
ameshinda ,ameshinda tuondoe tofauti zetu tumsuppoert mtanznia wmenzetu bila kujali rangi ya ngozi yake
mmh! being a visible minority kweli si mchezo iko kazi kweli kweli ktk jamii yoyote ile

asanteni
Raceznobar
edmonton

Anonymous said...

Kwanini wasiweke vigezo vya ushindi vya wazi ili kila mtu anayeudhulia awe na haki ya kuchagua kulingana na sifa zilizowekwa badala ya kundi dogo la watu kusimamia na kutoa maamuzi ambayo kila mtu anaona wazi.tufike mahali watanzania tuwaachie wapenzi waamue nani anafaa badala ya kikundi kidogo cha watu ambao mara nyingine wanaweza kuwa na ajenda ya siri. ni kura tu za wapenzi zitumike mwisho kutoa maamuzi hii ingesaidia kwa namna kubwa kupunguza malalamiko.
asante sana Dada. chemi.
kwa nafasi hii nzuri.

nick mlay
University of Houston.

Anonymous said...

Stephen,wabongo wakiwa nje,hata wale waliozaliwa nje hawapewi nafasi tunazowapa sisi wadosi!Viwanda vya Tz vinaendeshwa na wadosi;ndio.. kwa vile miaka hiyo wakoloni waliwakumbatia na kutunyanyasa si wazawa,hivyo maendeleo walianza kuyapata wao kwanza, wengi wao wakaenda nchi za Ulaya(na sio India) kutokea huko wameweza kuendeleza zaidi comunity yao Bongo.Tumekuwa tunawapa nafasi hizi kwa kuwa tulikuwa na fikra finyu wengi walikuwa hawajaenda nje ya nchi kuona pia jinsi wenzetu wanavyo weka mbele wazawa wao!Angalia tuko wapi sisi sasa?Nataka sana kuona kama huyo Richa ataruhusiwa kuwa na boyfriend/mume mweusi!Halafu ndio uje unieleze nani kati ya sisi wabongo na hao minorities wana racist perceptions?!
Kama ni uzuri ni sawa kwamba ni mzuri lakini si uzuri wa Kiafrika,yeye si chotara wakibongo kama kina Mwisho!Hivyo bado tuko palepale kuwa hata kwa hayo hafai kuwakilisha Bongo.
Sasa hivi kila nchi inafagilia uzalendo wake,weusi nje ya Afrika wanabanwa wasifike juu na kama wanapewa nafasi ni only a few of them.
Nakubaliana nawe unapoandika kuwa tuige mfano wa wadosi katika organization;ndo tunafanya hivyo,ndio maana unasema tuache ubaguzi wadosi na waarabu ndo wenyewe"ALALAYE USIMWAMSHE..."Unataka tukipigwa kibao shavu moja tuachie na lingine lipigwe,hapana Asante.

Anonymous said...

Sijui kwanini lakini kinachonivutia sana kwa huyu dada Richa (Miss Tanzania), ni miguu yake na vidole vya miguu. I love her toes. Lazima nitamwambia nitapo onana nae jumapili inayokuja.

Anonymous said...

I know and have seen Richa (Miss Tanzania 2007) on Sundays and i must admit she s gorgeous. Good on her to win! to start with, she has very beautiful toes. Just look at them and see. Interesting enough is that i almost told her about her feet but was so embarassed.

I love her feet.

Anonymous said...

Richa hafai, huo ndo ukweli.