Monday, December 22, 2008

Ilitokea kweli - No. 1

Hapo zamani za kale, wabongo walichukuliwa kwa wingi na serikali ya USSR (Soviet Union) Urusi, kwenda kusoma huko.

Sasa si mnajua ubaridi wa kule. Yaani baridi hasa. Theluji na barafu kibao. Sasa kuna mBongo fulani, mwanaume alipenda sana kunywa vodka ya Urusi. Yaani baada ya kazi ngumu ya kubukua kazi kunywa vodka.

Siku moja baada ya kunywa alitoka na kawa anatembea barabarani. Theluji ilianguka kwa wingi mpaka jamaa akaona taabu kutembea. Aliamua kusimama na kupumzika kidogo mtaaani huko theluji inazidi kuanguka kwa wingi. Mwisho kalala hapo hapo alipokuwa.

Asubuhi yake, warusi walikuwa wanasafisha mitaa na kuzoa ile theluji iliyoanguka. Wakakuta maiti ya mwafrika mle kwenye snowbank (mlima wa theluji). Wakaita gari la kuja kuchukua maiti. Ile gari likaja na wakatia maiti ya mwafrika mle.

Kufika mortuary, wakailaza maiti mapokezi. Kumbe ile joto ndani ya gari la maiti na ndani ya jengo ilikuwa inafanya mambo. Jamaa ambaye alidhani maiti kakaa wima halafu kaongea Kiswahili! Wacha wazungu wakimbie!

Wataalam wanasema na sikumbuki vizuri lakini ilikuwa kama ile pombe ilipunguza metabolism sijui na ile theluji ilikuwa insulation ndo maana hakufa.

Nafurahi kusema jamaa alimaliza masomo yake Urusi na alirudi Bongo miaka ya 90.

2 comments:

Anonymous said...

Hadithi imeendelea tena kwani imetokea tena huko Oregon na jamaa nae anampango wa kurudi Bongo soon

Anonymous said...

na nyingine imetokea tena huko Mali kwenye jangwa la Sahara. na jamaa huyo hivi sasa anarudi bongo kwa kutumia ngamia.