Monday, November 16, 2009

Rais Obama Aonyesha Heshima Japan na Kuzua Zozo!

Yaani watu hapa Marekani wanadhani kuwa Marekani ndo nchi ya kuzidi nchi duniani. Kuna zozo sasa kwa vile Rais Barack Obama aliinama wakati anamsalimu Emperor Akihito wa Japan. Jamani, kuonyesha heshima kwa kufuata mila ya nchi unayotembelea ni kosa? Mimi nampongeza Rais Obama kwa kutambua na kuheshimu mila na utamaduni za nchi zingine.
Kwa habari zaidi someni:

8 comments:

Anonymous said...

Wamechukia kwa vile wanaona kama kashusha hadi ya kiongozi wa Marekani. MUCH RESPECT TO PRESIDENT OBAMA!

Anonymous said...

huyu jamaa anakili saani afu anaheshimu kila mtu.makaburu ndo wenye jeuri big up baraka hussein obama

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Jamaa wanasema haijatokea kwa rais wa Marekani kuwa anainamainama hovyo namna hii. Sasa Obama hii ni mara yake ya pili mwaka huu - kwanza aliinama mbele ya mfalme wa Saudi Arabia (ambaye wanamwona kama dikteta) na sasa ameinama tena kwa Mfalme Hirohito. Wanasema ni rais Nixon pekee ambaye alijaribu kuinama kidogo tu kwa Mfalme Hirohito zamani na hii iliwasha moto mkali sana.

Kwa wasoma ishara, hii tabia ya kuinamainama hovyo ya Obama eti wanaitafsiri kama kutokujiamini, kutokuwa na uhakika na hata kuwa kigeugeu. Wahafidhina akina Rush Limbaugh wameenda mbali hata kusema kwamba eti Obama naye ana mawazo ya "kidikteta" naye anatamani siku moja kuinamiwa na hata kuabudiwa. Wengine wanasema hii ni ishara kwamba dola la Marekani sasa linafifia na mwisho wake umekaribia (Uchina ndiyo inapigiwa upatu kunyakua ukiranja miongo michache ijayo).

Pengine ambacho hawakielewi ni kwamba huyu jamaa ana mizizi ya Kiafrika ambako kuonyesha heshima kwa wazee ni jambo la kawaida kulingana na utamaduni husika. Katika sehemu nyingi duniani pia kuinama kidogo wakati wa kusalimiana ni jambo la kawaida.

Mimi nadhani kelele hizi zote ni matokeo ya kiburi na "umbumbumbu" wa Kitamaduni wa Wamarekani - umbumbumbu ambao umewaingiza katika matata makubwa sana kule Iraq na Afghanistan. Inavyoonekana bado hawajajifunza!

Baada ya makelele yote haya sidhani kama Obama atainama tena

Anonymous said...

When you are in Rome you've got to do what the romans do. It's common sense. I've been living in Japan for nearly a decade now, I know what that means to them. Big up Baraka.

Anonymous said...

What is wrong with showing respect?

Kaghembe said...

Profesa Mbele tunaomba maoni yako juu ya hili kwani umeandika kitabu kinachoeleza juu ya migongano ya tamaduni. nadhani utakuwa na mengi ya kueleza.

Anonymous said...

Obama si wa kwanza kuinama, hata Rais George W Bush aliinama akisalimia mfalme mmojawapo Saudia.

Anonymous said...

kikwete kamfunda hayo.tehetehe