Wednesday, May 18, 2011

Tanzia - Mzee Habib Nyundo

(Pichani Mzee Habib Nyundo)

Nimepokea kwa masikitiko habari za msiba wa aliyekuwa Mwalimu wangu Tanzania School of Journalism (TSJ) miaka ya 1988-1990, Mzee Habib Nyundo. Poleni sana wanafamilia.

Mola ailaze roho yake mahala pema peponi. Amin.

***********************************************************


Tasnia ya habari imeendelea kukumbwa na misiba. Mzee Habib Nyundo (61) aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari –MAELEZO, amefariki dunia.

Taarifa ya Maelezo imemnukuu, ndugu wa marehemu Alhaji Marusu Msii Jijini Dar es Salaam akisema kuwa Mzee Nyundo alifariki jana saa tisa alasiri katika hospitali ya Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma alikolazwa kwa muda mfupi baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Mzee Nyundo alilazwa katika hospitali ya wilaya muda mfupi baada ya sukari kupanda ghafla na kujisikia vibaya wakati alipokuwa safarini kuelekea Dar es Salaam alipokuwa akitokea kijijini kwake Busi.
Marehemu Nyundo alistaafu kwa mujibu wa sheria tarehe 30 Aprili, 2010.

Poleni wana habari wenzangu, hasa watumishi wa Idara ya Habari Maelezo. Poleni sana na tutamkumbuka mzee huyu daima kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya habari nchini. Mungu mwenye rehema awape moyo wa uvumilivu wale wote walioguswa na msiba huu, hususan familia yake katika kijiji cha Busi, Kondoa.

Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors' Forum (TEF),

1 comment:

SIMON KITURURU said...

R.I.P Mzee Nyundo!