Wednesday, May 11, 2011

Sinema Maangamizi the Ancient One Iko You Tube!Kwa wasiofahamu, sinema ya Maangamizi the Ancient One ilipigwa nchini Tanzania mwaka 1994 na 1997. Mwaka 2001 ilikuwa sinema ya kwanza kutoka Tanzania kwenye Academy Awards (Oscars). Ilikuwa katika Forign Language category yaani sinema za lugha ya kigeni.

3 comments:

Anonymous said...

Asante DaChemi, kuna sinema moja ya zamani ilikuwa inaitwa Mlevi ilikuwa nzuri sana je inaweza kupatikana vipi na wapi najua wewe utakuwa unauwezo wa kufahamu hilo kwani iko kwenye tasnia yako

Chemi Che-Mponda said...

Nimewahi kusikia hiyo sinema, 'Mlevi' lakini sijui unaweza kuipata wapi. Una habari sinema zetu nyibngi za zamani zimepotea? Zimeoza, haziwezi kuonyeshwa tena Ukifungua kopo ni uji mtupu. Sinema ambazo zimesalia ni zile ambazo zilipelekwa nje ya nchi.

Kuna sinema, 'GUMU' ambayo ilitengenezwa mwaka 1934 na mkoloni. Nia ya hiyo sinema ilikuwa kuonyesha waafrika kuwa maisha ya mjini yalikuwa magumu hivyo ni bora wabaki kijijini. Sinema ilitengenezwa na Bantu Educational Kinema Experiment (BEKE) ambayo ilikuwa chini ya The International Missionary Council ya Waiingereza.

Anonymous said...

Asante sana dada Chemi. Nimefurahi sana kumuona Professor Amandina Lihamba akiwa kijana tena akiigiza. Nafurahi kuwa sasa ni professor wa fani hizo hapa udsm ninakofanya kazi pia.Pia wewe kumbe ulikuwa unaigiza. Nashukuru sana.
Nimefurahi