Monday, May 02, 2011

Osama bin Laden Ameuawa!Jana usiku nilikuwa nashangaa kwa nini majirani zangu wanapiga makelele za kushangilia sijui nini usiku wa manani. Leo asubuhi kuamka ndo nasikia kwenye taarifa ya habari kuwa wanajeshi wa Marekani wamefanikiwa kumwua Osama bin Laden huko Pakistan. Serikali ya Marekani ilijitolea kusafirisha maiti ya bin Laden kwao Saudi Arabia kuzikwa, lakini serikali ya Saudia walisema hawataipokea. Hivyo, maiti yake ilizikwa baharini kusudi watu wasipate nafasi ya kumwabudu.

Osama bin Laden alisababisha vifo vya maelfu ya watu. Atakumbukwa zaidi kwa maafa ya 9/11 mjini New York, lakini tusisahau kuwa kaua waTanzania na waKenya mwaka 1998. Tanzania na Kenya tulimkosea nini bin Laden?

Habari za kifo cha bin Laden ni habari njema. Ila tusisahau kuwa kuna wengi ambao watataka kumwiga na kuendelea kumwaga damu ya watu wasio na hatia.

6 comments:

emu-three said...

Duuh! Wapo wengi hawo, wakati nasoma hii, jamaa mmoja alikuwa akituhadithia lile bomu la Hiroshima, ...jamani dunia hii amani itakuja lini, tuache haya...kuuana, visasi , chuki!

Baraka Mfunguo said...

Isomeke Obama Bin Laden badala ya Osama Bin Laden.

Bongo Pix said...

Da Chemi hiyo tittle ndo ulivymaanisha au vidole vilipata kwikwi?

Chemi Che-Mponda said...

Wadau naomba samahani! Nimerekebisha. Nilikuwa nimesafiri jana kwenda kwenye msiba wa rafiki hivyo sikuwa na access ya computer.

Anonymous said...

Ding, Dong Osama's dead! Bado Gaddafi!

Anonymous said...

DAILY PRAYER TO OBAMA

we genuflect barack holy black jesus

born of biracial love in honolulu

worshiped by democrat masses

save us from the palin devil

perform miracle Gabby Giffords recovery

give us our daily healthcare bread

open red sea of immigrant borders

free us from corporate slavery

cast out wall street money changers

end republican global war crusades

save mother earth climate change

perform miracles of green technology

on your cross of tea party torture

bless you for eight years

Your prayer should be directed to the Navy Seals, they risked their lives to kill him, not your beloved Obama.
...