Monday, April 23, 2012

Lulu Mahakamani Kisutu Leo

 Mcheza sinema Elizabeth 'Lulu' Michael alifikishwa katika mahakama leo kuhusiana na kesi yake kuhusiana na mauji ya Bongo Star Steven Kanumba.  Kesi leo ilikuwa ni kutajwa tu yaani Mention.
Mcheza Sinema, Elizbeth 'Lulu' Michael, katika Mahakama ya Kisutu leo hii 23/4/12 (Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)  Kuona picha zaidi Mtembelee Kaka Michuzi


Katika hii picha ya Global Publishers Lulu anaonekana kuwa na kakitambi!   (picha kwa hisani ya Global Publishers)

MAELEZO KUTOKA GLOBAL PUBLISHERS

Mwigizaji Maarufu wa filamu za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo majira ya saa nne asubuhi amepandishwa kizimbani kwa mara ya pili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shitaka la kumuua Steven Kanumba. Baada ya kusomewa shitaka hilo na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama hiyo Elizabeth Kaganda mbele ya Hakimu Rita Tarimo hakutakiwa kujibu lolote. Mwendesha Mashitaka huyo alisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamailika hivyo kesi hiyo iliahirishwa mpaka Mei 7 mwaka huu.


23 comments:

Anonymous said...

hivi nikitambi au ndi mimba ya kanumba? pole sana my looove mungu atakusaidia najua hukupenda yakukute kama hayo.inshallah mumgu yupo.mungu wape wape wepesi wa kujua haki na batili juu ya mpendwa wetu lulu.

Anonymous said...

ni sehemu yamaisha jipe moyo na maombi kwa sana.

Pole sana kama kweli una mimba unapata wakati mgumu zaidi na hali hiyo.

Mungu yu nawe!!! usife moyo hakuna anayejua ukweli zaidi ya Mungu hata wewe umeshuhudia

Anonymous said...

hizo picha za hapo juu karibia zinitoe machozi! ni kipindi kigumu sana kwake hasa ukizingatia umri wake na tukio lenyewe analohusishwa nalo! Mwenyezi Mungu amsaidie tu! Mimi nilo tayari kumwoa akitoka kifungani!

JR said...

Polisi hao wote wa nini acheni kudanganya watu lulu hahitaji ulinzi huo wote.

Anonymous said...

Lulu mnafiki mkubwa! Hizo nguo ungevaa kabla ya tukio kutokea, usingefika hapo. unaonekana mtakatifu kumbe shetwani mtoa roho za wenzio.

Anonymous said...

Tanzania, Tanzania, Tanzania.......! Sasa haka kajitu ndo kanapewa escort ya namna hii!!!!! Huu ni ushenzi na upumbavu. alafu umaarufu wake ni nini!!!!! Tusipoacha upuuzi huu basi sote tutakuwa viazi

mafisadi wanapelekwa mahakamani kawaida ila aka kajitu ndo kanafanyiwa hivi? Hapa kanumba atatendewa haki. na yawezekana kanalala kwa J au R.

Anonymous said...

Pole yake, dila na ushungi kaujua. Ama kweli ulimwengu unamfundisha sasa. Hilo tumbo sidhani kama ni mimba, huyu tokea zamani tumbo lake lilikuwa kubwa. Kama ni mimba haifichiki, ipo siku itajulikana.

Anonymous said...

Some things can only happen in Bongo. Hivi hao maaskari wote ni wa nini? Huyu binti alisindikizwa na polisi na askari magereza si chini ya 20. Hivi hawa nia yao ilikuwa ni kumlinda Lulu au walitaka waonekane magazetini na kwenye TV?

Anonymous said...

Nobody killed Kanumba. The man was sloshed to his eyeballs when his lost his balance and banged his head on the floor. Wanamuonea Wema.

Anonymous said...

hana lolote wacha akome alisema akivaa nguo ndefu anawashwa sasa kiko wapi mbona kavaaa? ama kweli dunia inafundisha halaf hana uzuri wowote kumbe mpka ake uchi

Anonymous said...

Lulu, Je ule ujauzito uliopewa na Kanumba uliutoa ama? Natamani ujibu Yes, ili wengi wetu tufarijike, wala usishtuke na hilo swali. Lakini baada ya kuona hiyo picha naon a bado unayo!

Kabla Kanumba hajafa mwezi uliopita zilisambaa taarifa kuwa wawili hao wana mahusiano ya kimahaba, lakini wakakana, na kuhusu Lulu kuwa na ujauzito na Kanumba pia aliruka futi sita,
Sasa Leo hii ndo tumefahamu ukweli!

Anonymous said...

Lulu hanaga kitambi cha bia wala nini. Mama Kanumba subiri mjukuu. Inawezekana hiyo mimba nayo pengine ndio ilikuwa source ya ugomvi nasikia jamaa alikuwaga hapendi watu wajue kama ana mtoto nje. Isitoshe kipindi kirefu Lulu alikuwa haonekani kabisa si viwanja wala magazetini amejichimbia. Masikini Lulu, pole sana mdogo wangu.

Anonymous said...

KWAUFUPI HAKUNA BINADAM ALIYE KAMILIKA NA PILI SISI WABONGO TUSIPENDE KUSHADADIA VITU MALA OHOO ESCOT KUBWA MALA ETI LEO NDIYO KAKUMBUKA USHUNGI,MWACHIENI MUNGU NDIYE AUKUMU VIUMBE VYAKE TUKIWEMO MIMI NA WEWE!!!!!,KAMA HUNA DHAMBI ANZA KUSHIKA JIWE NA UMPIGE UNAEONA ANA DHAMBI,SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU MIMI JOFREY RUGIMBANA UWA NAJIONA NIMKOSAJI KULIKO WATU WOTE DUNIANI BUT CHA MSINGI TUOMBEANE KILA MTU NA DINI YAKE,MUNGU ATUBALIKI SOTE

Anonymous said...

Unajua watu wengine bwana huyo mtoto lazima apewe escort vinginevyo yatazuka mengine hapo hamuoni jinsi wanavyo mzingira?Pole mtoto Lulu Mungu yupo amini na utamaliza tu hayo ni mapito,bongo movies ndo wamemuacha???Inauma msihukumu msije hukumiwa.

Anonymous said...

Jamani twende mbele turudi nyuma huyo mtoto mtoeni tu, kama mauaji yashatokea, yangeweza kutokea hata kwa jali ya gari au vinginevyo, Da namwonea huruma tumbo na segerea sipati picha, Mbaya zaidi ukute hata baba wa mtoto hatambuliki,

Nameless said...

jamani mimi nina uchungu sana na huyu mtoto siyo sbb ya kuhusishwa na kesi ya
kanumba bali matendo yake ya nyuma ni machafu sana na pia kiburi, huyu si ndie
yule aliechanwa na wembe usoni katembea na mume wa mtu? mtoto huyu alistahili
kurekebishwa na mama yake maana jamii ilisha mshinda, kwanza maam lulu atueleze
lini alimkanya mwanae pale aliposema uongo tena kwenye media siyo mara moja ama
mbili mara kibao. lulu aliongopa ktk kipindi cha take one kuwa kamaliza shule
wkt hakuwahi kufika shule term nzima mpk mkuu wa shule st marry's akathibitisha
kuwa hajamaliza shule, huyu huyu alifanya party ya age 18 media zinatangaza,je
kama mzazi alichukua hatua gani?maana hapa tusitafute huruma ya watu wkt sisi
wazazi tunachangia watoto kuharibika, cha muhimu tusimuhukumu bali hili ni
fundisho kwa wazazi wote na lulu mwenyewe japo bbc walisema hakuonekana na
wasiwasi akiwa kizimbani lkn ni moyo tu amejipa apambane na hili. jamana tuache

Anonymous said...

police na uchunguzi tz ni zero. ndani alikuwa huyo lulu na marehemu, sasa sijui
yeye lulu kawaeleza vipi police mpaka wamempeleka mahakamani, ripoti ya
madaktari haijasema kwamba huyo marehemu kapigwa ama kasukumwa, imeeleza tuu
kwamba marehemu mekufa na tatizo gani na sababu zinazomfanya mtu akaumbwe na
hilo tatizo, sasa nadhani huyo lulu katoa maelezo gongana ndiyo maana hata
kafika huko mahakamani.

Anonymous said...

Hilo haliondoi ukweli kwamba kanumba ndio aliemuharibu huyu mtoto kwa kuanza
kumbaka akiwa bado mtoto wa miaka 14,hata kama tunampenda kiasi gani lakini
ukweli ni kwamba mpendwa wetu huyu alikua mbakaji na mungu kamuumbua,hili liwe
fundisho kwa wengine tunaofanya mambo kwa siri tukidhani tumejificha,mungu
anatyuona sema anatustahi tu anaweza kutuumbua kama alivyomuumbua mpenda wetu
huyu mbaya zaidi ni siku ambayo kama mkrosto alitakiwa kuwa kwenye mkesha
kanisani siku hiyo!
Mungu atusadie sana tuwe na mwisho mzuri hapa duniani
yasitupate kama ya mwenzetu kanumba siku ya mwisho ya uhai wake,tumuombe mungu
siku hiyo tuwe katika kufanya yampendezayo mungu

Anonymous said...

Pole sana. Ina maana wazai wa Lulu watabaki kulea mjukuu wao mana Lulu atafungwa maisha.

Anonymous said...

JAMANI JAMANI TANZANIA TUWE NA SHERIA HUYO MTOTO MNAAMBIWA HAJAUA NA MDOGO WAKE KANUMBA KASEMA HIVYO MPAKA LULU ANATOKA NJE KWENDA ZAKE JIRUSHA ALIKUWA HANA HATA WAZO KUWA KANUMBA ANAWEZA AKAFARIKI NYUMA YAKE , NA BWANA KANUMBA MDOGO KASEMA LULU ALIVYOONDOKA ALIIINGIA CHUMBANI NA KUMKUTA KANUMBA BADO MZIMA NA WAKAONGEA ILI AMWAMBIE DAKTARI WAKE NA AKAFUATIWA DAKTARI NA AKAJA NA BADO WAKA MPIGIA SIMU LULU AJE ILI WAMPELEKE KANUMBA HOSPITAL YEYE AKAWA HATAKI, KWANI HAIKUWA LAZIMA KWANI ALIMUACHA AKIWA KATIKA HALI NZURI TU SIO YA KUTISHA HIVYO. NA KANUMBA KAFARIKI HOSPITALI SASA INA KUWAJE HUYO MSICHANA UNDER AGE AWEKWE RUMANDE KWA KOSA LA KUMUUA MTU JAMANI KWELI NDIO TANZANIA?

NA VIPI HUYO KANUMBA MTU MZIMA WA MIAKA 28 KUWA NA LOVE AFFAIR NA MTOTO WA KIKE UNDER AGE HAJAFIKA UMRI WA MIAKA 18, SASA HAPO NANI ALIKUWA NA KOSA LA JINAI?

NA TANZANIA MPKA SASA TUNAFUATA SHERIA ZA KIINGEREZA VIPI MTOTO WA UNDER AGE AWEKWE MAHABUSU? HAKUNA DHAMANA SIKU HIZI TANZANIA AU KWA SABABU NI MTOTO WA MASIKINI?

HUYO MAREHEMU KAMA ANGEKUWA HAI YEYE NDIO ALIKUWA MTU WA KUTIWA NGUVUNI (R.I.P) HUU NI MFANO. AU NA WAZAZI WA KANUMBA WAMFUNGULIE MASHITAKA MAREHEMU KWA KUMLAWITI BINTI YAO AMBAYE HAJAFIKIA UMRI WA KUFANYA NGONO MPAKA AWE ANAANZA KUMUONEA WIVU?
WATANZANIA TAFAKARILI SANA HILO TUKIO SIO TU KWA SABABU NI KANUMBA NO HAKI ITENDEKE KWA KILA MTANZANIA DEMOCRACY IKO WAPI HAPO KAMA HAKUNA HAKI ZA BINADAMU?
NAMUOMBEA KILA LA KHERI MAREHEMU MUNGU AMUWEKE MAHALA PEMA PA MILELE APUMZIKE KWA AMANI, SIS WOTE TUTAFARIKI HAKUNA ATAKAEISHI HAPA DUNIANI MILELE, AMEEN

MDAU LONDON

Anonymous said...

Nimeongea na Mtumishiwa Mungu mmoja wa muda mrefu hapa Dar es salaam. ambaye hufanya huduma ya maombezi. Akaniambia kuwa watu wengi hawafahamu lakini Kanumba ameuawa kishirikina sema huyu Mtoto Lulu "kasakiziwa kishirikina". Yaani siku ile ilikuwa imepangwa Kanumba lazima angekufa. Sema Lulu akawa amekutwa katika mazingira yale na akaogewa kishirikina. Tatizo ni kuwa serikali haiamini mambo ya kiroho.

Lulu hajamuua kanumba sema kasakiziwa kishirikina tu.

Tunamwombea Mungu amsaidie

frank johnson jokes said...

mi naona uamuz tuiachie mahakama mengi yashasemwa

frank johnson jokes said...

mengi yashasemwa,tuiachie kazi mahakama