Thursday, April 12, 2012

Baba Lulu Aongea na Waandishi wa Habari

KWA HISANI YA BLOGU YA JAMII:

Mzee Michael Edward Kimemeta (picha na Dixon Busagaga)

Imeandikwa n Dixon Busagaga  - Globu ya Jamii Moshi


Baba mzazi wa Muigizaji wa kike wa filami nchini maarufu kama Lulu, ambaye anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba, ameibuka na kueleza kushtushwa sana na taarifa za kifo hicho pamoja na habari kuwa bintiye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli na kuwa anahusika na kifo chake.

 Baba Lulu, ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta(49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro, kaiambia Globu ya Jamii leo huko Moshi kuwa alimtambua Steven Kanumba kama mwalimu wa mtoto wake Lulu,lakini hakuamini masikio yake baada ya kupata taarifa za kifo hicho, huku bintiye, anayedaiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu, anahusika.


Lulu alifikishwa mahakamani jana April 11, 2012 akikabiriwa na mashtaka ya mauaji ya Marehemu Steven Kanumba, ikiwa ni siku nne baada ya kifo cha msanii huyo. Alisema kuwa Elizabeth ama Lulu alizaliwa tarehe April 17,1995 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, na kwamba alimaliza elimu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Midway mwaka jana na kamba hivi sasa ana umri wa miaka 17.

Bw Kimemeta alisema kuwa ni vyema polisi kuwa makini katika uchunguzi wao kwa kuzingatia kuwa tukio hilo limejenga chuki na uhasama baina ya Lulu na ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wa marehemu Steven Kanumba. Alisema kuwa kilichomshtusha zaidi ni taarifa za polisi kusema kuwa kulitokea ugomvi kati ya Marehemu Steve Kanumba na Lulu,huku ikitajwa kuwa walikuwa wapenzi.

“Hatukutegemea kama Marehemu Kanumba angeweza kuwa na mahusiano y kimapenzi na binti yetu; kwanza ndiye tuliyekuwa tukimtegemea kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza na kukikuza kipaji alichokuwa nacho Elizabeth”, alisema baba mtu. “Ninaomba Wanasheria na wanaharakati wa haki za kibinadamu kuingilia suala hili na kusaidia katika kupatikana kwa haki dhidi ya shtaka la mauaji linalomkabili binti yangu Elizabeth na pia naomba swala hili lisichukuliwe kishabiki ama kwa hisia bali haki ichukue mkondo wake”alisema.

Kanumba na Lulu mwaka jana.  Picha kwa hisani ya  Mpeli Jr Ngonywike
 Alisisitiza kuwa jamii inatakiwa kutambua mazingira ya tukio hilo,ambapo chanzo kinasemekana ni ugomvi uliopelekea tafrani kwa Lulu kutuhumiwa kumsukuma Marehemu Kanumba kwa kile kinachodaiwa kuwa ulikuwa wivu wa kimapepenzi na haiyumkini hakukusidua kumuua hivyo yeye anashangaa bintiye kuhusishwa moja kwa moja na mauaji.

“Ushiriki wa mwanangu kuhusu mambo ya sanaa nilikwishapata wasiwasi na mama yake mzazi alikuwa akiwasiliana na Marehemu Kanumba enzi za uihai wake ambaye alikuwa anamhakikishia usalama wa Lulu na kusema kuwa ataendele kubaki kama mwalimu…..lakini leo nasikia alikuwa ni mpenzi - nilishtushwa” alisema Kimemeta.

Baba Lulu pia ameelezea kusikitishwa kwake kwa kushindwa kuhudhuria mazishi marehemu Steven Kanumba kuhofia usalama wake, na kusema mazingira yatakaporuhusu hata sita kufika nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba na kutoa pole. Bw Kimemeta amesema kuwa anaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia ya Marehemu Steven Kanumba na kutoa mkono wa pole kwa msiba huo mkubwa ambao haukutarajiwa.Kasema kuwa Kanumba alikuwa bado ni kijana mdogo aliyeonyesha umahiri kwenye sanaa na kwamba amecha pengo kwa familia yake na Tanzania kwa ujumla.

Lulu na Mama yake Mzazi, Bi Lucrecia Kalugila

20 comments:

Anonymous said...

Baba Lulu, Pole sana kwa yaliyoikumba familia yako ila nina maswali kidogo tu:
1. Leo unatuambia kuwa mwanao ana miaka 17 alipohojiwa na Salama Jabiri yeye akatamka kuwa ana miaka 18 Mbona hukujitokeza katika magazeti na blog kupinga kuwa mwanao ni muongo hajafikisha miaka 18 ili asije jiingiza katika mambo yanayozidi umri wake?
2. Lulu amekuwa akisemwa kuwa na mabwana wengi tu achilia mbali Marehemu, na yeye siku 1 alihojiwa akasema kwani ni mtoto pekee ambaye anafanya mapenzi mtaani? mbona hukujitokeza na kukanusha hayo?
3. Hivi familia yako ni ya aina gani? mnakaa na mkeo ama mlishatengana? huwa unakaa na mwanao na kumfundisha jinsi ya kuishi?
Wahenga walisema asiyefunzwa na dunia hufunzwa na ulimwengu, nyie mlishindwa kumfunda mwanenu leo hii unakuja kusema eti haki za binadamu sijui na wana harakati hvi haki ya ALIYEKUFA NAYO HUWA INAZIKWA? HATA KAMA WATAMTOA KWA MBINU ZA KUMPUNGUZIA MIAKA AONEKANE NI MINOR KUMBUKA MUNGU NDIYE HAKIMU MKUU, WEWE KAMA MZAZI FIKIRIA MAMA NA BABA KANUMBA KWA HIVI SASA WANAJISIKIAJE? INGEKUWA LULU NDO AMEKUFA UNGEOMBA MAHAKAMA IMTOE MUHUSIKA KWAVILE MWANAO ALIYAKATA MWENYEWE? KUMBUKA " JUSTICE SHOULD NOT ONLY BE DONE BUT SEEN TO HAVE BEEN DONE"
LA MWISHO: KAMA UNA MTOTO MWINGINE BASI JIFUNZE KUONGEA NA WANAO NA KUWAELIMISHA UMUHIMU WA KUSOMA KWA BIDII, KUJIEPUSHA NA MAPENZI WAKIWA WADOGO NK.

Anonymous said...

Kumbe Lulu ana wazazi wote wawili. Mimi nilidhani ana mama tu! Kweli nimeamini kuzaa si kazi kazi ni kulea

Anonymous said...

Nimeshindwa kabisa kumwelewa Bwana huyu. Ina maana alikuwa haelewi kitu gani na kwa akili zake ilikuwa haki kumkabidhi Binti wa miaka 14 kwa mwanaume asiye na mke wala familia ili "amlelee mtoto wake wa kike"? Utetezi mwingine ni wa kijinga na unatia kinyaa.

Anonymous said...

mmmh! makubwa! mm nimeshangazwa kwa maelezo ya kuwa ninyi wazaziu mlikuwa mnamtegemea binti, hv kweli uliwaza mbali, au ulikua unachekelea tu? Hv na nyie mlisimama kama wazazi au mlikua mna act hii picha ambayo imekua kweli kwa sasa?

Anonymous said...

achukuliwe sheria ni mtu mzima huyo msilete zenu kuwa ana miaka 17 ameshafanya birthday ya kutimiza miaka 18 hana utoto wwte

Anonymous said...

MIMI NAFIKIRI UMEFIKA WAKATI SASA WASANII KUIGIZA NA SI KUYAFANYIA PRACTICAL YALE WANAYOIGIZA VILE VILE WANAUME LAZIMA TUJUE WANAWAKE WALIOSHINDIKANA WEWE UNAONA MTU ANA SKENDO KIBAO NA WEWE BADO UNAJIFANYA KUPOTEZEA NAFIKIRI TUJIFUNZE YA DIAMOND NA WEMA SEPETU. HILI LIMEKUWA KUBWA ZAIDI MAANA LIMESABABISHA KUTOWEKA KWA UHAI WA MTU. USTAA SIYO KIGEZO KAMA HUYO BINTI ANAVYOJITETEA KILA ANAPOHOJIWA NA WAANDISHI WA HABARI KWANI YEYE NDIYE STAA WA KWANZA? WAPO MASTAA KAMA PAUL SCHOLES,CELINE DION,PROF J NA WENGINE WENGI TUJIFUNZE KWA HAWA WATU

Anonymous said...

Kuna tatizo zaidi la tunavyodhania, huyu Mzee anaongea yuko Moshi mwanae yuko Lupango Dar, ni jinsi gani inavyoonekana hawajibiki kama Mzazi! eti akamwone JK!!! ili amsaidie kulea? au? Nidhahili huyu mama alitelekezwa! kuna sehemu nimesoma Mama yake Lulu alikuwa Muhudumu wa Ndege, isingelikuwa kutelekenzwa huyu mama angemlea mwanae na kutimiza ndoto zake, Sijawahi ona mhudumu wa ndege mjamzito yawezekama mama huyu alipoteza ajira yake nzuri pia

Inawezekana pia kuyumba kibiashara kwa ATC kulichangia mama yake Lulu kupoteza ajira na hivyo familia kukosa mwelekeo hatimae watoto kuishia kwa akina Kanumba, nimesoma huyu mtoto alikuwa tegemeo katika riziki ya siku ya mama yake, kwa ajira ipi? usanii au ukimada kwa Kanumba.

Huyu Mtoto wa miaka 16 aliyemaliza form four mwaka jana tayari alikuwa akimiliki gari huku akiwa tegemeo la familia! babayake aliwahi uliza kalipataje?

Kuna tatizo pia la single parent, Kanumba na Lulu wamelelewa na mamazao zaidi, hivyo yaelekea walikuwa na madhara ya kisaikologia ya tangu utotoni! Hatujaelezwa wazazi hawa waliachana kipindi gani? isijekuwa baada ya kutwangana makonde, hivyo hata watoto wakaamini ndani ya nyumba bila makonde haiwezekani!

Anonymous said...

baba yake amezidi kulikoroga anatuambia kuwa mwanawe ana umri wa Miaka 16 inamaa clouds walitudanya au walindanganywa pia mwaka jana akasherehekea miaka party ya Miaka 18 inamaa alikuwa anawadanya wenye kumbi za starehe na magesti kuwa amekuwa mtu mzima ili wakimuona huko wasimtimue mbona wazazi wake hawakujitokeza kipindi hicho wakanushe umri wake???

Anonymous said...

Haya masuala ya Lulu kusema umri wake ni huu au ule hayana maana yoyote. Lulu amezaliwa katika kipindi ambacho utunzaji wetu wa kumbukumbu ni mzuri kwa hiyo record zitaongea. sioni maana ya kuendelea kuzipa uzito wowote kauli zake maana hatujui alikuwa anazitoa kwa maslahi gani!

Mafry E said...

Nimevutiwa sana na tafakuri ya mazingira ya kifo cha Kanumba. Kiukweli mimi binafsi niligubikwa na simanzi nzito ingawa niko mbali sana kwa sasa takribani mwaka mmoja niko china. Kanimba ni mmoja wa wasanii ambao niliwakubali sana katika tasnia ya filamu na hata akanifanya nikubali bongo muvie, na siku ya tukio nilikua naangalia muvie yake ya "Crazy Love", na niliumia sana kwenye scene ile ya yeye kupigwa baada ya kukutwa na mke wa mtu, akapigwa hata akapoteza timamu zake kwa muda. Mimi sina mengi juu ya hukumu yake kwani Allah ndiye hakimu.
LAKINI,

Nikafunguka fahamu na kujiuliza maswali wa kadha, ambayo pia yamenifanya nijiunge na jamii forum kwani sikua mwanachama wa platform hii. Kiukweli haya ni majambo ya kiinteligensia kweli na labda kuna vyombo ambavyo viko responsible kushughulikia kwa mujibu wa katiba yetu, ila mwananchi mwema hakatazwi kutoa mchango wa kuliona hili kwa upana kwani hata hao ambao wanahusika kwa sasa watategemea watu ambao walikuapo kwenye tukio. Nilijiuliza maswali mengi na si kwa mantiki ya kumgandamiza Lulu, ila swali langu ni kama ifuatavyo;

1. Nini kilifanya Lulu aondoke ilhali yule ni mpenziwe na sidhani kulikua na kitisho chochote kwake kutoka kwa bwana bosco ambacho kilimfanya yeye akimbie?
Halafu tafakuri ya muvie alizoigiza kanumba kaka zinanipa mshutko juu ya nguvu za hawa watu wanaitwa "Illuminati", inasadikiwa by saa saba usiku wa tarehe saba bwana kanumba alifariki dunia akitokea kuoga. Kuna vitu kadha hapa vya kuvitafakari, saa saba (7), tarehe saba (7) na jina lake likiwa na herufi saba (7), jumla yake ni zile triple seven (777) zinazohusishwa na kafara ya daraja ya juu kabisa kwa hawa freemason, na kuoga kumerepresent "Rain Man". Nina wasiwasi tukio hili ni zaidi ya Lulu, kwa kuwa kwa ninavyomjua mimi Lulu hana ubavu wa kumsukuma the great, na Lulu alikua kama alivyozaliwa, freemason wanawatumia wanawake kama agent of evil, naye lulu alikua katika umbo lile la ibilisi tena kwenye ijumaa kuu (siku ya saba katika juma). Utajiuliza kwa nini muda wote huo kama ulivyoeleza hapo juu, saa sita mpaka saa kumi na moja alfajiri, kivipi?, hapo palikua na mipango inafanyika. Na pia huyu jamaa wa nigeria anaeitwa Ramsey alikua Bongo few weeks ago, unajua alikuja kufanya nini? huyu ndie walie act muvie pamoja ile ya Evil Kingdom, unapata somo gani kutoka muvie ile? jiulize kwa kina utapata majibu. Kwa hivyo kwa tafakuri yangu mimi Lulu alikua scapegoat kufanikisha lengo la kafara ya juu kabisa na hivyo High profile celebrity Kanumba karata ilimwangukia na wengine wanafuata muda utakapofika. NIMENUKUU TOKA JAMII FORUMS

Anonymous said...

Pole Mr. Michael, lakini nachelea kidogo kusema yafuatayo: Kwanza sintakosea kama nikisema bila shaka hujakuwepo nchini kwa muda mrefu na kama nimekosea basi kwa hili unapaswa kulaumiwa. Si juu ya tukioa la kifo cha ndugu yetu Kanumba la hasha! Bali ni juu ya malezi na makuzi ya mdogo wetu Eliza. Mr. Michael ni muda mwingi vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikilalamika juu ya mwenendo usioridhisha wa Eliza na hata ktk mitandao mbalimbali picha zake zilisizo na staha zimejaa. Lakini sikuwahi kubahatika kusikia sauti yako ikikemea mwenendo huo. Amefanya sherehe kubwa ya kutimiza miaka Kumi na nane ambayo leo hii anaikana huenda ni kutokana na dhahama iliyoko mbele yake. Nina mengi ya kukuambia baba Lulu, lakini naomba niwe na kiasi pamoja na busara niishie hapa, kwani hatujajua bado nini hatima ya mdogo wetu LULU. Namalizia kwa kusema hatukuziba ufa leo inatugharimu kujenga ukuta.

Anonymous said...

LULU NI MWONGO!
NINAMWITA MWONGO KWA KUWA AMEKUWA AKIDANGANYA KUHUSU UMRI WAKE. KATIKA INTERVIEW ZAKE HAPO NYUMA ALISEMA ANA MIAKA 18 NA ALIANDAA PARTY YA KUSHEREHEKEA UMRI HUO.

SASA HATUJUI ALIKUWA ANADANGANYA WAKATI HUO WA SHEREHE NA WA INTERVIEW AU ANADANGANYA SASA BAANDA YA KUPATIKANA NA KESI.

KWA KIGEZO HICHO NI VIGUMU KUJUA LULU ANASEMA KWELI WAKATI GANI?

LABDA AKAFANYIWE KIPIMO CHA "LIE DETECTOR"

Anonymous said...

mama naye weaving la blue?????????????

Anonymous said...

Inasikitisha sana kumpoteza kijana ambaye amelitangaza Taifa letu, Mungu atupe nguvu kustahimili msiba pia amlaze mahali pema peponi. AMENI

Anonymous said...

how l wish hako kalulu kafungwe ili iwe fundisho kwa wengine wenye vihere kama yeye na waswhili wanasema ukiona mwenzako ananyolewa na wewe tia maji so thoz who they think they no better than god should becareful with god coz there an he does not like wat u guyz r doing so heads up live like other person an stop doing stupid thingz in order kupata umarufu ambao mwisho wa siku unaishia pabaya by the way pooooooole lulu but u nid to learn ur lesson babygirl an stop being jlo.....

Anonymous said...

Wazazi wa Lulu wana maswali magumu ambayo wanapaswa kujibu. Huyu binti ana umri wa miaka 17 au 18 (hatuna uhakika na hili), lakini ukweli unabaki kuwa anatakiwa kuwa shuleni kwa maana ya kuwa high school au chuoni. Huyu Lulu alianza kujihusisha na sanaa mwaka 2007 akiwa na miaka 12 au 13 na baada ya muda mfupi akaanza kuonekana katika kumbi za starehe. Inaelekea kulikuwa na matatizo makubwa katika malezi yake na wakulaumiwa ni wazazi wake.

Anonymous said...

Huyu lulu, aliulizwa kwenye kipindi cha mikasi na salama "do yu have a bf" kikoje salama am too young sina bf wala sitaki! Shame on yu lulu!

Anonymous said...

What was a 17-year-old minor doing at the home of a 28-year-old man at midnight?

Anonymous said...

Inaonekana mmesahau Mchango wa uchawi katika jamii za Ki afrika.

Kanumba inaweza kuwa amelogwa na wachawi!

Msichana mdogo kama Lulu amepata wapi nguvu za ziada za kumsukuma mtu mwanamume hadi kumwua.

Kwa wale wasiojua kuna Majini Mahaba ambayo kama yamemwoa binti yanakuwa na wivu mkali sana na mara nyingi huwa yanawadhuru wanaume wanaojaribu kuwaoa au kuwatongoza wanawake hao.

Angalia Emmanuel TV Live service kila jumapili kutoka Lagos Nigeria utajionea makubwa ya watu wanaokwenda kuombewa huko wakiwa na kesi zinazofanana na kisa hiki.

Anonymous said...

NYIE WAPUMBAVU WA U TURN MNAOMUITA LULU MTOTO MNANIKERAAA,KATEMBEA MPAKA NA BABA
YAKO MZAZI HALAFU MNAMUITA MTOTO,KAFANYA BONGE LA PART YA KUTIMIZA MIAKA 18,NA
WAZAZI WALIUDHURIA BADO MNAMUITA MTOTO K....NINA ZENU.SASA HIVI WANATAKA KUFOJI
ILI KESI ISIFIKE MBALI.MPAKA MUAJIRI WAKE ANAJUA KAMA LULU NI 18,DOCUMENT ZAKE
ZIKO HUKO.18 YEARSSSSSSSS,MBUZI NYIE.MTOTO,MTOTO,MTOTO K..ZENU?SHUSHIIIIIIII