Tuesday, April 10, 2012

Mazishi ya Bongo Superstar Steven Kanumba Mjini Dar!

Wadau, ama kweli Steven Kanumba alikuwa Superstar!  Watu kuzimia, kuanguka vilio, si wanawake, si wanaume kwenye kilioni, kwenye mazishi mpaka inabidi wahudumiwa na Red Cross! Duh!  Inanikumbusha nilivyoona documentary kuhusu kifo cha mcheza sinema maarufu wa Marekani, Rudolf Valentino mwaka 1926. Valentino naye alikufa ghafla akiwa na miaka 31 tu!  Alikuwa anapendwa mno, tena mno. Watu walitoka kila kona kwenye msiba wake na kwenye mazishi na ilibidi polisi waingilie.  Habari niliyosoma leo kuhusu kifo cha marehemu Kanumba imenikumbusha msiba wa Valentino.  Wazungu wanaweza kusema, The similarities are eerie.

REST IN ETERNAL PEACE STEVEN KANUMBA!


Misa ya Kumwombea marehemu Steven Kanumba huko Leaders Club, Dar es Salaam


Picha Zote kwa hisani ya Michuzi Blog. Kuona Picha zaidi za mazishi tembelea MICHUZI BLOG:

3 comments:

Anonymous said...

KAMA WALIJUA MAZISHI YANGEKUWA HIVI KWA NINI HAYAKUFANYIKIA UWANJA WA TAIFA? TUPE HABARI ZA DADA YETU ELIZABETH MICHAEL LULU. HALI YA BINTI YETU INAENDELEAJE? HUYO BINTI MSHAURI AINGIE KWENYE BLOG ATAFUTE MUME AOLEWE MAANA MAISHA KAYA HALIBU MWENYEWE MAPEMA AKIWA BADO BINTI MREMBO NA MDOGO. CAREER KAIHALIBU KABISA NA AMEPOTEZA TRUST YA WENGI. SIDHANI KAMA KIUKWELI YEYE BINAFSI KAMWUA KANUMBA SI KWELI LAKINI JAMII HAITAKI HATA KUSIKILIZA HER SIDE OF STORY SASA CHA MSINGI AKITOKA ATAFUTE MCHUMBA NA AACHANE NA TABIA YA KULUKALUKA AANZE MAISHA SASA. HUU NI USHAURI WANGU. KIUKWELI LAST TIME NIMEONA MAZISHI KAMA HAYA NI PALE NYERERE NA KAWAWA WALIPO KUFA LONGTIME. LULU AMETOKA JELA? WAMWACHIE HUYO MTOTO HAJAMWUA KANUMBA IT DOESN'T MAKE SENSE AT ALL.

Anonymous said...

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, jana alisema Polisi inaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo hicho, ikiwa ni pamoja na kuchunguza mawasiliano ya simu.

“Inaonesha chanzo cha ugomvi wao ni wivu hasa kutokana na Lulu kutoka nje kwenda kuzungumza na simu, hivyo tunafanya uchunguzi wa mawasiliano ya simu na uchunguzi wa kisayansi kwa vielelezo vingine tulivyokuta eneo la tukio kama vile, mvinyo, soda na panga kama vilitumika.”

“Pia tunasubiri ushahidi wa kitaalamu wa madaktari ambao muda huu (jana mchana) walikuwa wakiendelea na uchunguzi kubaini sababu za kifo katika hospitali ya Muhimbili.”

Kamanda Kenyela alisema kutokana na kosa lenyewe, Lulu hataruhusiwa kuhudhuria maziko ya Kanumba.

Kuhusu kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, Kenyela hakutaja siku maalumu ya kufanya hivyo zaidi ya kueleza na kuwa atafikishwa kwenye vyombo vya sheria pindi taarifa zote muhimu zitakapokamilika.

“Siwezi kusema ni lini atafikishwa mahakamani kutokana na aina ya kosa lenyewe, tunataka tujiridhishe na kila upande upewe haki stahiki na tunataka kulitekeleza hili mapema zaidi. Ninachoweza kusema ni kuwa Lulu yuko katika hali nzuri”

Soma habari nzima kwenye gazeti la HabariLeo

Issa Ismail said...

washikaji zangu mimi nafeel kishenzi sana yaani kifo cha huyu mr.ni cha kusikitisha sana kwa maana alikuwa hana mfano ndani ya Bongo movie.Naitwa ISSA ISMAIL napatikana maeneo furani ya Mbagala