Wednesday, April 11, 2012

Maggid Mjengwa Aomba Jamii Imsamehe Lulu - Kifo cha Steven Kanumba



Lulu, alivyokuwa na maskendo (scandals) sijui kama itakuwa rahisi kwa jamii kumsamehe katika jambo la kifo cha Steven Kanumba!

**************************************************************


KUTOKA MAGGID MJENGWA BLOG:
Neno La Leo: Jamii Ya Walo Wema Imsamehe Elizabeth ' Lulu' Michael

Ndugu zangu,

Jana amezikwa Steven Kanumba , kipenzi cha wengi.

Mauti ya Steven Kanumba yanatukumbusha wanadamu ukweli huu; kuwa maisha yetu hapa duniani ni mafupi sana. Hivyo, lililo jema kwetu wanadamu ni kuishi kwa kutenda yalo mema. Kuwatendea mema hata tunaodhani wametukosea, maana, tutawasaidia kujifunza kutenda mema. Na ni mwanadamu gani asiyekosea?

Na moja ya adhabu kubwa mwanadamu unaweza kuipata humu duniani kutoka kwa wanadamu wenzako ni adhabu ya kutengwa na wanadamu wenzako.

Msichana Lulu ameshapata na anaendelea kuipata sasa, adhabu kubwa sana kutoka kwa wanajamii. Adhabu ya kupewa hukumu ya mauaji na kutengwa na wengine. Lulu , ambaye ni mmoja wa waliokuwa karibu na marehemu Kanumba hata katika dakika zake za mwisho maishani, na ambaye alikuwa mpenzi wa Kanumba, hakuweza kushiriki mazishi ya mpenzi wake. Hiyo nayo ni adhabu kubwa kwa Lulu kupewa na wanadamu wenzake.

Yumkini Lulu ana mapungufu yake kama mwanadamu, lakini, kwa sasa hastahili adhabu kali hiyo kutoka kwa wanajamii. Kwa kosa ambalo hakuna aliye na hakika leo kuwa amelitenda. Ndio, Lulu aweza kuwa mwanadamu mwenye mapungufu yake mengine, lakini , hayo yasitufanye wanadamu tuwe na haraka ya kumpa hukumu isiyo ya haki. Na kwenye mienendo ya maisha, ni mwanadamu gani asiye na mapungufu?

Maana, tangu mara ile ilipofahamika, kuwa msichana Elizabeth ‘ Lulu' Michael alikuwepo kwenye mazingira ya kutokea kwa kifo cha Kanumba, basi, jamii, huku ikisaidiwa na vyombo vya habari, haraka ikapata wa kumnyoshea kidole. Na hukumu ya Lulu kutoka kwa wanajamii walo wengi ikawa imetolewa hapo. Kwamba Lulu ndiye muuaji. Kwa sasa, hukumu hiyo haiwezi ikawa ya haki mpaka pale wenye mamlaka ya kututhibitishia hilo watakapofanya hivyo.

Na hata kama ugomvi, uliotokana na wivu wa kimapenzi , wa Lulu na mpenzi wake ulipelekea mauti ya Kanumba, bado maelezo tuliyoyasikia hayamwonyeshi Lulu kuwa na dhamira ya kutaka kutenda maovu anayohukumiwa na wanajamii kuwa kayatenda. Hivyo, naye, kama mwanadamu, anastahili msamaha kutoka kwa wanajamii wengi walo wema.

Katika wakati huu mgumu sana kwa msichana Lulu, vyombo vya habari viwe mbele katika kumsaidia Lulu kama mwanadamu mwenzetu, badala ya kutumia balaa lililomkuta kama mtaji wa kuandika na kutangaza udaku wa kuuzia magazeti na kuvutia watazamaji wa runinga na wasikilizaji wa redio.

Maana, kwa adhamiriae kutumia magumu yanayomkabili msichana Lulu kuvuna, basi, hana atakachokivuna zaidi ya kuvuna dhambi.

Badala yake, media isaidie katika kutufanya wanajamii tujitafakari. Kwa vile, habari za matukio ya mahusiano yasiyo na staha na matendo ya kiuhuni yanayofanywa na baadhi ya wanajamii wakiwemo wasanii, huwa yanashabikiwa na vyombo vya habari badala ya vyombo hivyo kushiriki kukemea na kuelimisha jamii. inasikitisha, kuwa katika wakati huu, vyombo hivyo vya habari vyaweza kabisa kuwa kwenye harakati za kuandaa stori zaidi za ‘ kumning’iniza’ zaidi Lulu ambaye tayari ameshaning’inizwa hadharani.

Ndugu zangu,

Kama wanajamii, na wengine kama wazazi. Lulu anabaki kuwa ni msichana mdogo anayehitaji kusaidiwa katika wakati huu mgumu kwa maisha yake. Yumkini vyombo vya dola vinaweza vimtie au visimtie hatiani. Hivyo, kumwachia huru Lulu.

Lakini, bado hukumu ya jamii ikabaki pale pale. Hukumu ya Lulu kutengwa na jamii. Hiyo ni hukumu mbaya zaidi inayoweza kuchangia hata kuyafupisha maisha ya msichana huyu mdogo. Jamii haina faida na hukumu kama hiyo. Ni heri ikamwacha huru aende akapambane na yanayomkabili mbele yake. Ndio, akapambane na maisha haya magumu ya dunia hii bila kujisikia kutengwa na wanajamii wenzake.

Na naamini, leo kuna wengi kama mimi, wenye kufikiri hili, kuwa jamii ya walo wema imsamehe Elizabeth ‘ Lulu’ Michael.

Na hilo ni Neno La Leo.

http://www.mjengwablog.com/

Maggid Mjengwa
Dar es Salaam.

9 comments:

Anonymous said...

Liwe fundisho kwa mabinti wadogo wenye mambo yanayowazidi umri. SIna maana kuwa namuhukumu kuwa ameua; ila kwa umri wake hakupaswa kuwa nyumbani kwa wanaume muda mbaya hivyo. Nina imani wazazi wake walishamshindwa wakaacha dunia imfunza na ndo funzo lenyewe hilo.

Anonymous said...

Elizabeth michael pole sana mdogo wangu,mimi sina uwezo ila jamani mwenye uwezo baada ya kesi yake amchukue aende nje ya nchi walau apumzike jamani,hatujua anajutia kiasi gani maana anaweza fanya maamuzi magumu hasa akijichukia mwenyewe,wasamaria msaidieni lulu apumzike,namuonea huruma sana sasa hapo kichwani sijui anawaza nini,siajabu anajuta sanaa,mahakama imsamehe tu kwani wangapi wanafanya makosa?hata ikimbana kiasi gani uhai wa kanumba utarudi?lulu mama omba hata kimoyo moyo mungu atasikia sala zako,nasi tunakuombea,nakupenda sana lulu,single parent ni tatizo sana.

Anonymous said...

lulu hana kosa ni bahati mbaya tu iliyomkuta sioni haja ya kumuombea msamaha ila ss wenyewe tupime na tuone uzito wa hili tatizp alilonalo hapo mahabusu nafikiri hakuna kitu kinachomuuma kama kushindwa kumzika mchumba wake ambaye inavyosemekana walikuwa ktk hatua za mwisho za kuoana tusihukumu mapema hv amesema yeye mwenyewe kila kitu kitajulikana muda si mrefu tumuombee mungu amsaidie hajakusudia yaliyotokea yatokee bado mdogo mno

Anonymous said...

Nasikia tetesi mitaa ya sinza,,kwamba marehemu alikuwa anakula mzigo bafuni ghafla ndo simu ya Lulu ikaita chumbani,,baada ya lulu kustop kwenda kuikimbilia simu yake,,marehemu the great naye akamuungia kumfuata,,bahati mbaya akateleza akitokea bafuni na kuanguka,,,,wapo wanaodai wakati daktari anafika marehemu alikuwa mtupu..

Haya basi tuwaachie mapolisi wetu wa kibongo waendeshe hii movie.

RIP The Great

Anonymous said...

Na mimi nimesikia theory:

Inasemekana walikuwa wakigombea mlangoni. Mmoja anafunga mwingine anafungua.

Inaonekana aliyekuwa anataka kukimbia ni marehemu baada ya kuona pumzi zinamwishia baada ya kuwekewa kitu cha kudhoofisha. Aliyekuwa anafunga mlango ni Lulu kumdhibiti marehemu asikimbie ili ile dawa aliyowekewa ifanye kazi.

Maana mara baada ya kufungwa mlango dakika tatu baadaye lulu akawa anatoka marehemu akiwa chini.

Kama Kanumba angekuwa mzima asingebamizwa na msichana kwa jinsi ilivyotokea.

Inavyosemekana na baadhi ya watu kuwa hii ilikuwa ni conspiracy wa watu kadhaa.

Simu iliyopigwa ilikuwa ni kucheck kama kila kitu kinaenda kama ilivyopangwa na ya kwamba operation ianze.

Hii ni theory ya wale wanaofuatiliaga Murder Mysteries

Anonymous said...

It is sad how watanzania wanavyo nmjaji mtoto huyu, lulu sioni kama ana hatia,
angekuwa ana nia ya kumuua marehemu asingemfuata kwake akamuulie chumbani kwake
ile ilikuwa ajali kama ajali nyingine na siamini hata kama alimsukuma, pliz
people stop judging this kid acheni sheria itumike na jaji awe na akili zake
maana judgement nyingine za kibongo bongo hata hazieleweki tukumbuke Ditopile yy
alimshuti mtu kabisa na gubunduki ba still ilikuwa kuua pasipo kukusudia, this
girl doesn't deserve all of that, mwe i wish akishinda kesi wamtoe kwenye hio
nchi akaishi mbali nahapo maana watu hawataacha kumnyoshea vidole

Anonymous said...

It is sad how watanzania wanavyo nmjaji mtoto huyu, lulu sioni kama ana hatia,
angekuwa ana nia ya kumuua marehemu asingemfuata kwake akamuulie chumbani kwake
ile ilikuwa ajali kama ajali nyingine na siamini hata kama alimsukuma, pliz
people stop judging this kid acheni sheria itumike na jaji awe na akili zake
maana judgement nyingine za kibongo bongo hata hazieleweki tukumbuke Ditopile yy
alimshuti mtu kabisa na gubunduki ba still ilikuwa kuua pasipo kukusudia, this
girl doesn't deserve all of that, mwe i wish akishinda kesi wamtoe kwenye hio
nchi akaishi mbali nahapo maana watu hawataacha kumnyoshea vidole

Anonymous said...

Kwa vyombo vyetu vya dola na sheria kutofuatwa sawasawa, nina wasiwasi kuwa huu pia ndio mwisho wa Lulu kwani huenda atakaa rumande kwa zaidi ya miaka hata miwili kabla kesi yake haijasikilizwa. Sheria inasema kuwa mtu hana hatia mpaka ionekane kweli ana hatia hiyo (not guilty until proven)

Ingawa mimi siyo mwana sheria, nina imani kuwa kuna mambo kadhaa ya kuangaliwa kisheria:

(1) Chanzo cha kifo: Inatakiwa kuwe na autopsy itakyoonyesha sababu halisi ya kifo. Iwapo sababu ya kifo itaonekana kuwa ni jeraha lililotokana na kuangukia kicha baada ya kusukumwa na Lulu, basi hapo ndipo Lulu atakapokuwa na kesi ya kujibu. Hata hivyo iwapo sababu ya kifo itakuwa ni kitu kingine kwa mfano cardiac arrest au stroke ambayo kwa coincidence tu ilitokea wakati anasukumwa na Lulu, basi Lulu atakuwa hana kesi yoyote ya kujibu na atabaki raia huru kama mimi na wewe.

(2) Sasa iwapo autopsy itaonyesha kuwa kifo kile kimetokana na jeraha lililosababishwa na kusukumwa na Lulu, basi kuna maswali mengine ya kujiuliza:
(a) je Lulu alifanya makusudi kumsukuma Kanumba kusudi apate majeraha yale?
(b) Je Lulu alijua kuwa Kanumba akipata majeraha yale atakufa
(c) Je Lulu alikuwa na nia ya kumuua Kanumba kwa kumsukuma vile?
Majibu ya maswali haya yatasaidia kuweka kesi ama ni ya murder, manslaughter, au ni just unintended accident. Ni Murder iwapo Lulu alip[anga na alijua kuwa kwa kumsukuma Kanumba, ataanguka, kuumia na kufa. Ni Manslaughter iwapo alipanga na alijuwa kuwa akimsikuma ataanguka na kuumia lakini hakuwa na nia ya kumuua. Ni Just an accident iwapo alimsukuma kwa nia ni kuongeza nafsi baina yao tu na wala hakuwa na nia yoyoye ya kumwumiza kwa lolote lile.

Kama Lulu akionekana na hatia ya mauaji kwa maana ya murder, basi adhabu yake ni kunyongwa hadi afe. Iwapo ataonekana na kosa la mansalughter basi atafungwa kwa kipindi fulani na baadaye kuachiwa huyu, na iwapo itaonekana kuwa ni accedent tu, basi Lulu ataachiwa huru mara moja; anaweza kuendelea kushikiliwa na polisi kwa ajili ya usalama wake wakihofia kuwa wapenzi wa Kanumba watamdhuru.

Anonymous said...

Kesi nyingi za kuua bila kukusudia nyingi adhabu zake ni kifungo kinacho'range kati ya miaka mi'5 mpaka 7 Gerezani,kwa uzoefu wa kesi zilizowahi kutokea hapa Tanzania Mshtakiwa hutumikia Gereza katika kipindi kisichopungua miaka 8 na kuendelea ksbb ile ikishathibitika Mshtakiwa anahusika tu Gerezani akisubiri hukumu hukaa kwa kipindi kisichopungua miaka mi'3 mpaka mi'5 ndo hukumu inakuja kutolewa anafungwa rasmi sasa hiyo miaka kati ya mi'5 hadi 7 niliyoisema hapo awali,kwahiyo jumla ya miaka ambayo tuko likely kumkosa Ka'dada wetu(ikiwa mambo yatakwenda kama ilivyozoeleka) ni kati ya miaka 8 hadi 12,anyway ksbb bado ana miaka 17/18 atatoka bado anadai kidogo labda msosi umzeeshe kule Segerea,kipindi hicho labda unaweza kukuta Ray yuko kama Mzee Chilo kwahiyo atakuwa anendelea kubembea kama kawaida