Monday, May 19, 2008

Wananchi Afrika Kusini waua Wageni Nchini Mwao!

MMalawi akiokolewa na Polisi!

Waafrika Kusini wakisherekea kupigwa na kuuliwa kwa wageni nchini mwao!

Leo kuna habari ya fujo zilizotokea huko Afrika Kusini. Wanasema kuwa wananchi wenye hasira wanaua wageni/wahamiaji kutoka nchi zingine amboa wako kwao. Mpaka sasa watu 22 wameuliwa. Kisa eti ni chanzo cha wao kukosa kazi! Wengi ya waliouliwa wanatoka nchi za kiafrika kama Zimbabwe, Mozambique na Malawi.
Wageni huko wanakimbilia vituo vya polisi na makanisani kuomba hifadhi kusudi wasiuliwe.

Hivi Afrika Kusini imelaaniwa nini? Watu ni wepesi kusahau. Miaka mingapi Tanzania na nchi nyingi za dunia ziliwasaidia waAfrika Kusini mpaka walivyopata Uhuru wao. Mnakumbuka Mwalimu Nyerere alivyozuia timu ya Olympiki ya Tanzania kushiriki katika michezo kwa vile Wazungu kutoka Afrika Kusini walikuwa wanashiriki wakati weusi huko wananyanyaswa na Apartheid? Mnakumbuka Dakawa na Mzimbo huko Morogoro? Na tusisahau hao WaSouth Africa walioacha mbegu Bongo!

Hebu tukumbuke ni MSouth Africa aliyesababisha ajali iliyotoa roho mpendwa Waziri Mkuu wetu, Edward Moringe Sokoine! Na yule jamaa yuko wapi? Je, ni moja wa hao wanaotaka kuona waBongo huko wanauliwa!

Askofu Desmond Tutu amewaomba waache kuua watoto wa watu waliowasaidia kutoka kwenye mikono ya Apartheid. Ni aibu!

Kwa habari zaidi someni:

7 comments:

Anonymous said...

Hii mijitu imekaa kama wanyama tu, yaani nimeangalia picha hizo, hapana Wazulu wajinga!

Anonymous said...

Hao weusi wa huko wajinga watu! Bora wangebaki chini ya APARTHEID! Ilikuwa dawa yao!

Anonymous said...

Nchi enye laana hiyo! Waachie wenyewe watachinjana tu!

Anonymous said...

kwa kweli Mungu atanusuru sana na Tanzania yetu hii tuliyozoea amani na utulivu,watanzania tuna matatizo mengi sana nchini mwetu lakini tunaishi kwa amani bila machafuko,Mungu ibariki Tanzania.
proudly Tanzanian.

Anonymous said...

Dada Chemi.mimi nahisia tofauti na hii issue ya wa-sauzi kuwaua wageni.Ni naamini kuna kitu kipo nyuma ya mauaji.sijafahamu vizuri kiini cha mauaji japo inasemekana ni tatizo la ajira lakini bado sishawishiki na hiyo sababu.ukiangalia watu waliouwawa wengi ni wazimbambwe na Msumbiji(Hakuna mtanzania?) na hawa wote ni majirani.Hapana dada,labda kuna jambo linalosababisha ambalo hatujalifaham,ebu tisilaumu kwanza.

Anonymous said...

Nyani bwana? Wahindi wanawaogopa, wanaonea wabantu wenzao.

Anonymous said...

Mungu atawapa adhabu hao wasauzi.