Wednesday, May 28, 2008

Wayehudi wachoma moto Biblia huko Israel


Leo kuna habari kuwa huko Tel Aviv, Israel, wayehudi wenye siasa kali wamechoma moto biblia kadhaa zenye Agano Jipya. Agano Jipya inahusu Bwana Yesu Kristo, na wayehudi hawaamini habari zake.
Watu wanauliza kama wayehudi hawaoni kama kuchoma Biblia ni sawa na jinsi Hitler alivyochoma moto Torah zao.

Sasa wakristo wanaoenda kuhiji huko Israel kuona sehemu Bwana Yesu alipozaliwa wameanza kuwa na wasiwasi na usalama wao.

Habari pia zinasema kuwa kundi la Messianic Jews (wayehudi wanaoamwamini Bwana Yesu) ambao ni wachache huko Israel nao wameanza kuwa na hofu kuhusu usalama wao na haki yao ya kuabudu. Wengi wa Messianic Jews ni Wayehudi kutoka Eithiopia ambao ni weusi!

Messainic Jews huko Israel wamekutwa wakibaguliwa na Wayehudi wengine. Pia miezi miwili iliyopita, mtoto wa mchungaji wa Messianic aliumizwa vibaya baada ya kufungua barua enye bomu iliyotumwa kwa baba yake.
Nchi ya Israel ilianzishwa mwaka 1947 na wayehudi kutoka Ulaya waliyokuwa wananyanyaswa vibaya. Karibu wayehudi milioni 6 waliuliwa na Hitler. Waliteka nchi ya Palestina kwa vile ilikuwa nchi ya mababu zao tangu enzi za Musa na ni chanzo cha matatizo kati yao na waarabu hadi leo.

Kwa habari zaidi someni:

4 comments:

Anonymous said...

sishangai sana si ndo hao hao waliomsulusha Yesu.duniani kuna mambo wacha waendelee kutimiza unabii.

Anonymous said...

wewe unaongea nini sasa nchi ya Palestine ilikua ya mababu zao enzi ya Nabii Musa..???

Unzijua FACTs,

Musa amezaliwa Egypt?? na amekulia Egypt, sasa Musa wapi na wapi na Palestine ?

Unaosoma biblia upside down, kaisome vizuri..

Anonymous said...

Nabii Musa ndo aliwapeleka wayehudi Palestina kwa amri ya Mungu. Alisema ndo Promised Land yao.

sophiasclub said...

Anonymous 5:14 AM usikarike basi msamehe dada yetu haya mambo wote tunaelimishana. Kitu kingine cha kurekebisha ni kwamba Waisrael hawakuiteka Palestine walikuwa wanarudi kwao. Pia nadhani si sahihi kusema Wayahudi wanamatizo na WAARABU ni bora kusema wanamatizo na WAPALESTINA maana kuna Wayahudi wanaozungumza kiarabu wanaitwa Serphadic Jews (Walikuwa wakiitwa arab jews ila kuondoa contradiction wakaitwa hivyo)- by A Jewish woman