Wednesday, May 14, 2008

Kitoweo BarabaraniHapa kwetu Cambridge/Boston kuna bata kibao. Zamani wazungu walikuwa wanawawinda kwa ajili ya chakula. Siku hizi na supermarket hawana haja nao. Kwanza wamesahau utaalamu wa kuwinda, hata kuisafisha baada ya kuchinja hawawezi. Bahati yao hao bata wamekuwa kama pets tu. Wanabakia kuwaangalia tu.

Hii picha nilipiga leo maeneo ya Alewife, Cambridge.

12 comments:

Anonymous said...

sasa dada huko mbona kwa ajabu ALEWIFE(alewife) mie sikubali tunakula wote kwa wife ndie anajua utamu wa mnyama huyo pekee

Anonymous said...

Bongo haponi huyo! Mlo wa watu 20!

Anonymous said...

Dada chemi naomba nikulize.ivi kwa mfano ukienda kumkamata huyo bata utashitakiwa?kama hapana mbona mnawalazia damu hao bata?

Chemi Che-Mponda said...

LOH! Hapa umkamate tena! Kuna watu wengi wa Third World wanataka kuwala hao bata lakini ni kosa la jinai kuwakamata! Yaani fikiria nashuka kwenye gari na kumkamata. wazungu wangepiga simu 911 na ningekamatwa mara moja! Au kama nisingekamatwa hapo, basi ningekuwa kwenye TV jioni..."Heavyset black woman wanted for catching a goose at Alewife!" Na wangeongeza commentary huyo mama lazima ni katili na an roho ya kutu..kwa nini anakamata bata asiye na hatia!

Miaka ya nyuma hapa Boston waChina walikamatwa wakikamata bata na njiwa maeneo ya Boston Common. Walitiwa ndani!

Ila unaweza kwenda kwenye pori zingine na kuwakamata lakini ni lazima ununue leseni.

Anonymous said...

Marekani mnyama ana thamani kuliko binadamu!

Anonymous said...

huyu bwanyenye anapenda kula jamani yaani kila discussion zake yeye ni kula tu kweli unatabu

Lazarus said...

Ni kweli kwa wenzetu mnyama ana thamani sana. Pia kuna sheria zimewekwa kwa ajili ya kuwinda hao wanyama na zinafuatwa.
Kwa mfano hapa Ontario kuna msimu wa uwindaji wa kila mnyama kama hao bata, swala, nk kwa hiyo kitu cha msingi lazima uwe na leseni kwanza ambayo itakuruhusu kuua wanyama wangapi kwa siku au msimu na pia lazima uende kuwinda wakati wa msimu na si kila siku. Pia kwa mfano hao bata wakati unawinda huruhusiwi kuua jike lazima ni dume tu. Lengo ni kuhakikisha kunakuwa na hao wanyama kwa vizazi vijavywo na pia wanyama wasije zidi idadi.

Constantin said...

nachukia sana kuona watu wanawatukana wamiliki wa blogs, lazima tufahamu kuwa hizi ni blogs zao na wana uhuru wa kuweka habari yoyote wanayoitaka na sisi wasomaji hatujalazimishwa kuzitembelea hizi blogs, hivyo sioni sababu ya mtu kumtukana mwenye blog au mchangiaji yoyote. Nimeona mara kadhaa Chemi akitolewa lugha chafu,naona imefika wakati Chemi ahariri maoni yanayotolewa na wachangiaji kama wanavyofanya bloggers wengine

Anonymous said...

Jamani acheni kelele pia nyumbani tunazo hizo sheria za kuwa na kibali kuwinda mimi baba yangu alikuwa muwindaji mara moja moja just for fun kwahiyo sheria zipo.sio tunashangaa kila kitu tukija nje.tatizo nyie wengine mlifungiwa sana maisha mnafikiri kwenda Kariakoo tu tembeleni mikoa mingine mjifunze

Chemi Che-Mponda said...

Constantin, asante kwa concerns. Huwa nachuja comments kama zina matusi ya nguoni. Na nazipata kweli kweli. Sijui watu wanaona raha gani kutukana matusi ya nguoni au kwa vile wako nyuma ya 'Anonymous' wanadhani hawajulikani. Wanasahau habari ya IP address.

Kuhusu hao bata, kuna siku hapa Boston kijana wa kizungu alikanyaga vifaranga wa bata na gari lake. Alifungwa jela miaka sita! Aliwakanyaga kwa maksudi!

Na kuna siku niliwahi kumwambia mzungu, kama kutatokea maangamizi hapa Marekani na hakuna supermarkets mimi sitakufa njaa. Aliniuliza kwa nini? Nikamwambia, hao njiwa, squirrels, bata etc. wanaliwa! Alishangaa. Nikamwambia unadhani ukienda supermarket huyo kuku anajisafisha mwenyewe na kujita kwenye mfuko. Supermarkets zimeharibu watu hapa. Na hata ukisema umewahi kuchinja kuku wanakuona mtu wa ajabu kabisa!

Anonymous said...

nakubaliana na wewe chemi kuwa ukiwambia wazungu kuwa umewahi kuchinja mnyama unaonekana katili na hata ukipata kesi ya mauaji unakuwa kwenye disadvantage ingawa wanasahau kuwa hapa kwao kuna watu hawajawahi kuchinja mnyama lakini wamawachinja wenzao kikatili hujawahi ona hii inanikumbusha testimony aliyotoa ex-wife wa kupaza
"Kupaza went to trial, where his former wife testified about his abusive behavior. She also alerted police about his background in Tanzania, where families often butchered their own livestock"

http://www.crimelibrary.com/criminal_mind/forensics/k9/1.html

Anonymous said...

Acheni nicheke kwanza, mie ninapoishi nyuma ya hii nyumba unapita mtu, si mkubwa sana lakini si mdogo, basi hukaa dirishani kwangu na kuangalia mabata na bata mzinga wakipita na kucheza hapo mtoni! Basi tukapata flat mate kijana mdogo wa kichina (ametoka China kwenye kamji kadogo), akaanza kusema napenda kula nyama ya bata na mbwa, mwenyewe yuko 'I eat everything'. Ilibidi tumkalishe kitako na kumsomea sheria za hapa kuwa mbwa hawaliwi na akitaka bata basi akatawanunue supermaket. Still bado anawatamani hawa wa mtoni na sungura ndio usiseme wako wa kumwaga yaani ni wengi haswa. Sasa you can imagine watu mate yanavyowatoka na kuwala hawawezi.

Chemi mtu anayekutukana bila kosa wala sababu ana matatizo kichwani kwake, ni ugonjwa wa akili huo haiyumkiniki mtu ukamtukana mtu bila sababu yoyote, kisa kaandika kuhusu bata kwenye blogu yake. Namshauri tu awaone wataalam wa ushauri nasaha ana abusive behaviour au mepata sononi sasa anaona hapa ndio mahala pa kujitibu, na akimaliza kuandika hayo matusi yake anajisikia raha kweli kweli kama wale wanaosubiri kuchapawa viboko kabla ya shughuli. So achana nao, tupo wengine ambao hatulali mpaka tuingie kwenye hii blogu tuone kimejiri nini huko US.

Mdau UK vijijini.