Saturday, August 15, 2009

DHARURA Dallas, Texas - Prisca Mushi

UPDATE - Prisca Mushi Amefariki


Familia ya Bw. George na Bi. Judith Muro wa Dallas TX USA, wanayo huzuni kutangaza kuondokewa kwa mama yao mpenzi, Prisca Mushi, kilichotokea jana August 16, 2009 nyumbani kwao Dallas Texas.
Utaratibu mzima wa mazishi na safari ya kuelekea Tanzania utatolewa baadaye, ila kwa wote watakaoweza, mnakaribishwa nyumbani kwa wafiwakatika anuani hii:1652 Crown Point Dr
Frisco TX 75034
Kwa maelezo zaidi tafadhali
piga simu kwenye namba hii
940 465 5195.
*************************************************************************
Tangazo la dharura Dallas

Ndugu Watanzania,

Kwa niaba ya Jumuiya ya Watanzania waishio Dallas na familia ya ndugu George na Judith Muro ya Frisco, Texas tunapenda kuchukua fursa hii kuwataarifu kuwa mama yetu Prisca Mushi ambaye amelazwa katika hospitali ya UTSouthwestern@Zale, atasafirishwa kurudi nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo. Uamuzi huu umeafikiwa kati ya madaktari, mgonjwa na familia ya ndugu Muro. Taarifa hii ni ya muda mfupi, lakini tunategemea Watanzania wote mliopo popote pale, mtaelewa kuwa hii ni dharura hivyo tunaomba msaada wenu wa hali na mali. Kutokana na hali ya mgonjwa, itabidi aambatane na nesi, ndugu wa karibu na machela (stretcher). Gharama ya kuwasafirisha watu wote watatu kutoka Dallas mpaka Kilimanjaro-Tanzania ni $8000. Hii imetokana na masharti ya waganga pamoja na shirika la ndege. Msaada wako utafanikisha safari hii ambayo tunatarajia iwe jumapili au jumatatu.
Tafadhali wakilisha mchango wako kwenye:

Benki: Wells Fargo
Jina la akaunti: George Muro
Namba ya akaunti: xxxxxxx8424
Anwani ya mwenye akaunti: 1652 Crownpoint Dr, Frisco TX 75034

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Ndugu Muro simu: 940-465-5195

Tunatanguliza shukrani na Mungu akubariki kwa msaada wako.

Simon Nkanda na Abdul Amiri
(Mwenyekiti na katibu wa muda)

No comments: