Saturday, August 29, 2009

Mazishi ya Senator Kennedy


Leo mji wetu wa Boston umejaa viongozi karibu wote wa Marekani. Ma Senator wote wapo hapa, Rais Obama, Bush II, Carter wapo, pia kuna maGavana kadhaa! Kisa, wako kwenye mazishi ya Senator Edward Kennedy. Misa ya kumwombea inafanyika kwenye kanisa kuu la kikatoliki (Our Lady of Perpetual Help) ya ghetto letu, Mission Hill! Ghetto imekuwa ikisafishwa tangu juzi, yaani naangalia kwenye TV nasema kweli ndo Tremont St. hiyo! Lakini sisi makamchape hatuwezi kusogea karibu na hapo! Ulinzi mkali mno! Tunaangalia kwenye TV!

No comments: