Tuesday, August 11, 2009

Semina Kubwa Dallas, Texas


Kwa mara nyingine kupitia mtandao huu tuupendao,ninapenda kuwakaribisha watu wote kutoka Afrika katika mkutano wa kihistoria ambao unaandaliwa na makanisa kutoka nchi mbali mbali za Afrika.Nchi hizi ni Uganda,Ghana,Kenya, Nigeria,Sudan na wenyeji Tanzania. Mkutano huu unawafanya APOSTLE VERNON na Mke wake PASTOR ANN, ambao ni wamiliki wa kituo cha Television cha Agape cha nyumbani Tanzania kuwa miongoni mwa wahubiri wachache kutoka Afrika kuandaliwa mkutano na nchi zaidi ya moja hapa Marekani.

Baadhi ya watumishi kutoka Afrika ambao huwa wanaandaliwa mikutano ya namna hii ni Robert Kayanja kutoka Uganda, Theresia Wairumi kutoka Kenya,Bishop Bismak kutoka Zimbabwe, Bishop Duncan William kutoka Ghana na wengine wachache ambao sijawataja.Kwa ujumla huu ni ukurasa mpya kabisa katika historia ya nchi yetu na kanisa kwa ujumla.Kuanzia wiki ijayo gazeti kubwa la hapa lijulikanalo kama DALLAS MORNING NEWS pamoja na redio station ya KLTY 94:9 FM,Zitaanza kurusha matangazo ya mkutano huu.Tunategemea pia Television ya DAY STAR itamrusha hewani huyu mtumishi wa Mungu pamoja na mke wake siku moja kabla ya mkutano.Ili kuhakikisha tunapeperusha bendera ya nchi yetu vema naomba tuweke uzalendo mbele.Ndugu zangu, naomba mnisaidie kufanya yafuatayo;

-Kwa watanzania ambao watasoma ujumbe huu na wanandugu,jamaa au rafiki katika jiji hili la Texas naomba muwajulishe juu ya mkutano kwa kuwaandikia email au kuwapigia simu kwani huenda wasisome tangazo hili.
-Kama wewe ni member katika FACEBOOK naomba uwakaribishe watu kupitia njia hiyo ya mawasiliano hata kama upo nje ya Marekani.
-Kama una watu maalumu ambao ungependa niwakaribishe na wako huku Marekani naomba unijulishe kwa kuniandikia email.
-Kama utapenda kuhudumu katika mkutano huu kwa njia moja au nyingine pia nijulishe.
-Kama utapenda kuchangia pesa ili kufanikisha maandalizi haya naomba uwasiliane nasi kupitia

JESCA KATARAIYA -972 506 7780 au 972 387 7104(kataraia@hotmail.com)
Kwa mawasiliano zaidi, nipigie au niandikie:

PASTOR ABSALOM NASUWA
UMOJA INT'L CHURCH
12727 DALLAS TEXAS,75230
CELL:214 554 7381, 972 780 2668
FAX:972 991 9460

2 comments:

Michael Abila said...

Aise poti nimesoma kwa masikitiko na mshangao habari ya huyu renowned scholar wa Harvad ku dhalilishwa tena ndani ya compound yake mwenyewe na mapolisi wa kizungu ( sgt Crowley) ambao Obama amewaita ni wajinga. Nashindwa kushangaa kama nchi kama MAREKANI ambayo ni wahubiri wakuu wa haki za binadamu ndiyo hao wa kwanza kuweka rekodi mbaya kama hii kila kukicha. Matukio ya nyuma ya ubaguzi wa rangi tunayakumbuka jinsi weusi tena wa Marekani kwenyewe wanavyo baguliwa sembuse wale wa kuja kama kina Mobhare! Hivi kama hali ndiyo hii nyinyi mna ji contain ama mn fit vipi katika system?

Nimesoma pia blog ya Chemi Che mponda kuhusu bwana moja ambaye anaishi Cambridge karibu kabisa na Harvard alivyouliza na mzungu anafanya nini eneo hilo hali alikuwa akiosha gari pembeni kwenye nyumba yake mwenyewe, na pia namna ambavyo watoto wake wanavyo ogopa kupita katika mitaa ya wazungu baada ya siku moja kuitiwa polisi kuwa ni wezi. Jamani poleni sana kama ndiyo maisha hayo mnayo cope nayo huko sisi tutakuja kutembea na kugeuza tu.Na hili tena kwa new specie/ strain ya ukimwi imegundulika kwa mwanamke aliyotoka CamerĂșn( Africa tena). Jamani huu mzigo wa udhalilishaji utaisha???

Huku Bongo salama tunaendelea kusukuma gurudumu la maisha.

Salaam kwenu mnao-miss Nyamachoma.

Chemponda keep up the spirit. Blog yako idumu!

Michael Abila- Wazo Hill, Dar es Salaam.

Chemi Che-Mponda said...

Mdau Michael Abila, asante sana kwa comments zako. Nitakuwa Bongo hivi karibuni na nategema kufaidi nyamachoma!