Saturday, August 01, 2009

Jumuia ya WaTanzania Gauteng

Mkutano wa kuanzisha jumuia ya watanzania katika Jimbo la Gauteng

Watanzania waishio katika Jimbo la Gauteng (Johannesburg na Pretoria) wanatarajia kufanya mkutano wa kuanzisha jumuia yao tarehe 22 mwezi wa Agosti 2009 jijini Johannesburg.
Mkutano huu utatoa fursa ya kujadili mambo mbali mbali yatakayohusu jumuia hii pamoja na kuchagua viongozi wa kudumu.Watanzania wanaoishi kwenye miji ya Johannesburg na Pretoria ambao wangependa kuwa wanachama na pia kushiriki kwenye uchaguzi wa uongozi wa jumuia wanakaribishwa kuwasiliana na wajumbe wafuatao kwa maelezo zaidi:

Brian Mshana b_mshana@yahoo.com

Laurean Rugambwa bwanakunu@gmail.com

Faustine Ndugulile drfaustinen@aol.comShukrani

KAMATI YA MAANDALIZI

No comments: