Tuesday, August 04, 2009

Tanzanian Summer Get Together New England

Ndugu wapendwa,
Natumaini wote mu wazima wa hali, na shughuli mnaziendesha ipasavyo.

Napenda kuwafahamisha rasmi kwa niaba ya wanakamati wenzangu kwamba Jumuia ya watanzania waishio New England (MA,NH,CT,RI,ME,VT na NJ), ikiwa chini ya mwamvuli wa NEW ENGLAND UMOJA FOUNDATION, INC, inawakaribisha rasmi kwenye ile shughuli ya kuvunja na shoka inayofanyika kila mwaka pale Greenfield, Ma.

Siku ya ijumaa usiku DJ Eddy and DJ Masoud watakuwa THE BOYNE,458 western ave,Brighton,MA
Siku ya Ijumamosi @4PM to 6PM Kutakuwa soka ya iana yake kati ya Boston Na Stars United kutoka Kila kona ya USA
Usiku wa Jumamosi, D.J Rich Maka atafanya vitu vyake pale KickBack Lounge, 1534 Stete St. Springfield Ma. 01109 (Tel. 413-746-0100), atakuwa na mpya kali "fresh" kutoka bongo!. Njoo uburudike mwa'kwetu.......Maisha yenyewe mafupi haya!.
Siku ya Jumapili August 09/2009 ndio Shughuli yenyewe. N.E.Umoja inatimiza miaka Minane tangu zilipoanza sherehe hizi. Njoo wewe, na wale wote uwapendao ufurahi na watanzania wenzako kutoka sehemu mbalimbali, kuadhimisha siku hii muhimu tukikumbuka na kuuenzi utamaduni, desturi na mila za Ki-Tanzania!.
Shughuli hii itafanyika palepale Camp kee-wanee
PLEASE BE ONE TIME

(www.campkeewanee.org), Greenfield MA. 01301.(9AM-9PM).

**ILANI: POMBE NI MARUFKU KATIKA CAMP SITE...PERIOD!!!!**(THE CAMP IS ALCOHOL FREE, AND WE MUST RESPECT THAT RULE PLEASE)

Shughuli hii ni ya aina yake mwaka huu,kwani kutakuwa na mapambano ya mpira wa miguu, (Majeshi hayaruhusiwi Tafadhali).
Boston watambana na ndugu zao wa Leominster/Fitchburg area,na Springfield watapambana na New Hampshire. New Hampshire wamesema watataka kuonyesha mpira wao japo kuwa Springfield wamesema kuwa N.H ni sawa na maharage ya mbeya,Lakini vijana wa N.H wanasema Mpira unadunda huo!!!!
Vile vile mwaka huu, kwa mara ya kwanza kabisa, kutakuwa na pambano la soka kwa watoto wadogo (miaka 4-7). Pia kutakuwa na mbio za watoto wa kiume na wa kike, vijana, kina mama na pia kina baba.
Vile vile Akina Mama nao watakuwa na mbio za chupa,ikifatiliwa na netball , volleyball, na Basketball ya vijana.
Pia kutakuwa, mashindano ya kuogelea, ndugu Baraka Mchome atatuimbia Mashairi, kutakuwa na ngonjera na mashindano ya Fashion show ya aina yake,Bila ya kukosa waimbaji wenye vipaji Akiwemo Uncle

Stephen Tomi.na surprise song Kibao kipya hakijawahi kutoka!!!(Grammy nominee).
Bila Kusahau kutakuwa na Mahanjumati ya hali ya juu,Na wale wanaokula Halali wasiwe na wasiwasi kuna ngo'mbe wa miguu minne ataakungushwa Jumamosi na atachinjika kihalali. Kwa wale ndugu zetu wasio kula nyama,wasiwe na wasi wasi kuna Samaki wa kupaka, Mtaalam Maalum Kutoka Zanzibar,na walaji wa Pilau ya Nyama bata ipo!!!

Shughuli hii itafanyika Jumapili August ,09/2009 palepale Camp kee-wanee, Greenfield MA. 01301.(9AM-9PM).
**ILANI: POMBE NI MARUFUKU KATIKA CAMP SITE...PERIOD!!!!**(THE CAMP IS ALCOHOL FREE, AND WE MUST RESPECT THAT PLEASE)

Kumbuka, ni jukumu lako na langu kuifanikisha shughuli hii, kwani New England Umoja ni wewe na mimi. Ninaomba mfikishe salam hizi kwa ndugu, jamaa na marafiki zako wote, popote waliko hapa Marekani. Kama ilivyo miaka yote, itakuwa ni siku ya furaha kwa watanzania wote, siku ya kujivunia utamadini wetu,Umoja wetu, na upendo baina yetu na marafiki zetu. Njoo wewe, na na wale wote uwapendao upumzike mwa'kwetu!!.
YOU REALLY DON'T WANT TO MISS THIS YEAR'S EVENT

Lakini tafadhali fika kwa wakati

Kwani kutakuwa na supu ya nyama ya Ngombe na kichwa chake
Na wale wanywaji wa supu ya Makongoro vilevile supu yao ipo

Directions: from New York, Jersey City, Connectcut, and Springfield area:
I-91 North, to exit 26-bear and turn Right off the ramp) towards Rt.2A East-Greenfield Center. Proceed, passing Applebee's & Mobil gas station. Go thru 2 sets of Lights (you'll pass 2 gas stations , Dunki'n Donuts &Enterprise). Continue until you see Dillon Chevrolet Dealership. Turn Left on Conway St.. *DO NOT GO TO DOWNTOWN GREENFIELD!*. Drive for exactly 4.3 miles from Conway St. to the sign/entrance at Camp Keewanee (It is a residential area, which will turn into a farm area). Conway st. will turn onto Leyden Rd. Then you'll make a very sharp LEFT turn (almost like a U-Turn) @ the CAMP KEE-WANEE SIGN. Proceed slowly thru the gate, since the road is unpaved one, all the way to the Camp!
From Boston, New Hampshire, Rhode Island, Worcester, Fitchburg, Leominster, and Gadner.....
Take Rt.2 west to I-91 SOUTH , (DO NOT GO TO 91NORTH, You'll find yourself in Vermont!!)
then take Exit 26 (to Rt. 2 West). It is the 1st exit on your Right). Go around the Rotary, and follow the above directions. Gas stations all around Greenfield on either side of the Rotary
* If lost/need assistace, please call:
Siraji 978-413-1164
Richard 413-262-0400
Stephen 413-658-5253
Salum 617-308-2971
Sangiwa E. 1-978-846-9898
Baraka 413-364-8151
Jamal 978-846-6218
Eddy 781-608-0665

*Gas Stations Rt. 5 &10 Both directions, also on Main St. in Greenfield
Please forward these directins to as many people as you can, or visit our website, www.NewEnglandUmoja.net . for more details on friday and Saturday "Pre-soccer celebrations..................KARIBUNI SANA WOTE!!!!!!!!!!!

Katibu N.E.Umoja Foundation
P0BOX 4252
Springfield,MA01101

No comments: