Thursday, August 13, 2009

Shkurani Kutoka New England Umoja

Ndugu wanajumuia.....
Kwa niaba yangu Binafsi,Na hasa kwa niaba ya wanakamati wenzangu Napenda kutowa shukurani zangu za dhati

Kwenu nyonte Mliochangia,Mlioshughulikia,Na hasa kuhudhuria Kwenu Na Kufanikisha Tena Shughuli yetu ya mwaka huu
Kwani Imefunja record kwa idadi ya watu
Bila ya upendo wa moyo wenu wa kujitolea,Shughuli hii isingefanikiwa na Haitafanikiwa...
Baada ya Uchofu wa Tangu Jumapili kuanza Kupunguwa,nimeona ni muhimu kama ada yetu Ahsanteni sana
Kwa yote Mazuri Yaliyotendeka
Tunatowa Shukurani kwa wale wote waliochoma nyama, na wale wote waliojitolea kupika Mahanjumati
Vilevile tunawashukuru wale wote Walioandaa Fashion Show,ilikuwa Babu Kubwa
Tunatowa Shukurani vilevile kwa Ndungu Zetu wa New Hamsher kwa Mara yao ya kwanza kwa kujitokeza kwa wingi

Bila ya kusahau kwa mara nyengine tena Boston wameibuka kuwa washidi,Hawakamatiki
Tutakuwa na kikao cha mwisho cha kufunga Kutathmini shuhuli yetu
kwa Ujumla kitachofanyika Jumapili 2:00PM
August16,2009 kwa Mwanakamati Mwezetu Ahmad Mkambavange 96 Warregan St Chicopee MA 01013
(Tunashukuru Familia Ya Ahmad kwa Kutukubalia kufanya Mkutano huo)Ambao utafatiliwa Na nyama choma

Baada ya kikao tutawatumieni Email kuwajuulisha yote tuliyoyazungumza
Katibu
N.E.Umoja faundation

1 comment:

Mzee wa Changamoto said...

Ni jambo la BUSARA saana kuwashukuru waliofanikisha lolote lile maishani.
Shukrani kwako pia kwa shukrani kwa waliofanikisha na shukrani kwa waliofanikisha kwa kukuwezesha kufanya mlilotarajia.
Blessings