Thursday, August 27, 2009

Mrembo Auwawa Dar!

Sijui na sikuwepo lakini baada ya kusoma hii habari niliona kama hao waliomwua mrembo, Tina Athumani (25), walitumwa kufanya hivyo! Mnaonaje wadau?

**************************************************************
Kutoka ippmedia.com

27th August 2009

Mrembo mmoja anayefahamika kwa jina la Tina Athumani, 25, mkazi wa Jijini, ameuawa kikatili na watu wasiojulikana baada ya kuvamiwa usiku na kucharangwa mapanga na kisha mwili wake kuachwa mbele ya nyumba anayoishi.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mark Kalunguyeye, ameiambia Alasiri leo asubuhi kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, majira ya saa 7:00, pale katika eneo la Kunduchi Salasala ambako ni nje kidogo ya Jiji.

Kamanda Kalunguyeye amesema kuwa mwanadada huyo, amekutwa na umauti baada ya kukubali wito wa kutoka nje ambako alikuwa amesikia mayowe na hivyo kutaka ajue kinachoendelea.

Akasema, mara baada mwanadada huyo kutoka nje, ndipo alipokumbana na watu watatu ambao walimvuta pembeni ya nyumba na kuanza kumcharanga mapanga, pasi na sababu za kufanya hivyo kufahamika.

Hata hivyo, watu hao ambao dhamira yao haikufahamika, waliuvuta mwili wa marehemu huyo pembezoni mwa nyumba yake na kuutelekeza hapo na kisha kutokomea kusikojulikana.

Kamanda Kalunguyeye amesema hadi sasa, Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi ili kuweza kuwapata wauaji na hatimaye kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

No comments: