Sunday, August 23, 2009

Tanzia - Dr. Abdulhashim Masudi

Wadau, nimepokea habari za kusikitisha ya kifo cha Dr. Masudi leo hii. Alifariki mwezi uliopita 27/7/09. Poleni sana wafiwa na hasa mjane wake Da Flora.

Mola Ailaze Roho Yake Mahala Pema Peponi. AMIN.

*************************************************************
Waungwana,

Dr. Abdulhashim Masudi aliyekuwa Mhadhiri Mwandamizi, na Mkuu wa Skuli ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dodoma amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya mkoa wa Dodoma. Maziko yanatariwa kufanyika kesho kijiji kwao Usangi. Kabla ya kifo chake, Dr. Masudi aliwahi kutumikia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Elimu kuanzia mwaka 1985 hadi 2007 alipojiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma.

Inna Lilahi wa Inna Illaihi Raj'uun

Subira

No comments: