Wednesday, August 12, 2009

Peter Owino na Familia Wavamiwa na Majambazi Nzega

Kutoka Michuzi Blog:

HABARI ZA HUZUNI ZINAWAKILISHA KUWA NDUGU YETU PETER ANG'IELA OWINO ALIYEKUWA ANASAFIRI BARABARA KUU YA KATI AMEVAMIWA NA MAJAMBAZI MAENEO YA NZEGA AKIWA NA MKE NA WATOTO WAWILI WA MIAKA MIWILI NA MWINGINE MIEZI TISA NA WOTE KUKATWA NA MAPANGA VIBAYA NA YEYE YUKO MAHTUTI HOSPITALI YA BUGANDO, MWANZA.

NDUGU OWINO ANAISHI UINGEREZA NA AMEWASILI JUZI AKIWA LIKIZO FUPI KUELEKEA NYUMBANI SHIRATI, RORYA.

MAJAMBAZI HAO WAMEWANYANG'ANYA KILA KITU WALICHOKUA NACHO HADI LISHE ZA WATOTO HAO WADOGO WALIOJERUHIWA PIA. POLISI NZEGA WAMETHIBITISHA KUTOKEA KWA TUKIO HILO LA HUZUNI, NA HABARI ZAIDI ZINAFUATA.

PETER OWINO NI MMOJA WA WATU WALIOTOA MAPOKEZI NA HIFADHI KWA WATANZANIA WENGI WALIOKWENDA KUSOMA UINGEREZA TOKA MIAKA YA 1990
TUMWOMBEE NAFUU YA HARAKA.

1 comment:

Anonymous said...

Loh! Majambazi wanaumiza hata watoto wadogo siku hizi! Mimi sirudi nyumbani N'GOO!