Monday, September 07, 2009

Happy Labor Day!


Leo ni sikukuu ya wafanyakazi Marekani (Labor Day). Inasherekewa kila jumatatu ya kwanza ya mwezi Septemba. Ni nafasi kwa watu wengi kupumzika na kutokwenda kazini. Pia ni siku ya kukumbuka waliopigania haki za wafanyakazi Marekani. Zamani watu walifanyishwa kazi kama punda kwa masaa mengi na malipo kidogo. Mimi nimelala mpaka saa 6 leo! Si rahisi kupata nafasi kama hii hapa Marekani, labda uwe tajiri.
Sikukuu Njema!

1 comment:

Anonymous said...

Poleni na Kazi!