Wednesday, September 23, 2009

Mwanamke Afariki Dar Akiwa Anasaka Maji!


Nilipokuwa Tabora Girls (81-83), maji yalikuwa ya shida na mara nyingi tulienda kisimani kuchota maji na kufua nguo zetu. Kuchota maji kwenye kisima kama hiyo pichani ina ufundi wake! Nilipokuwa jeshini Masange JKT nilianguka ndani ya kisima. Nilikuwa peke yangu siku hiyo na sikuwa na jinsi ya kutoka. Kila nikijaribu kutoka naanguka tena mpaka nilichoka. Bahati yangu kulikuwa na afande karibu ambaye alikuwa anafua nguo zake, alinisaidia kutoka. La sivyo sijui ningetokaje maana matope yalikuwa yanateleza kweli maana yalikuwa 'clay soil'.

Hivyo, nimesikitika sana kusikia habari ya huyo mama aliyekufa akiwa anatafuta maji. Huenda alipata matatizo ya moyo. Kujitusha ndoo nzito kichwani ni kazi kweli ukiwa na umri mkubwa.

Lakini naomba niwaulize. Miaka karibu 50 ya Uhuru na bado wananchi wengi hawana maji safi ya bomba, inabidi wachote maji kwenye visima na kukinga maji ya mvua! Wengine wanaletewa maji na boza. Wengine inabidi wanunue maji kwa wanaopita na mikokoteni. Kweli ni maendeleo?


******************************************************
Kutoka ippmedia.com

Mwili wa bibi mwenye umri wa miaka 60, umekutwa ukiwa jirani na kisima cha maji katika maeneo ya Pugu Stesheni Jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Faustine Shilogile amesema mwili huo ulikutwa jana mishale ya saa 12:00 jioni katika maeneo ya Pugu Stesheni, jirani na makazi ya bibi huyo.

Amemtaja marehemu kuwa ni Selina Joseph, 60, mkazi wa Pugu Stesheni.

Akisimulia tukio hilo, Kamanda Shilogile amesema pembeni ya mwili huo kulikuwa na ndoo ya maji.

Amesema chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika na kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Amana.

Hata hivyo taarifa kutoka kwa baadhi ya wananchi wa maeneo hayo zinadai kuwa bibi huyo alikutwa na mauti akiwa katika harakati za kusaka maji ambayo yamekuwa kero kubwa katika eneo hilo.

Kufuatia tukio hilo, wananchi hasa akinamama wameiomba Serikali kuangalia namna ya kuwasaidia.

CHANZO: ALASIRI

9 comments:

Anonymous said...

Nyie ambao tungesaidiana kuleta maendeleo Bongo mko ughaibuni kuendeleza mataifa ya wengine. Mnaishia kulalamika na kuuliza maswali!

Mzalendo said...

Wanaorudi Bongo wana kuwa FRUSTRATED! Sawa wanaenda na moyo mzuri wa kutaka kujenga taifa, lakini wanaserikali wanaweka vikwaza vingi mpaka wanavunjika moyo! Ni kweli ni AIBU KUBWA kuwa na hali tuliyonayo 'Maji Shida' miaka 50 baada ya Uhuru!

Matangalu said...

Hii shida ya maji dawa yake ndogo sana. Introduce English as medium of instruction at primary school level.
Tatizo la maji kwishnei

Anonymous said...

Hela waliokula mafisadi ingetosha kuweka water system mpya Tanzania nzima. Tuna maziwa makubwa, Nyasa, Tanganyika, Victoria halafu tuna shida ya maji.

Anonymous said...

Kila kitu nyumbani standard zimeshuka sasa hivi nasikia watu hata mtoto akimaliza la saba wala hawahangaiki kwenda kuangalia majibu mtoto anapelekwa private, sasa sijui tunaelekea wapi vyuo ndio usiseme, mlimani na sikia Nkuruma hall mwalimu anafundishia ubao na chaki halafu wanafunzi wamejaa mpaka nje mwalimu hawamuoni, hakuna slides, projector au hata LCD wakaazime benchmark basi, jamani kaaazi kwelikweli ndio itakuwa habari ya maji na umeme je?

Anonymous said...

HILI ni tatizo la kupata uhuru mapema ,na viongozi wenyewe wasanii.

Anonymous said...

Polepole tutafika. Tulipotoka na tulipo ni mbali haswaa. Si mnakumbuka miaka ya 70 tulikuwa tunapanga foleni kwenye maduka ya ushirika. Leo tuna supermarkets.
Maji nayo tutapata tu hasa tukiwapata watendaji wazuri na wenye nia safi na nchi yetu.

Anonymous said...

Sasa Mbowe akisema hali ya sasa afadhali enzi ya Ukoloni mbona mnamtukana..!!???

Enzi hizo barabara zilikuwa safi, maji safi, elimu bomba, matibabu bomba, usafiri ndio kabisa barabara na reli mpaka mashambani, viwanda vinazalisha kama kawaida...leo kiko wapi; 90% ya watumishi wa umma ni majambazi..!!

Anonymous said...

Picha kama hizi mwandishi wa habari anaeziweka kwakweli niwakumchinja kabisaa.Kutwa kutuaibiisha kwani magazeti ya hapo Tanzania haya toshi??Nikweli ndio maana kumekuwa na tatizo la internet.