Wednesday, September 16, 2009

Rais Obama Anavyotukanwa Hapa Marekani!Yaani lazima nikubaliane kabisa na Rais mstaafu Jimmy Carter, aliyesema leo kuwa watu wanamfanyia Rais Obama vituko na kutomwonyesha heshima kama Rais.

Mfano, wiki iliyopita Rais Obama alikuwa anatoa hotuba bungeni. Aliposema kuwa katika 'mpango wake wa afya' wasio na makaratasi hawatapewa huduma, mzungu Joe Wilson, alifoka, 'You Lie!" (Mwongo). Wilson alizomewa.

Katika historia ya Marekani hakuna rais aliyewahi kuzomewa akiwa anatoa hotuba Bungeni. Huwa watu wankunja uso na kuguna, lakini kufoka hivyo ilikuw haijawahi kutokea. Watu wanasema Rais Obama angekuwa mzungu, Wilison asingethubutu kufanya hivyo.

Rais Carter anasema hiyo mizozo na fujo tunazaoona kwenye mikutano ya wananchi (Town Hall) ni kutokana na wazungu kushindwa kukubali kuongzwa na mtu mweusi. Hawawezi kutukana Rais Obama waziwazi hivyo wanafanya fujo. Hata kuleta bastola kwenye mikutano anayohotobia Rais Obama.

Niliwaambia ubaguzi bado uko Marekani. Watu walibisha....mnaona sasa?

7 comments:

Anonymous said...

Kwa vile Obama mweusi basi ni witchdoctor?

Anonymous said...

M/mungu ndiye alimchagua kuongoza hao mashetani weupe wanaojiona bora kuliko watu wengine katika hii dunia lkn ukweli utabaki kuwa Obama ni Rais na anawatawala na atawatawala mpaka hapo mungu atakapoamua kama watamuua au kumfanya ashindwe uchaguzi ujao, lkn HABARI NDIYO HIYO keshawatawala hata ingekuwa ni kwa dk 1 tu mbuzi zao. hii yote Miujiza ya mungu kuwaonyesha kwamba wao si lololte wameumbwa tuu km viumbe wengine.

Yaani hapa Utah hiyo kitu pia ipo utaona hata barabarani ukindesha gari wanakufanyia vitimbi fulani tena wanataka ufanye makosa makusudi, lkn yote maisha sote wapita njia tu. tutaambaa ambaa nao km kawa!

Anonymous said...

Hata wakisema nini, Obama ndio rais anaewaongoza whether they like it or not.

Anonymous said...

Binadamu wote ni sawa. Awe mweusi, mwekundu, mweupe , wa njano au wa bluu ni binadamu tu. Na ukijikata damu inayotoka ni nyekundu. Watoe mawazo yao mgando. Anawaongoza na ataendelea kuwaongoza tu

Kaka Trio said...

Kumbukeni lakini sio weupo woote wanamchukia Obama, ni wachache tu tena wengi wa wachache hao ni wale walioko south. Kwa ivo jaribu kutowaweka wazungu wote kwenye kundi moja, kwani bila hao wazungu wangine wazuri Obama asingalikuwa raisi kwa ivo lazima muwapeni credit hao ambao hawakuona rangi ya Obama ila waliona potential zake na wakampigia kura kwa misingi hiyo

Anonymous said...

KACHAGULIA NA WAUPE SIO WEUSI, KUTANIANA NI JAMBO LA KAWAIDA, binti wahitaji kuwa na data zote sio unaandika tuu. Kila rais huwa wanamfanyia vituko hii ndio nchi huru my dear.

Anonymous said...

Mbona George Bush Jr alikuwa anachorwa kama kikatuni mtu si mtu nyani si nyani(Masikio na mdomo), Je hao wachoraji walikuwa weusi?