Wednesday, September 16, 2009

Twiga Maarufu Afariki Dunia Boston!Wadau kuna kilio hapa Boston, MA leo. Twiga 'mcheza sinema maarufu' hapa Marekani kafa hapa Boston! Alikuwa anaigiza katika sinema, The Zookeeper' (stelingi wake Kevin James). Huyo twiga alikuwa anaitwa Tweet. Alimaliza kuigiza katika scene yake ya mwisho huko Franklin Park Zoo. Alikuwa analishwa chakula cha jioni, ndipo kaanguka na kufa papo hapo! Nitauliza wacheza sinema wenzangu wa hapa Boston waliokuwa huko mambo yalikuaje halafu nitawajulisha.

Nzoga ya Tweet itafanyiwa uchunguzi na wataalam wa wanyama pia FBI (Federal Bureau of Investigation) wanachungza kifo cha Tweet. Tweet alikuwa ameigiza katika yale matangazo ya Toys R Us, na sinema za Evan Almighty na Ace Ventura. Watoto wananjua zaidi kama Geoffrey.

Rest in Peace Tweet!
Kwa habari zaidi someni:1 comment:

Anonymous said...

Huyo Twiga walimtoa Mikumi nini?