Tuesday, November 10, 2009

Chemi Kijijini Ilela, Manda

Kaburi la marehemu bibi yangu, Gandula Mary Makatochi. Alifariki 1977 nikiwa mwanafunzi wa Form One, Zanaki Girls Sec.

Manda saa za jioni, mnaona Ziwa Nyasa


Muhogo ni chakula kikuu huko Manda. Hivi sasa kuna ukame. Nashangaa kwenye picha naona kijani kijani, lakini nilivyokuwa huko kila kitu kilikuwa 'brown' shauri ya kukosa mvua! Ugali wa muhogo na dagaa wa Ziwa Nyasa tamu sana.

Nilionana na ndugu wengine sana huko Ilela. Wengi walinikumbuka kwa vile nilikuwa mtundu sana nuikiwa mdogo.

Kaburi la Marehemu baba mdogo, Prof. Crispin Hauli huko Ilela. Alipofariki mwaka 2001 alikuwa mbunge wa Ludewa na pia Naibu Waziri wa Fedha.


Njia kati ya Nsungu na Ilela, Manda Mnaona mlima wa Manda. Inaitwa Mt. Likolombola. (wadau naomba mnisaidie jina sahihi)


Ndugu huko Ilela Manda (Mama Nsumuka)

Niko na Ndugu wengine

Mimi na Bibi Mburuma, siyo bibi yangu lakini ni ndugu wa karibu.
Sara binti wa ndugu yangu Cassian ananisalimia
Niko na Happy, mtoto wa ndugu yangu Mama Rose

18 comments:

Anonymous said...

Mhhmmmm Da Kemi umefaidi kituuu yaani wee acha naina huko ulikuwa unakula ORGANIC food tu mpaka raha.

Anonymous said...

jamani Chemi this is beda si,ku zote ni heri kurejea katika root. goodgirl. Ungelipitia daily ukaonana na jamaa zako wengine. natumaini umeshapona malaria. ingawa sina hakika kama marekani wanajua dozi zetu hapa.

Anonymous said...

Hongera da Chemi kwa kuweza kufika kuwaona ndugu, jamaa na rafiki.

Baraka Mfunguo said...

Nimependa sana na ninaweza kuiita vekesheni ya ukweli. Hakuna kitu "fake" hapo. Watu wengi wanatabia ya "kufake" uhalisia wa maisha ya mahali wanapotoka. Wapo hata wale ambao wanajiita walioelimika toka waondoke nyumbani kwao wamekata mguu labda warudishwe wakiwa ndani ya box hawasemi. Huo ndio ukweli wenyewe. HONGERA SANA DADA CHEMI.NYUMBANI NI NYUMBANI NA "MCHEZA KWAO HUTUZWA"

Unknown said...

Karibu tena Bongo Da Chemi, walisemaga East or West home is best.

Anonymous said...

Picha nzuri mno. Na ninaamini likizo ilikuwa nzuri sana. Nyumbani ni nyumbani hata kuwe shimoni ni nyumbani tu.
Napenda sana ulivyo muwazi na mkweli maana umetuwekea kitu halisi na sio picha za kwenye mahoiteli na maghorofa.

Anonymous said...

Absolutely beautiful! Asante sana kuturudisha nyumbani!

Anonymous said...

We mwali chemponda umenifurahisha sana na umenikumbusha mbaaaaaaali sana hasa hiyo njia ya ilela na nsungu kwani wakati nasoma manda sek ilikuwa mvua ikinyesha na maji yakijaa nyamasheli tu basi hiyo siku shule hamna.next uzuri wa hiyo njia ni msimu wa maembe,ilikuwa ni msosi shuleni matunda njiani wakati wa kurudi VERY GOOD OLD DAYS.Mungu azidi kukupa hekima zaidi ya kuvuya kunyumba.

Mbele said...

Dada Chemi, umefanya mambo mengi mazuri katika maisha yako, kama tunavyoona kwenye blogu yako. Lakini hili la kwenda kijijini na kutuletea hizi picha murua naona limeweka historia ya aina yake.

Kama wadau wengine, nimeguswa sana na hii ziara yako Ilela, nyumbani kwa wazee. Marehemu Dr. Crispin Hauli tulifahamiana, na aliwahi kututembelea tulipokuwa tunaishi pale Ubungo-Kimara. Hii ni mara ya kwanza ninaona picha ya kaburi lake. Nakushukuru sana.

Anonymous said...

Hey Chemi,

Ama kweli "mcheza kwao hutunzwa" umenifikisha vema kwenye dimbwi la uhalalia wa makwetu.Kumbe utajiri ni kujua ulikotoka na wala uliko sasa.Bravo dada Chemi wafundishe na wengine wanaoishia barabara ya Mandera na Titi.

safari ya mwaka kesho tutakuwa wote nitakufikisha hata kwetu Mwakaleli kwenye milima ya Kyejo na Livingstone.

Kila la heri dada mwema.

Mdau Minnesota.

Anonymous said...

Hapo karibu sana na Mlima Likolomboga(kwa kiswahili mboga za majani)ndipo nyumbani kwa babu yangu hayati Jackson Ngalawa,yeye alizikwa kule kwenye makaburi ya kanisani,njia kama unakwenda nyumbani kwa akina Kolimba ukivuka ule mto wenye mba wengi na wakali!

Kwa kweli Manda ni sehemu tulivu na bado watu wanaishi kwa misingi ya ujamaa;maana harusi yako ni yao na msiba wako ni wao pia!

Ipo siku nitarudi na mm kuona kabuli la babu yangu na Manda is in my though forever!

Mdau Oslo-Norway!

Kazungu Samuel said...

Haki hii imenishika.Yaani kumbukumbu nzuri.Maisha huwa hivi Da chemi.

Anonymous said...

Mimi sioni cha kumsifia kwetu kaskazini kwenda home kila baada ya muda fulani ni muhimu tatizo lenu watu wa kusini mnaona Da Chemi kamfanya kitu kipya kwa taarifa yenu ni wajibu wenu kurudi kwenu na kusalimia ndugu acheni kusifia kama vile amegundua machimbo mapya kwanza kwa kukaa muda mrefu bila kwenda amewapotezea sana muda hao ndugu kuacha kazi na kuzunguka nae hadi ziwani angalia hata huyo mtoto hajaenda shule. lakini ukiwa unaenda mara kwa mara wanakuona mmoja wao. Da Chemi wamewaonyesha njia fuateni

Anonymous said...

Mimi sioni cha kumsifia kwetu kaskazini kwenda home kila baada ya muda fulani ni muhimu tatizo lenu watu wa kusini mnaona Da Chemi kamfanya kitu kipya kwa taarifa yenu ni wajibu wenu kurudi kwenu na kusalimia ndugu acheni kusifia kama vile amegundua machimbo mapya kwanza kwa kukaa muda mrefu bila kwenda amewapotezea sana muda hao ndugu kuacha kazi na kuzunguka nae hadi ziwani angalia hata huyo mtoto hajaenda shule. lakini ukiwa unaenda mara kwa mara wanakuona mmoja wao. Da Chemi wamewaonyesha njia fuateni

son of alaska said...

WELL,WELL,WELL-this is why your blog is a must see for any sane person-those photos just swept me off my feet-long may you continue,always looking at the bigger picture.keep it up

Anonymous said...

SASA DADA CHEMI ME NINACHOKUSHAURI BADALA YA KUWAOMBA SERIKALI WAJENGE KIBANDA CHA WATU KUPUMZIKA WAKATI WANASUBIRI MELI,KWA NINI WEWE USIFANYE HARAMBEE UKO UNAPOKAA (U.S.A) UKAENDA KUWAJENGEA PALE ,MNAANA SIDHANI KAMA NI EXPENSIVE HIVYO,UKIWACHANGISHA WALE MA ACTOR NA MACTRESS WENZAKO NA WATU WENGINE WENGINE BAADA YA KUWAONYESHA HIZO PICHA ULIZOPIGA PALE SIDHANI KAMA WATAKATAA JAPO USD 2-5 KILA MTU..
HUO NI MTAZAMO WANGU TU....
MDAU UK

Priscillah Mushi said...

Kweli dada Chemy umenikumbusha mbali sana!! Nilazima mtu akumbuke alipotoka!!

Unknown said...

Safi sana dada