Saturday, May 10, 2008

Chipsi Kuku

(Picha asante Jiachie Blog)

Wadau, mkipata msosi huo Bongo unajiona umeukata! Lakini kinachoniudhi zaidi ni kuwa dume akimnunulia binti chipsi kuku anategemea kupata mavitu! Akina Dada miskubali kuhongwa kwa chipsi kuku!
Tuache utani lakini. Chipsi za nyumbani ni tamu maana ni viazi fresh. Siyo hizi zilizokuwa processed na frozen mara tano kabla ya kufika kwako.
Na hata hapa Marekani tunazikumbuka, hapa Boston miaka ya nyuma tuliwahi kufanya Chips Mayai Party.

8 comments:

Anonymous said...

wewe ulihongwa...sio kila mtu anahongeka na kitu kama chips. Na ukisema mtu anajona sana akila hizo ni uwongo sio siku hizi

Anonymous said...

Si uwongo watu walikuwa wanahonga visichana chipusi kuku. Wengine walipata mimba za chipusi kuku.

Anonymous said...

We Chemi Cola vipi wewe?
Usitupeperushie ndege wetu bure!
We mwenyewe ulipokuwa student mbona ulihongwa chips?
We vipi wewe?

Anonymous said...

Jamani Chemi kila siku na kwambia kwanini unapenda kula sana wewe kutwa kuongela mloo

Anonymous said...

da chemi usikatae unakumbuka enzi hizo niliwahi kukuonga chips tena dume wakati unasoma kisutu usikatae kama uamini nikutumie email nikukumbushe ni mimi b/f wako wa kwanza

Anonymous said...

jamani hayo mambo bado yapo kwa wanafunzi haswa wa secondary na primary hapa bongo,ila siku hizi imeibuka tabia ya wanafunzi haswa secondary kuhongwa simu ya mkononi.

Anonymous said...

Unajua Da Chemi huwa napenda sana changamoto zako, huwa nafurahi maana ujumbe wako huwa haufichi hisia zako na kwa hili nakushukuru sana. Siwalaumu sana dadangu zangu na ama mama zangu kwa sababu ya kitu kimoja. Kwa waafrika tulio wengi hususani watanzania: Chakula, mavazi, na malazi bado ni mahitaji yetu ya msingi kwa mantiki hiyo yeyote anayekujali kwa kimoja kati ya hivyo basi hisia hukupeleka na kuamini ya kuwa huyu mtu ananijali kwa tafsiri nyingine ananipenda. Na daima huwa tunapenda kulipa fadhila na mara nyingi huwa tunaangalia kitu ambacho kimo ndani ya uwezo wetu na ndo maana wengine huidhinisha ngono kama sehemu ya kusema asante. Kwa uzoefu wangu ni mara chache sana kukuta msichana ama mwanamke wa kitanzania kutoka nje (outing) na jinsia tofauti na yeye na kugharamia gharama zote zilizofanywa na rafiki yake wa jinsia tofauti. Maana dhana potofu imesha jengeka vichwani mwa wengi ya kuwa mwanamke ni kutumia tu na mwanaume ni kulipa, na ndivyo inavyoendelea hadi hivi sasa. Wito wangu ni kwamba madai ya haki sawa yangeenda na misingi ya kimapinduzi na kukabiliana na changamoto za kisasa. Mwanamke usiwe wa kwanza kushabikia ofa, kupewa ofa, nawe jikakamue toa ofa, ukifanya hivyo unyanyasaji mwingine usiokuwa wa lazima utapungua kama si kutokomea kabisa. Asante.

Anonymous said...

mimi mke wangu nilimpata kwa gia ya chips mayai,teheteheee,zinasaidia mbona kuwanasa akina dada walafi.
isipokuwa huku uswazini kwetu manzese kuna mtindo wa kuzikaanga kwa kutumia mafuta ya transfoma pia zinawekwa hamira kidogo ili ziumuke.lakn wabongo tunatia ndani tuu.