Tuesday, May 27, 2008

Mtalii wa kiMarekani afa baada ya Kugongwa na Treni Italia


Leo kuna habari za kusikitisha kutoka Italy. Mzee wa kizungu kutoka California, Frank Phel, (74) na mke wake walikuwa wanatalii huko Ulaya. Walikuwa wamemalzia cruise ya meli kwenye bahari ya Mediteranean, na walifika Roma, Italia.

Walikuwa wanasubiri usafiri wa basi asubuhi kwenda Poland. Basi ilikuwa inaondokea huko kwenye kituo cha treni. Ugomvi ukatokea katika ya kundi fulani. Wale wazee walianza kuwa na hofu. Akatokea Mzee wa KiItalia na kuanza kuongea nao na kujifanya rafiki. Akawaletea vinywaji aina ya cappucino. Kumbe mle yule baba alitia madawa ya kulevya. Wale wazee walikunywa zile cappuciono. Walivyolala, yule mzee wa kiItalia kawaibia kila kitu walichokuwa nacho. Kuamka asubuhi, na kuona hawana kitu, yule mzee alimwambia mke wake kuwa anaenda kutafuta mizigo yao, huko bado kalewa yale madawa. Alikuwa anatembea kwenye njia ya treni ndipo aligongwa.

Kwanza polisi wa Italia walidhania kuwa yule Mzee alijiua. Baada ya kuchunguza video ya stesheni waliona yule MwiItalia anawapa zile cappucino na kuwaibia.

Hivi sasa, yule MwiItalia amekamatwa na polisi. Sijui sheria za Italia lakini huyo mshenzi anastahilia dhabu ya kifo! Habari zinasema huko Roma, kuna vibaka na wezi wengi wanaovizia watalii!

Halahala mkienda ugenini.

Kwa habari zaidi someni:


2 comments:

Anonymous said...

Masikini m-babu.hao waitaliano inabidi waimarishe ulinzi kwa watalii na mali zao.huyu mwizi adhabu yake iwe nzito pia.
Zaka

Anonymous said...

shauri yake mwenyewe utakulaje vya kupewa tu na mtu ambae humjui