Thursday, May 22, 2008

Mwalimu Obain amekuwa DEPORTED!

Maandamano nje ya Ofisi za INS mwaka 2005
Mwalimu Obain (pichani)



Yaani kuna ushenzi na washenzi kwenye ofisi za INS (Uhamiaji) hapa Boston! Leo tumepata habari kuwa Mwalimu Obain Attou0man (raia wa Ivory Coast) alikuwa DEPORTED jana. Tena INS walimtorosha kimya kimya!
Kisa, mwaka juzi walipotaka kumdeport wanafunzi wake na watu wengine waliandamana kwenye ofisi za INS Boston. Pia walimwomba Senator Kerry na Senator Kennedy waingilie kusimamisha deportation order. Senator Kerry aliingilia na walitoa amri kuwa apewe residency (haki ya kukaa Marekani). Congress walilalia na ile order ilikwisha juzi, haikupita. Hivyo Mwalimu Obain alivyoenda kureport kama kawaida huko Ofisini INS Boston walimkamata!

Ameonewa huyo kaka! Ni mtu mwema, ni mwalimu mzuri sana wa hesabu Fenway High School (na hapa Marekani kuna upungufu). Ajabu ameoa mMarekani lakini bado wamemfukuza.

Haya sasa kampeni imeanza ya kumrudisha Marekani. Arudi kwa wanafunzi wake hapa. Yaani wanalia si mchezo. Na lazima niseme, siku hizi ni walimu wachahe sana hapa wanaopendwa na wanafunzi.
Kwa kifupi alfika Marekani kama mwanafunzi miaka ya tisini. Aliomba hifadhi (political asylum). Alikosea kusoma tarehe ya hearing kwenye notisi. Ndo walianza kumdeport.

Habari zinasema kuwa amefika salama huko Ivory Coast.

STAY STRONG Mr. OBAIN! You are not a criminal, you are a law abiding, caring and skilled person who does not deserve to be treated like you have. Our children need postive black role models like you!
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

5 comments:

Anonymous said...

Dada kem.kwani huyo mwl aliingia US kama mkimbizi au kama mwanafunzi au kisa hasa ni nini?Na sheria zikoje/zinasemaje kuhusiana na chanzo cha suala lake?isije ikawa jamaa wanafuata sheria na naamini mtu hawezi kuonewa huko sio kama kama hapa bongo.Pia niliwahi kusikia kuwa mtu ambae yuko talented anapewa uraia uko,sasa huyo imekuwaje,pia niliwahi kusikia ukimwoa mmarekani unapewa uraia,sasa hapo vp?ebu tupe ufafanuzi ili tujuwe hayo ya dunia ya kwanza,kwani nasi labda tutafika uko siku moja ya Mungu ni mengi.
ZAKa

Anonymous said...

The article mentions that, "Along the way, though, he misread a notice in which he was given a court hearing date to argue his case, leading a judge to order his deportation". I guess partly it is his fault for not complying with immigration rules in the United States. We all know that the US has enforced strict rules after 9/11 and as immigrants it is our responsibility that we comply with these rules and regulations.

I understand that he has married a US citizen so once his paperwork is processed by USCIS he will be back in the US.

Anonymous said...

The issue of misreading a date is frivolous. But then again Americans believe everything in the world should be 'their' way. This is what happened. In African we write dates 2.3.08 (meaning March 2, 2008). In USA 2.3.08 means February 3, 2008. That is what happened. Cultural difference. But then again black people aren't supposed to have culture,education or anything!

Chemi Che-Mponda said...

Mwalimu Obain, aliingia Marekani kama mwanafunzi. Alivyokuwa anasoma mambo yaliharibika huko Ivory Coast/Cote D'Ivoire, mambo ya vita etc. Aliomba Asylum. Tatizo lilitokea alipokosea tarehe ya hearing. Hivyo waliamuru awe deported. Wala hajanyimwa Asylum. Inavyoelekea atarudi hivi karibuni. Mke wake ni Mmarekani na amefaili mume wake arudishwe.

Watu wanachoshangaa ni kuwa huyo baba ni Role Model kwa vijana weusi na pia ana kipaji cha kufundisha hesabu. Hapa Marekani Role models wa kiume ni wachache kwenye community maana wengi wanaishia kufungwa gerezani na kuwa wauza madawa ya kulevya. Pia watu wa kufundisha hesabu ni pungufu hapa.

Na ajabu zaidi kuna wahalifu kibao kutoka nchi za nje hapa wasio na makaratasi lakini wanakata mitaa tu. Kwa nini hao wasiwe deported!

Anonymous said...

NA YEYE MJINGA HUKO KWAO IVORY COAST KUNA WALIMU WA KUTOSHA HADI AKAFANYE KAZI USA- WANAOJIDAI KUANDAMANA WAMLIPE HUO MSHAHARA AKIWA IVORY COAST NA WAMUWEZESHE AFUNGUE SHULE WAPELEKE WATOTO WAO KAMA NI MWALIMU BORA KULIKO WOTE.