Monday, March 02, 2009

Rais Castro wa Cuba alipotembelea Bongo 1977

Mimi nilikuwa Form One Zanaki Girls, wakati huo 1977. Tulikuwa tunasoma darasani kama kawaida. Ghafla Mwalimu Mkuu katuambia lazima tuende Ikulu kumpokea Rais Castro wa Cuba. Tuliaacha masomo, na kukaguliwa uniform. Tulitembea hadi Ikulu, na tulipangwa ndani ya geti ya Ikulu upande wa bahari. Nakumbuka Castro alikuwa amevaa magwanda ya kijani na mandevu yake halafu alionekana mrefu kweli alivyonipita. Alitupita sisi wanafunzi huko tukishangalia 'CASTRO - NYERERE'! Baadaye kulikuwa na maneno kuwa eti Rais Castro alijialika Bongo ndo maana watu walikuwa hawajajiandaa vizuri. Sijui kama ni kweli lakini. Lakini nikicheki uso wa Mwalimu kwenye hii picha...sijui.

*********************************************************

Kwa habari zaidi soma:

1 comment:

Anonymous said...

Hao walitujengea Kibaha Seconday School. Ilikuwa safi sana lakini sisi hatuna culture ya kumenteni!