Friday, March 13, 2009

Aliyempiga Mzee Ruksa Afungwa Mwaka Moja!


KIJANA IBRAHIM SAIDI A.K.A SULTANI A.KA. USTAADHI AMBAYE LEO AMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA JELA KWA KOSA LA KUMPIGA KOFI HADHARANI RAIS MSTAAFU ALHAJI ALI HASSAN MWINYI WAKATI WA BARAZA LA MAULIDI MNAMO MACHI 10, 2009 KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE HALL JIJINI DAR.

Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Neema Chusi, Amesema kabla ya kusoma hukumu kwamba mahakama imezingatia jinsi mshtakiwa huyo alivyokubali kosa hilo na kuona kwamba anashtahili adhabu hiyo.

Akijitetea kabla ya kuhukumiwa kifungo hicho, mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Said alidai kuwa anakiri kufanya kosa hilo na kwamba anakubali kupewa hukumu na mahakama hiyo.

“Mimi ni kiumbe dhaifu, labda nisiiombe mahakama ila nimuombe mwenyezi Mungu Subhana wataallah kama atataka nitapunguziwa adhabu”alisema Said.

Said ambaye kabla ya kuongea maneno hayo alikuwa akizungumza lugha ambayo haikuweza kutambulika na mahakama hivyo kumfanya Hakimu Chusi kumtaka kubadili lugha hiyo ili mahakama iweze kumuelewa.

Baada ya mshtakiwa huyo kuondolewa kizimbani hapo huku akiwa chini ya ulinzi wa Polisi, ndugu akiwemo mama mzazi wa Said walionekana wakilia nje ya mahakama hiyo.

5 comments:

Anonymous said...

yes mwache aende jela akajifunze ustaarabu, wastaarabu hupigana kwa nguvu ya hoja na siyo magumi na mateke... mshamba tu

Anonymous said...

Hiyo ni damu kwenye sharti?

Anonymous said...

Jamaa kachafuka kweli! Lazima aliminywa magololi!

Anonymous said...

udini dini mbaya sana , maana huwezi kuwa mdini alafu usiwe mbaguzi. ndo hayo sasa yamemkuta jamaa na udini dini wake.

ibrahim said said...

mshamba ni wewe usiejua baya na zuri.jamaa ni shujaa kwani alikuwa tayari kulinda maamrisho ya mwenyezmungu yasihalalishwe na wajinga wasiojua athariya wanayozungumza kwenye jamii.shujaa huilinda hoja yake kwa maneno na vitendo.jela kitu gani hata wakimnyonga ujumbe umefika.