Friday, March 27, 2009

Wasomi Blog

Katika kuendeleza libeneke tumekuja na wazo la kuwaunganisha wasomi wote wa kitanzania popote pale walipo hapa ulimwenguni, wale waliomaliza masomo yao, wale wanaoendelea na pia walimu wanaowafundisha hao wasomi katika vyuo vya Tanzania. Hivyo basi kuna huu mtandao unaokwenda kwa jina hili: www.varsitycollegetz.ning.com. Tayari mwezi mmoja umeshapita toka huu mtandao uingie hewani na kuna wadau wasiopungua 179 hadi leo hii wakibadilishana mawazo kuhusu mustakabadi wa Taifa letu hili changa Tanzania. Karibuni wadau tuunganishe nguvu za hoja ili na sisi tufike wenzetu walipo sasa hivi.

Ahsante sana.

No comments: