Tuesday, March 10, 2009

Wodi ya Uzazi Hospitali ya Temeke


Wakinamama waliojifungua katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakiwa wamejipumzisha kabla ya kuruhusiwa! Ninachojiuliza ni kwamba watu wanazaliana kupita kiasi, huduma ni hafifu ama kuna haja ya kupeana zamu ya kuzaa ili wake zetu wasilale chini?

Wadau kusema kweli hali hii inasikitisha kupita kiasi,kwa mtindo huu hata watoto wanaozaliwa hapo wanaweza kutoka salama kweli katika misingi ya yale magonjwa ya kuambukizana haswa katika msongamano kama huu,wengi watasema ati ni umaskini.! ni umaskini kweli huu.!????.Picha hizi kwa hisani kubwa ya mpoki.blogspot.com/
**********************************************************

Wadau, Mwaka 2009, bado tuna hali mbaya hivyo Bongo. Je, huko chooni/bafuni mwa hospitali kuna hali gani? Je, una uhakika utampata mtoto uliyemzaa au utapata wa mwingine hapo? Khaa! Wanawake wangapi wana share kitanda? Hivi na Mzee Bush si alitoa hela za misaada kwa ajili ya hopsitali hiyo alipotembelea Bongo mwaka juzi?

4 comments:

Anonymous said...

Unakwenda hospitali na uonjwa moja unatoka na ingine.

Anonymous said...

chemi hiyo inaitwa wodi sio wadi. kiswahili ninakupotea sasa urudi nyumbani.

Chemi Che-Mponda said...

Mdau wa 11:50pm, asante kwa sahisho.

Anonymous said...

Asante dada Chemi kwa kuonyesha ukomavu-kiusomi kukubali kukoselewa: naomba ugombee Ubunge wa Temeke, maana huko tungekuwa na viongozi wanaokubali kukoselwa tungekuwa mbali mno, na pengine na wodi nzuri ya wakina Mama