Thursday, March 05, 2009

Yaliyompata Wema Sepetu

Sijui niseme nini. Naona macelebrity wetu wanataka kuanza kuwa na maskandali kama za Hollywood. Sina habari kamili lakini inaelekea Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, alichukua gari ya mwigizaji maarufu Steven Kanumba aka Denzel wa Tanzania, na kuliharibu. Kama ilikuwa ajali si amsamehe na wapatane kuhusu matengenezo? Kwa sasa macho yote kwao.

*********************************************************
mrembo wema sepetu akipewa pole na rafiki yake baada ya kuachiwa kwa dhamana leo mahakamani kinondoni anakikabiliwa na shtaka la kuharibu gari la mwigizaji steve kanumba. mrembo huyu aliyepata kuwa miss tz alikuwa rumande toka wiki iliyopita baada ya kukosa dhamana alipofikishwa kizimbani kwa mara ya kwanza
mama mzazi wa wema sepetu akisaidiwa na nduguye wa kiume ilibidi watumie nguvu wema aondoke nao wao na sio rafikiye ambaye alifika hapo mahakamani

**********************************************************************************


Former Miss Tanzania Charged

2009-03-04

By Hellen Nachilongo

Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu was yesterday brought before the Kinondoni Resident Magistrate`s Court over allegations of malicious damage to a motor vehicle.

Sepetu (20), a resident of Tabata Senene, and Aisha Jumbe (23) appeared before the magistrate in charge Emilius Mchauru to answer the charges levelled against them.

Inspector of Police Nassoro Sisiwaya told the court that willfully and unlawfully the accused maliciously damaged a motor vehicle wind screen with registration no T 993 ASD Toyota RAV 4 brand, the property of actor Kanumba Stephen.

It was alleged that the offence was committed at Magomeni Mikumi area in Kinondoni District on January 1, this year.

However, the accused pleaded not guilty just after the charge was read to them and were returned to remand custody after failing to meet bail conditions.

The court required two reliable sureties working from any recognised or established company to sign a bond of 500,000/- for each of the accused. No body stepped up to rescue the charged duo.
The case was adjourned to March 18, this year when it comes up for mention. Investigation is still in progress.

SOURCE: Guardian
****************************************************************

Wema Sepetu atupwa Segerea

2009-03-04
By Adam Fungamwango

Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu (20), jana alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shitaka la kuharibu mali baada ya kuvunja kioo cha gari chenye thamani ya Sh. milioni moja, mali ya muigizaji wa filamu, Steven Kanumba.

Sepetu alisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Emilius Mchauro, analiyesikiliza kesi hiyo.

Mwendesha Mashitaka Insepkta wa Polisi Nassoro Sisiwaya alidai mahakamani hapo kuwa, Sepetu na mwenzake Aisha Jumbe (23) wanadaiwa Janauari 29 mwaka huu, saa 3:00 usiku huko Magomeni Mikumi, walivunja kioo cha mbele cha gari la mlalamikaji chenye thamani ya Sh 1,000,000.

Ilidaiwa kuwa gari hiyo aina ya Rav 4, lenye namba za usajili T 990 ASD, ilivunjwa kioo na washitakiwa hao na kusababisha hasara ya fedha hizo.

Mahakama iliwataka washitakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. 500,000 kila mmoja.

Washitakiwa hao walikana shitaka hilo, na wamepelekwa gereza la Segerea baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Aidha, mlalamikaji wa kesi hiyo Kanumba hakutokea mahakamani hapo.

Hakimu alimhoji mmoja wa aliyejitokeza kuwa mdhamini kama ana hati za dhamana, ambapo badala ya kuzitoa alidai kuwa amezisahau ndani ya gari.

Kwa kutumia busara, Hakimu Mchauro alimtaka mdhamini huyo azifuate, lakini alitumia zaidi ya dakika tano bila kurejea.

``Hii ni mpya, hakimu anamsubiri mdhamini aliyesahau hati ndani ya gari!.

Labda huyu mheshimiwa alitaka watu wajue tu kama na yeye ana gari,`` alisema Hakimu Mchauro. huyo.

Baada ya kusubiri vya kutosha Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 18 mwaka huu na hapo ndipo pakawa na ugumu wa wadhamini kukubaliwa dhamana kwa sababu tayari hakimu alikuwa ameshasaini.

Sepetu muda wote wa kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa alionekana kutokujali kufikishwa kwake mahakamani hapo, alikuwa yuko kawaida kama vile hakuna kilichotokea na hata baada ya kesi kusomwa alisikika akiwapigia kelele waandishi hasa wapiga picha wampige picha wanazotaka.

Na hata alipotolewa kwenye mahabusu ya polisi kupelekwa kwenye basi la jeshi la magereza, bado alikuwa akipiga kelele kwa waandishi akitaka waandike huku akiwataka askari waache wapiga picha wampige wanavyotaka, lakini haikueleweka alikuwa akisema hivyo kwa hasira au alipenda mwenyewe.

Kwa mara ya kwanza, kesi hiyo ilifikishwa kwenye kituo cha polisi Magomeni mwezi uliopita na Kanumba, ambapo Wema alitiwa mbaroni na kulala kituoni hapo kwa muda wa siku mbili.
Kesi hiyo itatajwa tena, Machi 18, mwaka huu.

SOURCE: Nipashe

Pia soma DAILY NEWS: http://www.dailynews.co.tz/home/?n=632

12 comments:

John Mwaipopo said...

Nimefuatilia sana story ya wema kuswekwa rumande lakini naona akili inanituma vingine kabisa. Uhusiano aliokuwa nao kanumba na wema katika filamu na nje ya filamu sio wa kumsotesha huyu dada (ingawaje naye ana mambo yake) rumande kiasi kile eti kwa kioo cha RAv 4. Siamini. Kuna hisia za visasi, chuki, roho mbaya, wivu, mtimanyongo na maneno yanayoendana na hayo.

Maggie said...

Chemi umenichekesha leo, eti Kanumba aka Denzel wa bongo, seriously!!

Anonymous said...

mwai umenena! uhusiano walokuwa nao si wa kumsotesha wema rumande sbb ya kioo cha gari?! mwanamme gani wewe? watu wanatiwa hasara ya mamilioni katika ugomvi na wapenzi wao lakini yanaisha, unamdhalilisha unafikiri wewe ndo unaonekana umewini? ni ulimbukeni, ufala,ulofa, visasi' chuki mavi na wivu wa kanumba (kwani bado anampenda wema), na hii inaonyesha wazi wameshirikiana na mama wa wema amfunge yeye akamtoe arudi naye nyumbani, lkn umesahau huyo mtu mzima na etna kunguru hafugiki!

Anonymous said...

Itakuwa ni hizo drugs anazotumia huyo BF wake Yusuf Jumbe, na yeye ameshaanza kuzitumia, kwanza ukimuangalia utajua tu. Halafu ugomvi uliozuka kati yake na mama yake hapo mahakamani akimtaka asiondoke na huyo bwana wake bali aondoke na mama yake unaprove kuwa tayari ameshaanza kuathirika na hayo madawa.

Anonymous said...

Da chemi samahani hapa kwa wema si mahala pake lakini kuna habari kuwa mama Anna tibaijuka kashushwa cheo unaweza kutupatia habari kamili pleaaase nakuaminia. Habari za mwanamama shupavu kama huyu ni muhimu kujua

Anonymous said...

Wema na wifi yake Jamila Jumbe walimvamia Kanumba na kumshambulia kwa kipigo huku wakitumia silaha zisizo rasmi kama vyuma, fimbo n.k

Ambapo vurugu hizo zilisababisha kuvunjika kwa kioo cha gari la msanii huyo. Kanumba aliripoti polisi tukio hilo.

Nadhani kilichomkera ni jinsi Wema na wifi yake walivyokuwa wakitamba ktk vyombo vya habari kuwa walimtia adabu Kanumba siku hiyo pamoja na kuharibu gari lake!

Hii ni zaidi ya dharau, mwacheni aende Segerea akapate heshima na kujifunza kuishi na watu!

Nawasilisha!

Anonymous said...

Imagine uko saluni unanyoa nywele, wanakujia wanawake wawili wanakuburuza nje wanakupiga na kukuvunjia kioo cha gari mbele ya wanaume wenzio wamekudhalilisha ungefanyaje? Bora hata alitumia akili ya kwenda kumshitaki polisi kuliko angenyanyua mkono na kumpiga yeye ndio mngeandika mpaka basi. Hakuna mtu aliyemtuma Wema amfuate kanumba alipokuwa, alikwenda mwenyewe na wifi yake na habari za mpiga Kanumba aliona sifa na kusema amemfundisha adabu.
Hayo madawa ya Jumbe ndio yanamchanganya binti wa watu, bora wamuokoe kabla hajazama zaidi aanze kulala majalalani, Madwaya kulevya wacha mchezo kabisa!!!

Anonymous said...

Matatizo ya kiroho ni jambo ambalo linatusumbua watu tulio wengi sana,mara nyingi sana tumedanganyika kwa muonekano wa nje wa mtu husika,lakini tumesahau au kutokujua ya kuwa,kila aliye binadamu,ana matatizo ya kiroho,ina maana kwamba,Wema hapendi kuwa km alivyo,ila anajikuta hivyo kwa sababu hana kinga ya kuweza kujizuia,wa ndugu zangu,dawa ya kila kitu ni YESU KRISTO,kwani unapomwamini,yeye ni mtatuzi wa matatizo yoote yahusuyo roho,kwani yapo matatizo 6 mhm ya wasio mwamini Mungu,ambayo hayaangalii una fanana vipi,ni mzuri kiasi gani nk,kwani km binadamu,tumedanganyika sana na masuala mengi yahusuyo mambo ya jijamii,na tunaweza kuzidi kujitahidi,ila tukumbuke,kila aliye na mwili anacho kikomo cha utatuzi,mhm kwa kila aliye na mwili ni kumwamini na kumpokea Yesu.

Anonymous said...

Hivi Wema Sepetu ana miaka 20 kweli? Ina maana alivyokuwa Miss Tanzania alikuwa na miaka 16?

Anonymous said...

....Ni Utoto tu. WAkikua wataacha.

Anonymous said...

Sasa nimefahamu kuwa Wema anatoa mapenzi yake kweli kweli. Akimpenda mwanamme anampenda kwa moyo wake wote. Hebu angalia, alivyompenda yule bwana mdogo aliyeshindwa kumwekea dhamana lakini ameendelea kumependa kwa dhati.

Inawezekana kuna sababu nyingine kuwa jamaa anatoa muhogo safi, lakini mapenzi ya Wema kweli ni mazito sana. Pamoja na udhaifu wake mweingine, lakini kwa mapenzi namvulia kofia

Anonymous said...

kaka yangu KANUMBA, wewe ulikuwa mkirsto safi sana siku za hivi karibuni sijui ibilisi gani alikuingia mpk ukajikuta unapata kudhalilika hadharani. mi nakushauri kama dada yako wa ktz wewe uanfahamu vizur maandiko i mean bible kama kweli unataka kuoa, biblia inasema mke mwema mtu hupewa na bwana, ebu kaa chini utafakari ni wapi ulipoanguka ukatubu alaf Mungu atakupa haja ya moyo wako, listen wat God tells u. nitapenda kusikia siku 1 umeoa and u are happily married. Mungu akusaidie sana

MS GBennett