Monday, March 30, 2009

Tanzia - Hamidu Bisanga (Mwandishi wa Habari)

Nimepokea kwa masikitiko habari ya kifo cha Mzee Hamidu Bisanga (pichani) kwa ajali ya gari. Nilifanya kazi naye miaka mingi Daily News. Nakumbuka sana sauti ya nzito na ucheshi wake. Ilikuwa bahati tu, nilikutana naye mwaka 2007 mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam. Aliniambia kuwa aliacha kazi Daily News na alikuwa anafanyia sehemu nyingine.

Poleni sana wana familia.

Mola ailaze roho yake mahala pema peponi. Amin.

**********************************************************

Kutoka Michuzi Blog:

Mwandishi habari wa siku nyingi Hamidu Bisanga hatunaye tena. Hamidu, aliyejulikana zaidi kama Hambi, amefariki jana katika ajali ya gari akiwa anaelekea nyumbani kwake oysterbay mtaa wa Chisiza, karibu na iliyokuwa La Dorce Vita. Mipango ya mazishi inafanywa hapo nyumbani kwake na anatarajiwa kuzikwa kesho saa saba mchana makaburi ya Kisutu.

Hambi aliwahi kufanya kazi kwa muda mrefu Daily News akiwa mhariri wa habari kabla ya kujiunga na shirika la maendeleo (NDC), na baadaye kuhamia kampuni ya BayPort. Alikuwa pia mwanachama wa klabu za michezo za SingaSinga ya relwe gerezani na Brake Point ya kijitonyama.

Katika picha hapo juu ni Februari 11, 2009 ambapo anaonekana Kamanda wa mkoa maalumu wa Kipolisi wa Dar es Salaam Afande Suleiman Kova akipokea traksuti 22 alizokabidhiwa na meneja wa masoko na uhusiano wa kampuni ya Bayport Hamidu Bisanga ikiwa ni msaada wa kampuni hiyo kwa timu ya polsi inayoshiriki michuano ya klabu bingwa netiboli kwa nchi za afrika mashariki na ya kati huko zenji.

1 comment:

Anonymous said...

Rest in Peace Brother Bisanga.