Wednesday, March 04, 2009

Mr. Bobos Class - Taarifa za Ajali

Habari ya kazi, napenda kukutaarifu kwamba nimekuwa nikishughulika katika sehemu inayohusiana na ajali kwa zaidi ya miaka 10.

Nimeshuhudia jinsi ajali zinavyowaathiri watanzania wengi kijamii, kiuchumi na kisaikolojia. Hivyo, ili kusaidia katika vita dhidi ya jinamizi la ajali, nimeamua kuanzisha Blog inayoitwa Mr. Bobos Class (http://ajali-traumaclass.blogspot.com), ni blog inayotoa taarifa mbalimbali juu ya madhara ya ajali mbalimbali zitokanazo na matumizi ya Magari na mashine, mbalimbali za kazi .Mbali ya kutoa taarifa pia ina lengo la kuwaelimisha waliopata madhara hayo ni jinsi gani wanaweza kupata msaada baada ya kuathirika kutokana na ajali mbalimbali.Blog hii itaungana na wadau mbalimbali wanaohusika na masuala ya ajali kwa njia moja au nyingine, kuelimisha na kutoa ushauri.

Tafadhali wajulishe watanzania kupitia blog yako juu ya hilo na kwamba michango yao inahitajika ili tuweze kupambana na hili jinamizi la ajali hasa ajali za barabarani.
Asante,naomba pia ushirikiano wako.

Mr. Bobos Class.

1 comment:

Anonymous said...

Da' Chemi nashukuru kwa ushirikiano wako, naona tupo pamoja kupambana na jinamizi la ajali. inasikitisha kuona watanzania wenzetu wanavyoteketea kutokana na uzembe!
Mr. Bobos Class