Thursday, August 20, 2009

Je, Semenya ni Mwanamke au Mwanaume?


Wadau, kuna huyo binti kutoka Afrika Kusini, Caster Semenya (18). Ni mwanariadha na ameshinda katika kukimbia mita 800 katika World Athletic Championships (wanawake). Tena aliwaacha wenzake nyuma kabisa!
Sijui, nikimtazama naona kama anashepu ya kiume, lakini uso mzuri wa kike. Halafu ana sauti besi kama dume! Lakini wanariadha wengi wa kike wana shepu za kidume, matiti na hips hakuna. Kama ni mwanamke nampongeza nadhani tutasikia mengi kutoka kwake. Hivi sasa wataalam wanampima na tutajua matokea baada ya wiki tatu.
Ila najua Afrika kuna watu wanazaliwa na nyeti zote mbili, na wanalelewa kama mtoto wa kike au kiume kwa chaguo la wazazi.
Mnaonaje?
Kwa habari zaidi someni:

11 comments:

Kaka Trio said...

Sio Africa tu wanakozaliwa watoto wenye nyeti zote, nimesoma kwenye net baada ya kuona habari hii, ni kila mahala duniani watoto wanazaliwa na nyeti zote au nyeti zisizojulikana kama walivosema kwenye article nyingi hali hiyo inaitwa "ambiguous genitalia"

Kazi kweli kweli!

Anonymous said...

Huyo kakaa kidume si mchezo.

Anonymous said...

Anaonekana kama CHALII. Labda ni maumbile yake tu.

Anonymous said...

they should test her coz total looks like he.kama atakuwa He south africa sitakuwa na chakuwarahumu coz wamejitangaza vya kutosha duniani kupitia huyu ni faida tosha kuliko hizo medal.

Anonymous said...

It is sad how many have reached to the conclusion she is actually a he without any reasonable evidence. Can you please put a photo of Maria Mutola and see how macsuline the lady is? this is just jealous nothing else

Anonymous said...

Da Chemi, nimesoma mahala kuwa huyo alilelewa kama mvulana halafu mwaka juzi walisema ni msichana. Nitatafuta linki nikutumie.

Anonymous said...

she\he gat Adam apple

Anonymous said...

Mwanaume huyo! Kasuka nywele tu!

Anonymous said...

Huyu ni msichana ila ana testosterone nyingi. Nilikuwa na ndugu yangu mmoja hivi na yeye alikuwa hivyo hivyo, hadi sauti, lakini ana uke kamili!

Anonymous said...

Huyo bila ubishi ni demu kwani ukimuangalia vizuri maeneo ya kiunoni chini kidogo utaona pako flati yani zile zaga za kiume hazipo,kwa wanariadha wengine wa kiume ni lazima zaga zitaonekana zimevimbavimba maeneo hayo but kwa huyu hamna kitu so ni wazi kabisa kuwa ni mwanamke.

Potz.

Edna said...

Sielewi kwa nini tunajidhalilisha na mjadiliano huu. Mama yake amesema yeye ni demu. Sasa maswali mengi ya nini? Kitu mwafrika akifanikiwa tunatafuta sababu za kumshusha. Mimi nakataa mjadala huu. Inabidi kuhimiza kuwa watu wanaomletea huyu dada hizi tabu wawekwe ndani. Ni haki ya huyu binti kufanana kama alivyo na ni haki yake afurahie ushindi wake bila shida, wazungu wanaita hali hii 'stigmatization' na hii kitu ni kinyume cha sheria.