Monday, September 14, 2009

Tanzia - Mohamed Mpakanjia

(pichani marehemu Mohamed Mpakanjia na mke wake marehemu Amina Chifupa)

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.

Kutoka Michuzi Blog:

HABARI ZIMEINGIA SASA HIVI ZINASEMA MOHAMED MPAKANJIA, ALIYEKUWA MUME WA MAREHEMU AMINA CHIFUPA, AMEFARIKI DUNIA MCHANA HUU KATIKA HOSPITALI YA LUGALO ALIKOKUWA ANAPATIWA MATIBABU, DURU ZA KARIBU NA MAREHEMU ZIMETHIBITISHA.

KWA SASA GLOBU YA JAMII INAWEZA KUTOA TAARIFA HIYO TU,
ZINGINE ZITAFUATIA BAADA YA KUHAKIKIWA.


*************************************************************************
Kutoka Lukwangule Blog:

MFANYABIASHARA maarufu na mdau mkubwa wa michezo na burudani nchini, Mohamed Mpakanjia(pichani) amefariki dunia leo katika hospitali ya jeshi la Lugalo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana katika hospitalini hiyo ambayo pia alifia aliyekuwa mkewe Amina Chifupa, Mpakanjia amefariki dunia katika hospitali hiyo majira ya saa saba mchana.
Chanzo chetu cha habari kilichopo katika hospitali hiyo kilisema kuwa mfanyabiashara huyo alifikishwa hopitalini hapo jumamosi iliyopita kutokana na kusumbuliwa na homa ya mapafu (PNEUMONIA).

"Aliletwa hospitalini hapa jumamosi akisumbuliwa na matatizo ya homa ya mapafu. Wakati analetwa alionekana mwenye afya njema lakini hali yake ilibadilika ghafla leo na mauti kumfika," kilisema chanzo hicho cha habari.

Katika uhai wake Mpakanjia alikuwa ni miongoni mwa watu waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya michezo na burudani hasa kutokana na kusaidia wasanii, wanamuziki na bendi nyingi za muziki hapa nchini.

Alikuwa mfadhili mkuu wa bendi ya DDC Mlimani Park 'Sikinde', Tanzania One Theater 'TOT Plus' na pia alidhamini albamu za pamoja za wanamuziki Ramadhani Masanja 'Banza Stone', Ally Choki na kiongozi wa Msondo iitwayo 'Sisi ndiyo Sisi' ya mwaka 2005.

Kwa upande wa sanaa alitoa mchango mkubwa kwa kuwasaidia wasanii wengi wa sanaa ya filamu na maigizo kwa kuwawezesha kifedha kukamilisha kazi zao hizo.
Mungu ailaze roho yake pema peponi. Amina.

Habari hii nimeletewa na Selemani Mkangara.

14 comments:

Anonymous said...

Both were beautfiul people and very wealthy too. Rest in peace.

Anonymous said...

Wamem CHIFUPA nini?

INN LLILAHI WA INE LI LLAHI RAJUN.

Anonymous said...

Wapumzike kwa amani. Inasikitisha. Namwoneahuruma mtoto wao.

Anonymous said...

wamejichifupa wenyewe

Nautiakasi said...

Mungu amlaze anapostahili...! Vinavyowauwa wawenye visent hapa bongo ni Pneumonia na Presha aka heart attack! Na kinacho wauwa wasanii ni malaria na Tb!!! Hivi lini tutaanza tabia ya kuambiana ukweli??? Mbona tumeshindwa kuiga mfano wa Mzee Mandela kwa Mwanawe?
Mtaishia kumalizika kimya kimya kama kuku wa mdondo...heri muambiane tu ili kule alikopita wengine wasipite...hii cheni ni ndefu sana Mungu atulinde!

Anonymous said...

Ni kweli kabisa, kifo cha Mpakanjia kimegusa wengi kama ilivyokuwa mkewe, hata hivyo sina budi kukubaliana na Nautiakasi hapo juu kuwa kulikuwa na gumzo la afya ya Amina na mumewe kwa muda mrefu iliyoambataniswhwa na ugonjwa wa Ukimwi, sasa hivi ukimwi ni kama magonjwa mengine tu hayawi siri tena, ila watanzania tunapenda sana kuficha suala la ukimwi haswa ikija kwa watu maarufu, masikini utasikia wamekufa kwa ukimwi, wanaojiweza wamekufa na Pneumonia au TB au pressure, wengi walihisi Mpakanjia ana Ukimwi kwa muda mrefu, sasa amefariki tukitaka ukweli tutaitwa waosha vinywa, magic Johnson alikuja wazi na ugonjwa wake kwani aliona wale washabiki na watu waliokuwa wanamuangalia kama kioo kwenye jamii wana haki ya kujua, lakini wabongoo wala tena bado wapo wanao husisha ukimwi na uchawi, hivi tutafika kweli, kama kwenye uhai wake aliweka wazi mengi na akifa pia ari iwe hivyo hivyo, ni bora ikawekwa wazi ili wale waliohusiana nae kwa njia au nyingine wakapime kujua hali zao nao hii ndio njia ya kukomesha ukimwi hakuna nyingine ukiachia abstinence.

Anonymous said...

Hao walilogwa! Hakuna cha UKIMWI! Watu waliwaonea wivu kwa vile walikuwa na pesa na mali! Mola amlaze mahala pema peponi. AMIN.

Anonymous said...

Nawashangaa sana nyie wabongo! Kwa nini mnataka kujua kafa na nini? Itawasaidia nini mkijua?

REST IN PEACE MY BROTHER MOHAMED!

Simon Kitururu said...

R.I.P Mkubwa!

Anonymous said...

hivi kweli bado watu wanamawazo finyu eti hawa watu wamefariki kwa sababu ya kulogwa! mpakanjia na mke wake walikuwa ni waathirika wa virusi vya ukimwi, na pneumonia ni moja ya yale magonjwa ambayo huambatana na ukimwi, au mtu amabaye kinga uyake imeshuka sana, mara nyingi inauwa wazee amabao pia kinga yao huwa inakuwa chini. nenda ka google kama huamini. kujitangaza una ukimwi sio kosa jamani, ukimwi ni kama magonjwa mengine tu amabayo hayana tiba kama kansa au kisukari, pengine ukimwi umepata publicity mbaya ndio maana.R.I.P mapakanjia

Anonymous said...

Watu hawana dogo.

Rest in Pest Meddy na Amina.

Anonymous said...

They were a beautiful couple. Can't believe they are both gone. Rest in Peace Mr. & Mrs. Mpakanjia.

Anonymous said...

he da kemi this man was aminas ex husband bana.si mwakumbuka alivyomtaliki amina kwa scandal tele na udaku.Hebu tusipotoshe habari na aina haja ya kumsifia marehemu wala hawasikii.Ukimwi ni hatari kwa maisha yako,eh mola tuusuru,vijana tunaangamia

Anonymous said...

Mtu awezi kufa kwa ukimwi, kwani ukimwi ni kukosa kinga mwilini. Ugonjwa unaweza kuwa wowote, sasa nini cha ajabu, nyie mnosema maneno yasiyo mazuri,,,hamna jamaa au rafki ambae ameadhilika? Wacheni manenu yasiyo na maana. Kwani kufa kwake nyie mmefaidika nini? STOP BEING STUPID MAN!