Tuesday, May 13, 2008

Mafisadi watajwa Bongo

Hivi kweli ni hao tu?

*********************************************************
Kutoka ippmedia.com

Mafisadi: Majina yatua ikulu

2008-05-13

Na Mwandishi wetu, Jijini

Hatimaye ile orodha ya watumishi wa Serikali wanaotuhumiwa kushiriki dili lililoiwezesha kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond kuweza kuingia mkataba wa kifisadi ulioiingiza nchi katika hasara ya mabilioni ya pesa imetua ikulu kwa ajili ya kusubiri hatua za kiutawala kuchukuliwa dhidi yao.

Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda amesema tayari Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo ameshakabidhiwa orodha ya wahusika na na kupewa maelekezo ya kuchukua hatua za kiutawala.

Amesema Bw. Luhanjo anatakiwa kuchunguza na kuwachukulia hatua watumishi wote wa Serikali wanaotuhumiwa na sakata hilo la mkataba `bomu` wa Richmond, lililozua gumzo kubwa nchini.

Akasema Katibu Mkuu Kingozi ataanza kwa kuwachukulia hatua watuhumiwa wote waliotajwa kwenye ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, iliyochunguza mkataba wa Richmond.

Miongoni mwa watuhumiwa waliohusishwa na sakata hilo na kutakiwa kujiuzulu kutokana na kuzembea ama vinginevyo, kutokana na ripoti ya Kamati hiyo ya Bunge ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, Bw. Edward Hosea na Mkurugenzi wa Nishati na Madini katika Wizara ya Nishati na Madini Bw. Bashir Mlindoko.

Kwa mujibu wa mapendekezo ya kamati hiyo teule ya Bunge iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Dk. Harrison Mwakyembe, kigogo mwingine anayepaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu ni Katibu Mkuu wa makosa yao au vinginevyo, kadiri sheria zitakavyoruhusu. ``Maelekezo yote amepewa Katibu Mkuu, suala hili sasa linafikia mwisho kwa kuwa anaandaa hatua za kuwachukulia, kama ni Wizara ya Nishati na Madini Bw. Arthur Mwakapugi.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Pinda, watuhumiwa hao wanaweza kutimuliwa kazini au kupunguziwa madaraka, kutokana na uzito wakuwafukuza kazi au kuwateremsha vyeo, well and good,`` akasema Bw. Pinda. Waziri Mkuu amesema hivi sasa Serikali haikubali kuchafuliwa na hivyo kila anayebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi anawajibishwa.

SOURCE: Alasiri

2 comments:

Anonymous said...

TUNATAKA KUONA WANATAJWA MAJINA YAO HADHARANI NA SIO BLA BLA,WATAKUWA WAPO WENGI TU.

Anonymous said...

Attorney-General, Inpector-General, na Director wa TAKUKURU wote ni walinzi wa serikali.

Hatutegemei mapya yafanyike! Wote ni kuondoa vithibitisho vya ufisadi!

Tunataka "independent" uchunguzi wa Bunge!