Friday, May 23, 2008

Mwanamke aliyekufa Afufuka!Ama kweli maombi yanasaidia. Huko Cleveland, Ohio Bibi Val Thomas (59) alikufa hospitalini. Ubongo wake uliacha kufanya kazi masaa 17, moyo ulisimama mara tatu na mwili ulianza kuganda (rigor mortis) na kubadilika rangi.

Bibi Thomas alikuwa kwenye life support, wakati wanafamilia na madatari wanamua wanfaye nini kuhusu Organ donation, yaani kutoa moyo, mafigo, ini, mapafu nk. kwa ajili ya watu wengine wanayezihitaji.

Walizima mashine, huko watu wanalia. Alishagwa na kusomewa sala za mwisho. Ndipo yule mama alianza kuongea na kufungua macho! DOH! Maombi yalijibiwa. Sasa madaktari wanasema atakuwa mzima tu hatakuwa na aathari zozote mwilini kutokana na kifo.

Bibi Thomas anasema anashukuru kuwa yu hai na kuwa lazimaMungu ana mpango naye, kuna kitu ambacho Mungu anataka afanye.

Kusoma habari zaidi na kuona video BOFYA HAPA:

4 comments:

Anonymous said...

Kweli ni miujiza. Maana mwili ulianza kudecompose kwa rigomotisi.

Anonymous said...

God is able

Anonymous said...

AMEN. Huyo mama bado ana kazi ya Bwana duniani.

Anonymous said...

hakufa hii habari ni ya uongo.....