Wednesday, July 09, 2008

Chachage Seith Chachage - Kumbukumbu


Chachage Seithy Chachage

Uwanjani naingia, kwa mbwembwe zisizo kifani,
Shairi naimba, lisilo na vina wala mizani,
ATB udsm tarehe 8 july usiku, simanzi zilijaa
Chachage Seith Chachage,Njoo barazani Udsm
Miaka miwili imetimia, tangu ulipotuacha,
Unakumbukwa kila mahala si Njombe wala Dakar tuu
Hukuogopa kitu,
Ulikuwa nyota ya muongozo wa haki,
Chachage Seith Chachage, Njoo barazani Udsm
Wanazuoni wanalia, machozi yasiyoisha,
Mbingu gani Ulipo? swali gumu twajiuliza
Kama ile ya kusadikika, Shabani Robert aliyonena?
Chachage Seith Chachage, Njoo barazani Udsm
Njoo barazani tujadili, mustakabali wa Taifa letu
Tunakusubili Nkurumah, tujadili hali ya Taifa letu,
Ufisadi kila mahala, si EPA wala Richmond,
Chachage Seith Chachage, Njoo barazani Udsm,
Wanyonge wanaonewa, si mchana wala usiku
Uchumi unamilikiwa na wachache,umasikini unakithili
Si MKUKUTA wala NEPAD, eti vitatusaidia,
Chachage Seith Chachage, Njoo barazani Udsm,
Utenzi unaishia hapa, niachie hadhila wanene
Wenye kujuvya na wajuvyao, ili wanyonge wapate nafuu
Beti hamsini hazifiki,wala sifananishi na Utenzi wa Shabani Robert
Chachage Seith Chachage, Njoo barazani Udsm,

Umetungwa na;
Godfrey C.L.Mpandikizi
Dar es salaam
email :
mpandikizigcl@hotmail.com
********************************************************************
Kwa kweli Mzee Chachage alikuwa mtu ambaye si rahisi kumsahau. Pale UDSM akiingia ukumbini cheche zinawaka! Ule usemi wa 'Sema Usiogope Sema!' ndiye yeye. Tunamisi ile mbaya. Rest in Eternal Peace.

2 comments:

Anonymous said...

Asante sana Da Chemi. Kweli nchi yetu ilipata hasara na kifo cha prof. Chachage. Alikuwa anawachemsha kweli ndo maana alikolimbwa.

Anonymous said...

Kama ingelikuwa binadamu anakata rufaa ya kifo kinapotokea mbele ya MUNGU naamini tungekata Rufaa turudishiwe Prof. Chachage na wengine ambao kwa namna moja ama nyingine walikuwa ndio wakombozi wa taiffa letu. Mimi binafsi nilimfahamu Prof. Chachage kwa undani kiasi baada ya kufanya nae kazi akiwa mkuu wangu wa Idara pale UDSM. Hakuwa mtu wa majungu hata kwa wafanyakazi wenzake, alikuwa ni mtu straight asiyependa kupindisha mambo na mzalendo wa kweli.
Nuru yake imezimika kama mshumaa uzimikapo uwapo kwenye upapo. Nani atatutetea watanzania Comred Chachage hayupo tena.

kama namwona vile ambavyo angewashughulikia mafisadi kwa kutumia silaha yake aina ya SMG Kalamu kama alivyoshughulikia katika Makuwadi!

Rest In Peace Comrade, Rest in Eternal Peace.