Sunday, July 20, 2008

Mnao lilia kuja Dar Shauri Lenu! - Father Kidevu

Mnao lilia kuja Dar shauri lenu!

Kutoka Father Kidevu Blog

Na Father Kidevu

YALAAAH! Jamanai mjini sasa hapafai na chonde chonde mlio huko mashambani wala msililie kuja jijini Dar es Salaama maana kuna tabu na karaha siku hizi.Nimelia maana sasa ninaona tunakokwenda kwa hizi nauli za daladala na mabasi ya kwenda huko kwa babu na bibi ni hatari.

Wajameni mimi leo nalia na na nimeamua kuropoka niwezavyo juu ya upandaji huu wa nauli hapa mjini na za kwenda makwetu, walahi ni zambi kabisa. sababu naambiwa eti mafuta na gharama za uendeshaji zimepanda, Haya mi mnyonge sina la kusema pandisheni tu hata misosi nayo hivi sasa sii ipo juu kisa mafuta.

Juzi hapa muuza madafu na machungwa wananiambia sasa dafu ni 300 badala ya 250 kisa eti mafuta. Mafuta haya hadi lini? SUMU ya MATRA nayo hiyo imekubali kutuua kwa kupanda kwa mafuta. haya tuendelee.

Ndio! Hatari sana, eti SUMATRA imeridhia baadhi ya nauli za mikoani kupanda, awali nilipo sikia ni nilihisi sasa maskani huko kwa babu watanisahau zaidi maana huu mwaka wa nne sijatia tumu bado naichanga nauri na leo huyu Izraeli Mwakilasa wa hiyo Mammlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini ameongeza tena.Kha!

Nitaendaje kwetu Kigoma kwa basi maana bila ya kuwa na shilingi 200 elfu/= sijaenda na kurudi kwangu Vingunguti. Nauri tu ya kwenda ni sh 84,elfu nikichanganya na msosi inaweza fika 100 elfu na zaidi.Lakini usishtuke hiyo ni ya ndugu zangu walio soma na wakabahatika kufanya kazi BOT au katika mashirika na taasisi kubwa kama Mabenki na kule TRA ambao hupenda kupanda mabasi yaliyo na raha kamili.

Mimi na mwenzangu hapo ambao hufanya kazi katika NGOs za kuzoa taka hapa mjini na kuropoka ropoka kama huku nauri yetu leo imepanda kutoka sh 40,500 hadi 49,000 hadi huko Kigoma.Nauri hii jamani inatugombanisha na kututenganisha na familia zetu.

Akina Masawe, Mushi, Manka, Kekuu, Mboro, Lymo, Mgonja, Mbaga, Msuya, Nendiwe, Nakiete na hata wewe Naelijwa kwenda kwenu kama mpo hapa Disim mtalipa sh 31,000 kama mmesoma na mnamiliki maduka makubwa pale Kariakoo na mnamabucha ya kule Koregwe ya kuuza Astaghafilula.

Ofkozi nitatumia ka eropleni kwenda kwetu Kyaka na hata kwa my frendi Prof. Rwegoshora wa pale Chuo kikuu cha Univasiti, lakini siwezi lipa 75,000 hadi Bukoba.Kaka Kyaruzi, nawewe Rwebangira mmesoma au ndio akina mimi?

Haya wewe Bishanga hukusoma lipa 44,000 tu hadi kwenu Kanyigo.Hahahahaaa! Yeto Msangi, unastuka nini kwani nani kakuita kuja hapa mjini uache mikahawa yako na makilaume kule kwenu, Masawe unalia sana, kama pato lako la chini panda mabasi yale yaliyo na Chesisi za malori ambazo nauri zake sasa ni 18,000 badala ya 14,900.

Akina Lukwangule, Msimbe, Mloka, Malonga, Chamhene, Mwenda na wewe Chuma mnaotoka hapo Matombo, Mgeta, Mlali na kule Gairo hadi Ifakara nauri hadi pale Msavu kituo Kikubwa Mjomba sasa uwe na buku sita (6,000) na sio 5,000 ya zamani.Be Mwakitosi, Se-Fute, Mwatagalile, kule kwetu Lilinga ah! Iringa, sasa kwenda kusalimia home kupata Ulanzi kidogo na tule tumboga twetu tudogo ni sh 29,000 taslim kama unataka kuangalia na video kama hutaki panda Upendo ulipe 17,000.

Wewe nani anasema kwa Akina Somo kule Ntwara na Lindi ni Mbali? Acha habari hiyo kule ukipanda basi swafi Video na Maliwato humo humo utalipa 25,00 tu hadi Lindi na kama utashukia Ntwara lipa 29,000.Jamani wewe bado unataka kuja bandari ya Salama tu, kwa kazi gani kubwa unayotaka huku, kuuza maji au mambo flani…. Tulia huko huko unaweza kushindwa hjata kurudi bush bure maana wengine kwa kuja na malori ama mabehewa ya Ng’ombe na mbio zamwenge ndio wenyewe halafu kurudi soo.Kuna watu wanacheka hapa!

Eti aende huko sijui Kigoma,Moshi na Iringa kuna nini ilhali babu yake mwenyewe kazaliwa Taasisi ya Saratani Ocean Road, nauri ya kuja kutoka Mwenge au Kimara ni 300 mara mbili hapo 600 umeliwa.Kwataarifa yako sasa nauri zote za hapa town zimepanda. Tobah!

Ndio Sekilasa wa SUMATRA amesema hivi sasa ukitoka Mbezi mwisho hadi Kariakoo au Posta utalipa Sh 600, Mwenge Posta sasa utalipa 500 na nauri ya chini sasa ni 300 hakuna kulia lia.Hapo sasa utajiuliza kwa mshahara gani niupatao nauri 1200 kwa siku?

Ebwana ninawazo sasa akili zikiniruka tu nahamisha watz wote weupe pale NHC za Posta na Kariakoo wakaishi Kimara naTegeta halafu WaTz weusi tuhamie zile nyumba za mjini amabazo hata kodi yake ni nafuu.

Watahama tu wao si, wanavipato vikubwa unafikiri watashindwa kukaa nje ya mji na magari wanayo.Waajiri sasa muangalie upya sakata hili la nauri kupanda na gharama nyinge za maisha, muwahurumie hao wanao wazalishia kwa kuwapa nyongeza kama ya SUMATRA.-------------------------------------------------------------------------------------------------

Wasomaji wa gazeti tando hili kuanzia sasa nitakuwa naweka maneno kama haya hapa chini na yeyote mwenye maoni au ushauri aniandike mrokim@gmail.com au sms +255373999.

2 comments:

Anonymous said...

Bado sikubaliani na Neno Israel kutumika kama "Ibilisi" kama mroki alivyoliyumia hapo God damn it.

Anonymous said...

Kwani Israel si yule malaika mtoa roho aliyetajwa katika Biblia au? Pole kwa kukwazika anony but sidhani kama mroki alidhamiria.

Pole ndugu yangu