Wednesday, July 23, 2008

Wabongo wachemsha tamasha la filamu la ZIFF?

Maoni ya Kaka Beda Msimbe Lukwangule Entertainment Blog:

Wabongo wachemsha tamasha la filamu la ZIFF?

There is something very seriously wrong with Tanzania artist and this can been seen katika tamasha la filamu la kimataifa linaloishi ndani ya nchi hii ZIFF ambalo hufanyika Zanzibar kila mwaka. What is wrong jamani!!!!!

Nikiandika katika busati la filamu Habari leo Jumapili nilishawahi kusema jamani tutumbukize filamu huku kwani ipo nafasi ya kwenda maeneo mengine, kukosolewa na pia kuna sababu... lakini Roma haikujengwa kwa siku moja, lazima tusonge mbele.. kwa kujionyesha hadharani.. lakini wapi kw amara nyingine tena tamasha la 11 lina upungufu mkubwa wa local component.

Watu wanatoka all the way from Europe,America and Far East to look for nafasi just to shoo his or her film but Watanzania wanaozalisha filamu kwa fujo kwa sasa wamepeleka filamu hizi zifuatazo na moja nadhani ni ya Da Chemi huko Marekani, Bongoland II ambayo katika entry imeelezwa director wake ni Josiah Kibisa.

ZIFF hufanyika Zanzibar kila mwaka na ni tamasha kubwa kama hutaki filamu yako iingie katika mashindano lakini angalau uonyeshe basi kwa watu:Nini majidai kama hatuwezi hata kufanya kweli kwenye tamasha lenye heshima Afrika Mashariki na Kati?

CEO wa ZIFF mtanzania mwenzetu, manake nasikia wakati ule (zamani) watani zetu wakiingiza filamu kama nyuki tulikuwa tunasema ohh Foreigners hawatutakii mema, sasa huyu mswahili wa Tanga mwenye utaalamu wa filamu ambaye ameishi ughaibuni na anafundisha ughaibuni ametoa wito sana toka mwaka jana akililia filamu za nyumbani lakini mwe wamesema waluguru chilanga komo, yaani unayashangilia maji halafu unakuwa kama huna akili nzuri jamaa wanakucheka, tuache hayo kwani tulikuwa tunazungumzia filamu zilizoingia ZIFF kutoka hapa nyumbani nazo ni hizi zifuatazo:Bongoland ll,Mwanahiti l (oloibon na Layoni)na ll Zawadi ya Fisadi;The Trip ya James Gayo; Sasa na Jando.

Can you imagine?

Watu sijui niwasemeje, labda sijui woga? Haya hatukupeleka hizo sineema zetu je tutaenda kuhudhuria kujifunza manake nasikia kuna manguli wa filamu kutoka Amerika ya Kusini, Amerika kaskazini, Nigeria na Asia ya mbali wanakuja kutufunza mambo ya ABC za utengenezaji sinema, tutakwenda?

Mimi yangu macho.CEO wa ZIFF Dr Martiun mhando amesema kwamba hakuwa na chaguo la kutosha kwani hata zile zilizoletwa hizo zitakazoonyeshwa ni nafuu zaidi na yeye anasema I wonder, kweli hata mimi namuunga mkono I wonder.Hatuwezi kukua kisanii kama tusipokubali kuwa tunamapungufu na lazima tuwasikilize watu watusaidie.

1 comment:

Anonymous said...

hongera san na nakuunga mkono wewe uliyeandika hii article
kilichosemwa ni ukweli hasa ktk suala la WATANZANIA KUKUBALI KWAMBA HATUJUI na hii sio tu ktk sanaa ya sinema hata kwenye mambo mengine mfano SOCCER,ULIMBWENDE,MAMBO YA MZIKI HASA HAYO YA BONGO FLAVA

Kwa maoni yangu sisi watanzania tuna hulka ya kujiona kwanza tunajua na tumeshafika
hatupendi kukosolewa (mkosoaji huonekana mbaya au si muungwana)

Kutopenda kujifunza pia ni hulka yetu mtu akiwa na Canon xl1,Lowel basic kit,Computer 512mb,pinacle au Adobe premiere basi mtu huyo tayari atajiita ni Pictures Inc,Prodution Ltd,Studios na majina mengine makubwa tuu kana kwamba kweli jammaa anajua kutengenza sanaa ya sinema .sasa watanzania wengi utaona kwamba akipata tujiprosumer tool kama hizo nilizotaja basi atajiita yeye ni mfanya sinema atakuwa yeye director,producer, you name it kila kitu
na ataanza na majivuno na kiburi eti ni celebrity producer ukimwambia wewe hujui mimi naona you have a long way to learn bwana endelea kujifunza atakuambia unawivu na maendeleo yake na hasa pesa anazopata kwa kuuza hizo crappy film zake

Pesa .utaona watu wengi wanajiingiza ktk sanaa fulani ili kupata shilingi za haraka na hivyo kupona njaa .hapa suala la kipaji,uwezo na ule mshwassha asilia wa fani hamna .suala la wabongo hapa ni ajira . Una kipaji au huna potelea mbali hii ni ajira kama vile kuwa accountant au kufanya kazi celtel nk

Benchmark/kipimo
watanzania kwa asili hatupendi kusumbua kichwa kwa kujiwekea bar na kujifunza kutoka kwa source ambazo sanaa hii ya film hutengezwa kwa utaalam wa juu sana na kwa kufuata very complex details za kiusanii na teknolojia
hapa nina maana sources za kujifunza kama vile Hollywood au hata hapo South Afrika tuu amabapo tumeona kwa miaka mingi mastudio makubwa ya hollywood wakicollaborate na wa south ktk kufanya kazi zenye ubora
matokeo yake sasa tunakimbilia vitu rahisi na takataka kama filamu za west africa ie Nigeria,ghana nk
kwa misingi hiyo hapo juu na mingine mingi tuu amabayo sijaelezea sioni kwa nini watanzania usichemshe mhando amesema kweli tuache mabo ya zima mato tujifunze si lazima ketafuta digree wapo wengi tuu amabao hawana digriihuko hollywood lakini kwanza wanavipaji pili wajiendeleza kwa njia mabadala kama kununua vitaji .cds,online training,workshop,private short coaching nk hii ni mifano tuu
ahsanteni
raceznobar