Thursday, July 10, 2008

Maneno ya Rev. Jesse Jackson juu ya Obama

Senator Obama na Rev. Jesse Jackson (Picha ya kinafiki)


Reverend (Mchungaji) Jesse Jackson, ni mtu aneyeheshimika sana hapa Marekani na duniani hasa kwa kutetea haki za watu weusi.

Kumbe Rev. Jackson ana usongo na Senator Barack Obama ambaye ni mgombea rais wa upande wa Democrats. Rev. Jackson alikuwa anahojiwa kwenye TV Fox News siku ya jumapili. Alidhani microphone imezimwa, ndo akamwambia huyo mtu aliyekuwa amekaa naye, " Huyo Obama anadharau watu weusi, natamani nimkate mapumbu!"

Duh! Kutoka kwenye mdomo wa mtu wa Mungu.

Rev. Jackson ameomba msamaha kwa maneno yake.

Hivi karibuni, Sen. Obama, alihimiza 'familia' kwa watu weusi wa Marekani. Watoto wengi wamezaliwa nje ya ndoa na akina baba wanakimbia wajibu wao kama wazazi. Jambo ambayo ni kweli. Takrimu kwa watu weusi hapa zinaonyesha kuwa watoto wengi wamezaliwa nje ya ndoa kuliko waliozaliwa katika ndoa.

Lakini tukisoma ndani zaidi si siri kuwa waMarekani weusi wengi wanachukia watu waliotoka Afrika ingawa mababu zao walitoka huko huko. Kuna wakati walisema kuwa Obama si mweusi halisi maana mamab yake ni mzungu na baba yake ni Mkenya.

Kwa habari zaidi someni:

http://firstread.msnbc.msn.com/archive/2008/07/10/1190777.aspx

http://www.smh.com.au/news/us-election/treacherous-sound-bite--jacksons-offcolour-words-about-obama/2008/07/10/1215658037955.html

http://blogs.usatoday.com/onpolitics/2008/07/whats-new-6.html

3 comments:

Anonymous said...

Ni kweli ulivyosema, wanaume wengi weusi hapa USA wanachojua ni kutia mimba tu. Malezi na matunzo wanaachiwa kina mama! Hii ni tabia mbaya sana manake hata kama umekosana na mzazi mwenzio wajibu wa kutunza watoto ni wenu wote wawili.

Anonymous said...

Si msmaha tu wa kutamka maneno mabaya juu ya Obama, Jesse alitakiwa pia aombe msamaha kwa kuamini vilivyo sivyo juu ya mtizamo wa Obama Kwa Wamarekani Weusi.

Maana hapa je microphone zingekuwa zimezimwa angeomba msamaha??????
I am still disturbed by his wrong belief and unwholesome talk!

Anonymous said...

Dada Chemi asante kwa blog yako. Kila siku ni lazima nicheki kama kuna updates zozote kutoka kwako.

Narudi kwenye mada.
Hawa political activists kama "Mchungaji" Jesse Jackson, huwa siwaamini. Ninawaona kama wanafiki. Wanachoangalia ni maslahi yao tu.
Wengi wao utawaona wanatokea kama kuna tukio litakalowaletea publicity ili waonekane kuwa bado ni muhimu. Lakini sijui kama wanaleta mchango wa maendeleo kwa watu weusi leo.

Ni muhimu tuutambue mchango wao na sacrifices walizotoa katika miaka ya 1960 - 70's (Civil Rights movement)... zilikuwa ni kubwa sana na zilifungua milango ya opportunities kwa weusi. Watu walistruggle sana na walipambana na system, hasa huko South.

Sasa huyu Obama ametokea ghafla (it seems), na ameweza kufika sehemu ambayo wengi wao hawakufika. Hii inamuuma sana Jesse Jackson (na wenzake) na sijui huwa anatumia lugha gani kuhusu Obama akiwa katika faragha.


Obama ana mtazamo tofauti. Mama yake alikuwa mtu masikini lakini aliitumia system kujielemisha na kuwaelemisha watoto wake, Soma kitabu chake cha Dreams from my Father utamuelewa Obama ni mtu aina gani.
Obama anajaribu kuwaeleza watu weusi jinsi ya kujikwamua kutoka kwenye umasikini. Anawafundisha umuhimu wa kuwapa watoto mwelekeo katika elimu na maisha yao kwa ujumla. Hii serikali haitafanya hivyo.


Obama yuko kwenye hilo suala la uzazi na majukumu ya uzazi. Single parenthood is an epidemic in this country. Na ukiwa single parent, ni vigumu sana kuondokana na umaskini. Lakini unaweza kuwaelekeza watoto wako wasirudie makosa yako.
Ninachompendea Obama ni vile anavyowaambia watu waache kulaumu wengine na kuanza kujikosoa wenyewe. Hata Bill Cosby ana msimamo huo huo, ingawa watu walimshambulia alivyotoa msimamo huo.

Viongozi wa Weusi (Akina "Mchungaji") huwa wanafundisha kuwa adui wa mtu mweusi ni Mzungu. Kazi yao ni kulaumu. Watu weusi hawachakariki, hawajui umuhimu wa kazi au elimu. Kwa kifupi hawana muelekeo. Na ni kweli wanaonewa, na sehemu nyingine wananyimwa opportunities. Lakini viongozi wao hawatoi solution.

Mimi nasilizia.

Asante Da Chemi