Monday, July 28, 2008

Yanga - Rest in Peace

Upinzani kati ya timu za soka, Simba na Yanga ni kali sana huko Bongo. Yaani nakumbuka watu wamepigana na hata ajali za gari na vifo zimesabishwa na upinzani huo. Lakini si mchezo jamani? Kwa nini watu wanachukulia 'serious'?

Hebu cheki washabiki wa Yanga walivyowatania timu ya Yanga leo! Wamebeba jeneza la Yanga! DUH!

*********************************************************
Kutoka Michuzi Blog:



Yanga yafungiwa miaka 3, na faini dola 35,000

KLABU ya Yanga imefungiwa kushiriki michuano inayoandaliwa Shirikisho la vyama vya soka vya nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kwa miaka mitatu sambamba na kupigwa faini dola za Kimarekani 35,000 kutokana na kugomea mchezo wa kuwania nafasi ya mshindi wa tatu ya michuano ya kombe la Kagame.

Akitangaza uamuzi huo uliofikiwa na kikao cha kamati ya uendeshaji wa michuano hiyo ya Kagame jana usiku mara baada ya michuano hiyo kukamilika, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicolas Musonye alisema mbali na adhabu hiyo ya kufungiwa pia Yanga imepigwa faini hiyo ambayo inatakiwa kulipwa katika kipindi kifupi iwezekanavyo.

Musonye ambaye alikuwa akizungumza huku akionyeshwa kukerwa mno na kitendo hicho cha Yanga kugomea mchezo huo, alisema jambo walilofanya Yanga ni kitendo cha aibu na ndio maana wameamua kuchukua hatua hiyo ili iwe onyo na fundisho kwa timu nyingine.

"Adhabu hii haina suala la kukata rufaa na adhabu hiyo itakuwa ikitekelezwa pale tu Yanga itakapokuwa imefuzu kucheza michuano ya Cecafa na endapo hatalipa faini yake iliyotozwa haitoshiriki michuano yoyote ile ya Cecafa hadi ilipe faini hiyo" alisema Musonye.

Musonya aliongeza kuwa wao kama Cecafa wameliomba pia Shirikisho la soka Tanzania ambao ndio walikuwa wenyeji wa michuano hiyo ya Kagame kwa mwaka huu kuichukulia hatua Yanga kutokana na utovu huo wa nidhamu iliyoonyesha.

Aidha Musonye alisema pamoja na kuwapa adhabu hizo mbili pia italiandikia Shirikisho la soka la Afrika (CAF) kuielezea juu ya kitendo hicho cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na klabu ya Yanga ili kuonyesha ni jinsi gani timu hiyo haina nidhamu.

"Unajua kitendo walichofanya Yanga kinaonyesha upambavu wa viongozi wa klabu hiyo na kwa kweli wana bahati sana mimi si kiongozi wa soka hapa la sivyo ningewafungia maisha" Musonye alisema.

Musonye aliongeza kuwa uongozi wa Yanga mbovu wa Yanga umeiletea hasara Cecafa na TFF kwa sababu ya uamuzi wa viongozi wachache wa klabu hiyo na wasipoangalia klabu hiyo ina hatari ya kuporomoka kabisa katika soka.

Aidha Musonye alikanusha kuwepo makubaliano ya aina yoyote kati ya Cecafa, TFF na klabu za Simba na Yanga za kupeana fedha kama ilivyodaiwa na viongozi wa Yanga na kusema huo ni uongo wa mwaka kwani kanuni za Cecafa zinajulikana wazi kabisa kuwa hakuna suala la timu kupewa mgao wa mechi na timu zote zinatambua hilo.

1 comment:

Anonymous said...

CECAFA ndiyo inapaswa 'to rest in peace! hebu sikiya busara ya kiongozi wake ambaye anajua wazi waandishi walikuwepo wanamnukuu, huyu anaongea kulipresent CECAFA sasa sijui kama kweli tutafika maana hata huyu Maoffside sijui magori naye pumba tuu eti Yanga wamepiga ramli unafiki tuu wanataka kujiosha kwa kuwapaka matope wanakabumbu wa yanga! Wanafiki wakubwa ni viongozi wababishaji wanakurupuka tu na kuongea pumba, hivi kauli zao za jana zina busara yoyote? Shame upon them!

brazatk@yahoo.com
www.mwakilaga.blogspot.com
Tkilager