Saturday, July 05, 2008

Venus Williams ashinda WimbledonMcheza tennis maarufu, Venus Williams, ameshinda taji la Wimbledon tena kwa kumtwanga mdogo wake Serena Williams.

Ni mara ya tatu kwa ndugu hao kugombania taji maarufu ya Wimbledon wakiwa katika top two (washindani wakuu). Na ni mara ya tano kwa Venus kushinda taji la Wimbledon. Serena ameshinda taji hiyo mara mbili.

Tulivyokuwa tunatazama mechi ilielekea kuwa Serena atashinda, lakini Venus alirudi kwa nguvu na kumshinda mdogo.


4 comments:

Anonymous said...

Hao Williams sisters wanaacha wazungu hoi! Hongera Venus na Serena!

Anonymous said...

Si kimchezo tu lakini leo hata pamba za Venus zilikuwa kali kuliko za mdogowe (hawa wadada huwa pia ni wakali wa kutinga vitu vya nguvu siku zote); hata speech yake baada ya kutwaa ushindi ilionyesha udada mkubwa!
Hongereni sana dada zetu. Nadhani kwa wote wawili zawadi zao ni jumla ya zaidi ya pound za Uingereza 100,000 kama sikosei.

Nilijisikia ushujaa wakati nashuhudia hilo gemu kali ambapo kama kawa wachongaji walianza konsipirasi zao eti oh! sijui wamepanga na ushenzi gani!
Gemu lilikuwa halitabiriki mpaka dada mkubwa alipofanya kweli!

Anonymous said...

NADAL NAYE KASHINDA KWA ME-MMOJA MMOJA,INGAWA KWA KWELI FEDERER BADO ANAONESHA KUWA NI CHAMPIONI MZOEFU KWELI MAANA KIWANGO CHAKE BADO KIKO JUU!

Anonymous said...

Media hapa uingereza did not cover the two sisters much at all!! Walie tu media ya uingereza!